Abunwasi,
Siku zimekwenda.
Kwenye maziko ya Abdulrahman Lukongo nilikutana na Hamisi
Kibunzi nikamweleza mazungumzo niliyokuwanayo na marehemu
Athmani Kilambo kuhusu yeye na Arthur Mambeta, Yusuf Salum
na wengineo.
Nikamwambia kuwa Yanga wakiwahusudu sana baadhi ya wachezaji
wa Sunderland na akinitajia majina.
Kilambo anasema, ''Unajua kulikuwa na watoto kule Sunderland wana
mpira mzuri sana kama Kibunzi na Arthur Mambeta na Mzee Mangara
akiwataka awalete Yanga kuongeza nguvu ulinzi na ushambuliaji...''
Kilambo anasema kuwa Mzee Mangara anatuuliza, ''Mimi nikamwambia
kuwa hawa watoto akina Kibunzi na Arthur hata tukiwaleta Yanga
hawataweza kucheza mpira huku wana mapenzi makubwa sana na
Abidjan.''
Siku zile jina lingine la Sunderland ilikuwa ''Abidjan,'' na sijui lilitokana
na nini.
Kibunzi alikuwa hana habari hizi hata chembe.
Akacheka akanambia, ''Kilambo kasema kweli sisi tusingeweza kucheza
Yanga tukipenda sana Sunderland.''
Kilambo alikuwa mzungumzaji wangu mkubwa na akijua mie siipendi
Yanga sasa yeye ikawa kila siku kuniweka roho juu.
Mechi ya Yanga na Simba Zanzibar mwanzoni 1970s, Yanga walitokea
Nigeria, basi kanifata ofisini kunitisha ananiambia, ''Tumekufanyieni
fitna kubwa Zanzibar mnachukiwa kama Hizbu.''
Kweli Zanzibar tukafungwa Yanga wakachukua kikombe.
Kilambo alikuwa muungwana akiingiliana na wachezaji wa Simba vizuri
sana na akipenda sana kumtania Emmanuel Mbele ambae akipenda
kumwita, ''Fullup.''
Waliosimama wa tatu kulia ni Athmani Kilambo, wa tano Abdulrahman Lukongo
timu ya East African Cargo Handling Services
Golikipa Athmani Mambosasa (Simba) kushoto ni Kitwana Manara na pembeni yake ni
Shaaban Baraza
Shaaban Baraza
Akijua mapenzi yangu ya mpira na alikuwa akinipa habari nyingi sana za
Yanga hadi uchawi wa kuloga mechi.
Siku za mwisho za maisha yake tukiswali pamoja msikiti wa Manyema na
akija akiniona hataingia ndani msikitini sharti kwanza aje anisalimie.
Athmani Kilambo (Yanga) kushoto na Abuu (Cosmo)
kulia kwenye khitma Saigon.
Kushoto wa kwanza mbele ni Hamisi Kibunzi, nyuma kulia wa kwanza Arthur Mambeta
anaemfuatia ni Emmanuel Mbele na wa sita ni Yusuf Salum.
[QUOTE="Ndinani, post: 17172926, member: 25719"]Yanga ya AHSANTE KOTOKO: baba watoto Kilambo Athumani akiwa na beki Kapera na Boi Wickens wanapaki bus nyuma; GOALKEEPER Elias Michael na Centre half wao Abdulhaman Juma. Hiyo ndio Yanga ya Mangara Tabu!!![/QUOTE]
Ndinani,
Abdulrahmani Juma hakuwa ''centre half,'' watoto wa mjiini wakiita
''mkoba.
''Yeye alikuwa akicheza mbele na Yanga wakimuita ''Bwana Fedha.''
Abdulrahmani alikuwa na ''gentleman player,'' ''excellent ball control.''
Sasa pale katika alikuwa akigawa mipira kila mahali kama vile ''cashier,''
anavyolipa fedha ndiyo wakampa jina hilo.
Yanga hawakuwa na staili ya kuzuia lango yaani, ''kuegesha basi.''
Yanga walikuwa na wachezaji hodari wa kufunga kama Maulid Dilunga.
Kilambo kwa kuwa alikuwa more ''flamboyant,'' na mpira akiweza kuuchezea
yeye alikuwa ''stopper,'' akicheza mbele ya Kapera kwa kuwa Kapera
alikuwa ''stiff player.''
Kwa ajili hii Kapera akawa, ''swipper,'' yaani akipitwa Kilambo ''striker,''
atakutana na Kapera.
Hii staili wakiita ''double centre half'' yaani ''stopper na sweeper.''
Ndiyo maana Yanga walikuja kupata tabu sana kuwashinda Simba enzi za
Abbas Dilunga na Willy Mwaijibe kwa kuwa walikuwa wanashambuliwa
kutoka pembeni na ma ''winger,'' wenye mbio na wepesi.
Nitakuambia kitu ujue vipi Allah anawapa watu nema zake.
Huwezi amini lakini juu ya kuwa Kilambo alikuwa hana elimu ya sekula
lakini alikuwa hodari wa kujifunza maneno ya Kiingereza khasa yanayohusu
mpira.
Nimejifunza mengi kutoka kwake.
Yeye ndiye akinieleza tofauti ya ''placing,'' na ''shooting.''
Alikuwa akinambia, ''Mwambieni Sabu si kila mahali ni ''shooting,''
mmetukosa kutufunga kwa ajili mipira mingi ambayo angefanya placing
yeye ana shoot inakweda juu. Ile mipira ange-''place,'' yote yale magoli.''
''Hapakuwa na haja ya ''lobbying,'' pale. Yeye angepiga kweye ''box.''
Kilambo alikuwa ''sportsman,'' wakati mwingine baada ya Simba na Yanga
bila kujali matokeo yeye atafanya uchambuzi wake wa mechi.
Utamsikia anawalaumu Simba anasema, ''Nyinyi Simba mechi ya jana ndiyo
mmeiharibu.
Hivi yule Bobeya mnampangia nini?''
Bobea alianza kama mlinda malango Zanzibar kisha akaja Simba kama
''centre half,'' lakini yeye akitumia nguvu sana uchezaji wake.
Kilambo atasema, ''Pale nyuma wangekuwa Arthur na Kibunzi mpira
ungekuwa mzuri sana jana.''
Kilambo hata alipokuja kuwa mwalimu wa mpira baada ya kustaafu soka
timu yake akiifunza kucheza staili ya Kibrazil.
Ulikuwa ukiongea na Kilambo unastarehe.
Utoto wake alikuwa Bagamoyo akivua samaki.
Akikupa strori za uvuvi utashika mbavu.
Jumapili iliyopita nilikuwa na Captain Malik kwa kipindi kirefu.
Captain Malik alikuwa Captain wa Yanga nadhani katika miaka
ya awali ya 1960 na ndiye aliyempokea Kilambo Yanga akitokea
Bagamoyo na kumtia moyo kuwa anaweza kupata nafasi kikosi cha
kwanza.
Juzi alinihadithia mkasa uliotokea Ilala Stadium.
Yanga walikuwa na mechi na wachezaji wote walikuwa weshaingia
uwanjani lakini Kilambo alikuwa kachelewa.
Hakuna aliyekuwa anamjua Kilambo wakati ule hivyo akazuiwa lango
kuu ikabidi Captain Malik aende akampitishe mlangoni.
Sifa moja kubwa ya Captain Malik ni kuwa yeye ni Encyclopedia ya
historia ya mpira Tanzania.
Kushoto: Boi Wickens, Captain Malik, Emmanuel Mbele na Khalid Abeid kwenye Khitma Saigon Club 2001 |
No comments:
Post a Comment