Ahsante Sheikh Mohamed Said. Kichwa cha habari chako kinaashiria dhana iliojengeka potofu kuwa 'Makomred' kwa maana ya wafuasi wa kilichokuwa chama cha Umma Party kilichoongozwa na hayati Abdulrahman Babu (Zanzibar 1963) walikuwa hawaamini dini.Dhana hii iliibuka kwa vile vijana wengi wa ZNP na hata wapinzani wao ASP walikiunga mkono chama cha Umma na walionekana wakifurahia mitaani ujio wa chama hicho kwa shamrashamra na vituko vya aina mbalimbali ambavyo jamii ya wazee wa visiwani hawakuvipenda na viliwakerehesha.
Mimi naona ni zile zile khulka na 'excesses' za UJANA ambazo baadhi yetu wengi huzipitia wakati wa kucharuka na huo ujana.Baadae ujana ukishapita kama moshi na utuuzima kuwasili hali ya mja hubadilika.Wengi huwa 'moderated' na utuuzima na kurejea kwenye silka,tabia na tamaduni za jamii zao asilia.Hili ndilo lililotokea Zbar.Hakuna mwana Umma aliebadilika na kuwa 'atheist' kwa maana halisi ya utamaduni wa wazungu wa Magharibi. Salim
Kaka Salim,
Ahsante sana kwa kunielimisha kuhusu yale yaliyotokea Zanzibar wakati wa kudai uhuru wake.
Nami ngoja nikupe kisa changu na Ahmed Rajab.
Tuko London ni mwaka wa 1991.
Jamaa pale walikuwa wanasoma uradi kila siku ya Alkhamis na kaka yangu Ahmed kwa kuwa mimi nilikuwa mgeni wake akataka tufuatane katika uradi.
Lakini Ahmed Rajab alikuwa na wasiwasi na mimi kuwa huenda I dont subscribe to that kind of Islam.
Basi akanianzia kwa mbali kunisaili kutaka kujua nafata msimamo wangu.
Kama utakumbuka miaka ile mafunzo ya kupinga Maulid nk. yalikuwa ''fever pitch,'' huku kwetu.
Nikamjibu kuwa mie nikiwa Dar es Salaam kila Alkhamis nakuwa katika uradi Masjid Ngazija siku zile uradi ukiongozwa na marehemu Sheikh Aboud Maalim.
Basi tukenda kwenye uradi nyumbani kwa Sheikh Mohamed Abubakar High Bennet na huko nikakutana na jamaa wengi mmojawapo akiwa Sheikh Mlamali Adam.
Lakini nami kilichonistaajabisha ni kuwa mbona wale makomredi wamegeuka kuwa masufi?
M
No comments:
Post a Comment