Thursday 8 September 2016

MOHAMED ''MSOMALI'' HASSAN: TAAZIA KUTOKA KWA KHERI MAULID CHOMBA KWA NIABA YA VIJANA WAPENDA SOKA KARIAKOO


Utangulizi

Rafiki yangu Kheri Maulid Chomba wa Kariakoo kaniletea taarifa ya msiba wa Mohamed Msomali na kwa haraka ya ajabu akaniandikia pia na taazia ambayo ameniambia walikaa vijana wapenda soka wa Kariakoo wakakumbusha enzi wakati Mohamed Msomali alipokuwa Dar es Salaam akicheza mpira Yanga kisha Cosmopolitan na baadae kuwa kocha wa Pan African. Nimeuomba aniruhusu nitumie taazia yao nay eye kwa niaba ya wenzake  amenikubalia.


Photo
Mohamed Msomali
(Picha kwa hisani ya Vijana Wapenda Soka wa Kariakoo)

[10:33pm, 08/09/2016] Kheri: Mungu ampumzishe kwa amani mzee Mohamed Hassan Msomali. Taifa limepoteza muumini mwingine wa ukweli wa soka. Aliyefanya soka  kwa mahaba na si shinikizo lingine.
[10:34pm, 08/09/2016] Kheri: Innalillahi. Wachache wanaomjua Mohamed Msomali. Ile TFF akuna anaemjua.
[10:34pm, 08/09/2016] Kheri: Ile Pan African tishio ya 1981/82 Coach Msomali
[10:34pm, 08/09/2016] Kheri: Half back 4 ya uhakika . Akili tupu
[10:34pm, 08/09/2016] Kheri: Wahid. Pan African ya 1982 iliyotwaa ubingwa Coach alikua Mzee Msomali. Ni kikosi bora kwangu kwa muda wote kila position ilikuwa na watu 2.
1. Juma Mensha/Idd Msakaa
2. Mohamed Mkweche/Jafar Abraman
3. John Fire/Hamis Swedi
4.Tenga/Saad Matheo.
5.Jella Mtagwa/Kassim Matitu.
6.Adoph Rishard/Carlos
7.Gordian Mapango/Omar Said
8.Hussein Ngulungu/Roma Mapunda
9.Abdallah Burhan/Ally Catolila
10.Mohamed Yahya/Peter Tino
11.Ibrahim Kiswabi/Wazir Ally.
 
Hii ni team bora katika Leauge Kuu kwa mtazamo wangu. Baada ya 1975. Yanga kuzaa Pan African.  Simba kuzaa Red Star
[10:34pm, 08/09/2016] Kheri: inawezekana kabisa ikawa ndio timu bora
[10:34pm, 08/09/2016] Kheri: ule ukuta wao ulikuwa wa chuma
Pondamali
Mkweche
John Faya
Tenga
Jellah 
Adolf Rishard
[10:34pm, 08/09/2016] Kheri: ni noma
[10:34pm, 08/09/2016] Kheri: huyu Mohamed Yahaya "Tostao" alienda kucheza mpira Austria pamoja na Kassim Manara.

No comments: