Monday, 28 November 2016

KUTOKA KUMBUKUMBU ZA JF: KIFO CHA ABDULLA KASSIM HANGA


Katika moja ya mjadala mkali sana kuhusu Abdulla Kassim Hanga niliandika maneno haya:

''Kuwa Hanga ndiye aliyekuwa kinara wa Mapinduzi ya Zanzibar hili si jambo lenye utata tena. Ikiwa hivyo ndivyo Hanga hatoweza kuutua mzigo wa roho zilizopotea katika mapinduzi hayo. Ikiwa Hanga atalaumiwa kwa vifo vya maelfu ya Wazanzibari nani alaumiwe kwa umauti uliomfika Hanga tena kwa kuuliwa kishenzi kwani hapana neno zaidi ya hilo linaloweza kutosheleza kuelezea jinsi Hanga alivyouliwa. Kichekesho kikubwa ni kuwa wale waliopoteza roho kwa hiyo kutangulia mbele ya haki, yao yalikuwa yamekwisha. Lakini kwa wale wajane na mayatima waliobakia nyuma wakihangaika, kifo cha Hanga na wenzake katika wale waliofanikisha mapinduzi kuuliwa kwao kulikuwa muujuza wa aina yake, uchawi usioelezeka nani fundi wake. Ilikuwa vigumu kueleza. Ingeeleweka vyema endapo kisasi cha kuitoa roho ya Hanga kingetimizwa kutoka katika mikono ya maadui zake waliopinduliwa. Haikuwa hivyo.


Wale wajane na mayatima walililipiziwa kisasi na watu waliokuwa maadui wakubwa wa waume na baba zao waliopinduliwa. Vipi Hanga kiongozi mkuu wa mapinduzi aje kuwa adui wa mapinduzi yenyewe kiasi cha kuwa hukumu ya kumtosheleza haikuwa kifo tu bali kifo cha kishenzi. Fikra ya Hanga ilikuwaje alipokuwa peke yake ndani ya selo Ukonga Prison 
usiku ukimpita bila ya hata lepe la usingizi akiwaza yanayomkabili. 

Nini kilikuwa kikipitika katika ubongo wake wakati wauaji wake walipomtoa katika selo yake na yeye akawakabili ilhali aikijua kuwa walikuwa wamekuja kuitoa roho yake. Fikra yake ilikwenda wapi? Ilikwenda kwa Sultan Jamshid bin Abdullah aliyempindua na kwa Masultani wengi waliopita ambao wameiaga dunia mikono yao ikiwa haina damu au kwa Abeid Amani Karume aliyeingia madarakani kwa mapanga ya Wamakonde kutoka Tanganyika, wakata mkonge kutoka Tanganyika wakifanya kazi mashamba ya Sakura na Kipumbwi? Fikra ya Hanga ilielekea wapi? Kwa Nyerere aliyemsaliti?

Hakika ni wazi hakutegemea mapinduzi aliyoyasisi yangemgeukia na kuwa sababu ya yeye kutolewa roho kwa kuuliwa kishenzi. Jambo la kusikitisha ni kuwa hadi pale alipokamatwa na kuwekwa jela Ukonga na kufikishwa mbele ya mkutano wa hadhara na kuadhiriwa na Julius Nyerere tayari alikuwa keshapoteza kila kitu achilia mbali dira ya mapinduzi aliyokusudia ingeongoza Zanzibar. Hanga hakuwa kamwe na uwezo wa kumfanya Karume lolote kwani Karume tayari alikuwa chini ya mbawa za Nyerere ngome ambayo Hanga asingeweza kuitikisa achalia mbali kuibomoa. Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa hirizi tosha ya kumkinga Karume.

Katika mkasa wa kuuliwa kwa Hanga ndipo msemaji mmoja akasema,
Maiti toka makaburini mwao walionyesha ujuzi wa kufanya miujiza na uchawi wao kwani laiti kifo cha Hanga kingesababishwa na wale waliopinduliwa kisasi chake kingekuwa cha kutisha. Ilibidi Hanga kwa miujiza ya maiti zile auliwe na wale wale aliowaweka madarakani watu ambao hapakuwepo na sababu ya wao kumuona adui. Halikudondoka chozi kwa kifo cha Hanga. Kila aliyepata mnongono wa kuuliwa kwake alikuwa kimya kama vile taarifa ile ya kifo haimuhusu.''


=======================
Mchangiaji mmoja anaejitambulisha kwa jina la EMT alichokoza mada kwa bandiko hili hapo chini:
[​IMG]

In 1969 after the trial of fourteen who were accused of coup planing by Karume followed by the execution of four defendants. Two of this are the First Vice President Hanga and the Ambassador to United States Mr Othman sheriff , no record of the trial proceeding no details of the court proceeding no composition of proceeding or evidence have ever been provided and the Tanzania Government had to date been unable or unwilling to provide the details to the family of the this individuals if were executed.

President Julius Nyerere was pictured on January 16th when he addressed an open air rally where the detained former Tanzania Minister and Vice-President of Zanzibar was brought to face the people. Mr. Kassim Hanga (seated between two police officers) is under detention with a number of other top Tanzanians after allegedly boasting that he had been called from voluntary exile in Guinea to lead an army coup on Zanzibar.ZANZIBAR REVOLUTION JOHN OKELLO, KARUME AND ABDALAHMAN BABU - YouTube

Karume did not like people who were educated; he did not trust them, so most of those from the ASP who were imprisoned were educated, like Othman Shariff. Shariff and Karume were rivals within the ASP before independence; after the revolution, Shariff was first appointed minister of education and then Tanzania's ambassador to the United States. It is said that, on a visit to Tanzania, he was seen taking photographs of the State House, and that was enough for the RC to accuse him of being an imperialist stooge and a CIA spy trying to help the Americans take over.

The authorities arrested him but released him after Nyerere intervened. He was reduced to serving as a veterinary officer in Iringa on the mainland. Later, some members of the RC were sent to arrest him and bring him back to Zanzibar, but Nyerere intervened again. They eventually convinced Nyerere to hand Shariff over, and once he arrived in Zanzibar, that was the end of him. 

Abdallah Kassim Hanga was Russian-educated and very popular among younger ASP members. After the revolution, he was named vice president but, after the union, was transferred to Dar es Salaam. Hanga eventually lost favor with Nyerere because he was very close to Kambona, Nyerere's minister of foreign affairs and defense. During the Tanganyikan army mutiny of 1964, it was Kambona who went to talk with the soldiers, while Nyerere remained in hiding. After Kambona fell out with Nyerere and went into exile, Hanga lost favor, because he was so close to Kambona. After Hanga was removed from the cabinet, he went to live in Conakry, Guinea, because he had married a Guinean woman.

After some time, Nyerere sent a delegation to President Sekou Toure, asking him to convince Hanga to come back to Tanzania, where he would be safe. Unfortunately, when he returned, he was arrested and publicly humiliated. At a rally at Mnazi Mmoja in Dar es Salaam, Nyerere had Hanga brought there in handcuffs. Nyerere publicly insulted him and then later agreed to send him to Zanzibar, where Hanga was tortured and killed.

Chanzo: DIRA YETU: TUMKUMBUKE MZALENDO MWANAMAPINDUZI YA ZANZIBAR ABDULLA KASSIM HANGA

Waweza pia kupitia kitabu cha Race, Revolution, and the Struggle for Human Rights in Zanzibar: The Memoirs (2009) By G. Thomas Burgess, Ali Sultan Issa, Seif Sharif Hamad hasa Chapter Five inayoenda kwa title: Karume The Terrible.

No comments: