Ramadhani Darsa Dar es Salaam, Lumumba Avenue Sharif Sayyid Muhammad bin Sharif Saiidi Albiidh kushoto akifuatiwa na Sheikh Burhani na Sheikh Abdallah Jabir |
Leo tarehe 23 Mfungo Tano 1438 tunakumbuka siku aliyoelekea
kwa Mola wake mwanazuoni huyu mahiri Mungu mrehemu mthibitishe makao yake
peponi kazi yake aliyoifanya duniani hana mfano wake Sharif Sayyid Muhammad bin
Sharif Saiidi Albiidh ni mwanazuoni wa Afrika na dunia kila unapomtazama
kila upande alitimia katika elim usiseme kasomesha mpaka mwisho wa uhai wake
kasimamia ujenzi wa muskiti zaidi ya 100 madrasa zaidi ya 100 katika uhai wake
alipata kuhesabu watu aliwasilimsha kwa mkono wake mpaka wakafika elfu 3000
akaona awache safari za daawa ndani ya Kenya Uganda Tanzania Sudani Kusini Somalia
Kongo Burundi Rwanda Misri Saudia Yemen uk Mashariki ya Kati Pakistani na maeneo
kadha ni mwanazuoni alietunga vitabu vya qaswida vitabu vya fanni kama Usulilfiqhi
Ulumil Qur ani nk amesahihisha vitabu mbalimbali ametunga vitabu vya lugha
tafsiri vitabu vya hoja mbalimbali istoshe katunga selabas muhim saana katika
maajabu mzee huyu ameanza kusomesha akiwa na umri wa miaka 13 ajabu kabisa katika
eneo la daawa yeye ni Mkenya kwa uraia lakini akija Tanzania Uganda utashangaa
yeye ndiyo akiwapeleka masheikh wa maeneo hayo katika vijiji vya maeneo yao
ajabu alikua mpenzi wa Mtume kisawasawa kwa mwaka akihudhuria maulidi zaidi ya
mia tano ikifika Ramadhani darsa zake kila kona katika nchi mbalimbali Ramadhani
nzima kwake akipita siku mbili tena kwa ratiba ya darsa nk ni ajabu maisha ya
kiongozi huyu ewe Mola thibitisha makao yake peponi nasi mola tupe barka zake
tuwezeshe walao kupata kheri baraka kutokana na kazi yake.
Kushoto Sheikh Faisal Al Kindy, Sharif Sayyid Muhammad bin Sharif Saiid AlBiidh na Sheikh Muhammad Idd |
No comments:
Post a Comment