Saleh Feruzi |
Mwaka wa 2011 nikiwa Tanga nilishiriki
pamoja nä marehemu Saleh Feruzi kwenye kipindi cha ''Meza ya Duara,'' cha DW.
Wakati ule marehemu Saleh Feruzi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar
Washiriki wengine
wakiwa Dr. Harith Ghassany akiwa Washington, Ahmed Rajab London na mimi Tanga
na marehemu Feruzi akiwa Zanzibar.''
Mwenyekiti wa kipindi hiki alikuwa Othman Miraj ambae ndiye alikuwa mtayarishaji.
Mada ilikuwa, ''Kumbukumbu ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Hiki kipindi kiliporushwa na kusikilizwa kilipendwa sana
nä wasikilizaji khasa jinsi mie nä marehemu Feruzi tulivyotofautiana na kupambana kuhusu mustakbali mzima wa siasa na maendeleo katika Zanzibar.
Marehemu Feruzi akisema kuwa mapinduzi yameleta maendeleo Zanzibar nami nikisema kuwa kama Zanzibar ingelibaki huru maendeleo yake yangekuwa makubwa sana, Ikawa kiasi wakati mwingine Othman Miraji inabidi aingilie kati kututuliza.
Zentrum Moderner Orient (ZMO) kutokana na
kipindi hiki kupitia Othman Miraj walinialika Berlin kufanya mhadhara na
kuandika mada.
Hii ZMO ni sawa na London School of Oriental and African Studies
(SOAS).
Nilikaa Berlin kwa mwezi mmoja.
Kutoka Berlin nilisafiri kwenda Humburg, Paris,
Amsterdam, Hague na Geneva.
Naamini marehemu Feruzi alikuwa na mchango mkubwa
kwangu katika kipindi kile kwa "kupambana," kiasi cha kuvutia
wasikilizaji.
Bahati mbaya nasikitika sikujaliwa kukutana na marehemu.
Allah amweke mahali
pema peponi.
Mwandishi akiwa ofisni kwake ZMO, Berlin |
No comments:
Post a Comment