Tuesday, 1 November 2016

USIA WA MAREHEMU ALLY SYKES KWA SAIGON CLUB NA BOI JUMA


Ally Sykes akiwa ofisini kwake Mtaa wa Mkwepu

Ahsante sana Sheikh Mohamed Said Salum. 

Leo umetuamsha na makala nzuri tu. 

Inatukumbusha sisi tuliokua karibu nae Almaruhum Mzee Ally Kleist Sykes.

Mimi nilizoea kumsalimia kwa kimombo. 

Nikiingia ofisini kwake tu "Good Morning Old man,'' na yeye hunijibu, ''Good Morning my Boy.'' 

Neno litakalofuata kuna habari gani mjini. 
Kisha ananiambia lilealilo niitia na hasa kuhusu klabu Saigon,

Mzee Ally aliipenda sana klabu yetu ya Saigon na sisi wanachama wote alitupenda. 

Alikua na kawaida kila siku ya Jumapili akitoka ofisini lazima apite klabu ya Saigon. 

Basi  hapo atazungumza na sisi wanae  mpaka saa sita mchana anarudi nyumbani 

Mzee Ally alikua nguzo ya klabu ya Saigon, hata ilipochafuka hali ya hewa. 

Kwa sisi wanachama kutokubaliana kimsimamo kwa mambo Fulani Fulani, ni yeye ndio alie leta Suluhu  na kutupa wasia. 

Alisema hapa Saigon ndio jicho la watu wa Dar es Salaam. 

Sasa mkifanya haya ya kugombana basi mtachekwa na watu wasio watakia mema. 

Tulimuelewa Mzee wetu Mwenyezi Mungu amuondolee adhabu ya kaburi.

 Amin.

No comments: