Utangulizi
13 Desemba 2016 Dar es Salaam
Hapo chini ni barua ya Tume ya Mufti wa BAKWATA ambayo inajieleza. Tarehe ya barua ni 13 Desemba 2016.
Angalia chini yaliyotokea miaka 48 iliyopita tarehe kama hiyo 13 Desemba 1968 BAKWATA ilipoundwa katika mkutano uliofanyika Iringa.
Mufti Sheikh Hassan bin Amir enzi za East African Muslim Welfare Society (EAMWS) |
Ili kuelewa vipi mali za Waislam ziliangukia katika mikono ya BAKWATA inabidi tufuatilie lau kwa muhtsari yale yaliyotokea Desemba 1968 ilipounda BAKWATA kwa msaada wa serikali.
13 Desemba 1968, Dar es Salaam
Ili kuelewa vipi mali za Waislam ziliangukia katika mikono ya BAKWATA inabidi tufuatilia lau kwa muhtsari yale yaliyofanywa na serikali ikishirkiana na baadhi ya Waislam waliokuwa katika kuunda BAKWATA:
''Baada
ya kuundwa BAKWATA, ili kuondoa wasiwasi na kuwarudishia imani Waislam, Katibu
wa Tume ya Waislam, Mussa Kwikima alitoa taarifa iliyosema:
Hakuna
anaeweza kutishia kuwepo kwa EAMWS isipokuwa wanachama wake, sheria na serikali,
lakini si watu binafsi hata ikiwa mikoa yote kumi na saba ikijitoa
haitamaananisha kuwa jumiya imekufa kwa kuwa kuwepo kwake hakutokani na kuwepo
kwa mikoa hiyo kama wanachama isipokuwa kuwepo kwa wanachama wake, Waislam.
Wakati
ilipotoka taarifa hii BAKWATA ilikuwa bado haijaandikishwa rasmi na Msajili wa
Vyama. Kisheria ilikuwa haiwezekani kwa kundi la Adam Nasibu kuunda jumiya mpya
iliyokuwa na malengo sawa na jumuiya ambayo tayari ishaandikishwa. Kwa muda wa
siku tatu BAKWATA na EAMWS zikawepo kwa wakati mmoja. Ilionekana kama kwamba
EAMWS itashinda vitimbi vya serikali na vya kundi la Adam Nasibu.
Tarehe
19 Desemba, 1968 serikali kama vile imegutushwa na taarifa ya Kwikima, iliipa
BAKWATA Cerificate of Exemption na kuifungia EAMWS. Waziri wa Mambo ya Ndani
Said Ali Maswanya kwa niaba ya serikali alitoa taarifa fupi:
Waziri
wa Mambo ya Ndani kwa kuamriwa na Rais anatangaza kuwa tawi la Tanzania la East
African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la la East African Muslim
Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini ya kifungu 6 (i) cha
Sheria ya Vyama.
Kwa
tangazo hilo la Rais wa Tanzania, JulIus Nyerere, Waislam walinyimwa nafasi ya kukutana
na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu Waislam peke yao. Kwa
ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili na kulitolea uamuzi tatizo hilo.
Viongozi
wa EAMWS waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa amekabidhiwa na
serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi shughuli za EAMWS.
Viongozi walifahamishwa kuwa chini ya sheria ya vyama mali zote za EAMWS
zitauzwa na madeni yatalipwa kutokana na fedha hizo na fedha zitakazobaki
watapewa wanachama. Serikali ilikuwa haiwezi kufanya kama sheria ilivyokuwa
imeelekeza. Ilikuwa jambo zito sana kwa serikali ya Nyerere kuonekana
anasimamia kuuzwa kwa mali za Waislam. Viongozi wa EAMWS walipoitwa kwa Kabidhi
Wasii mara ya pili walifahamishwa kuwa serikali imebadilisha mawazo yake
kutekeleza amri kama sheria inavyosema kwa ajili hiyo basi imefanya mabadiliko
ya sheria ya vyama ambayo yanaiwezesha sasa kutoa mali ya EAMWS na kukabidhi
BAKWATA. Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyochukuliwa na kupewa BAKWATA bila ya
ridhaa ya Waislam wenyewe. Hivi ndivyo shule zote zilizojengwa na EAMWS pamoja
na mradi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kilipoanguka katika mikono ya kundi la Adam
Nasibu. BAKWATA haikuwa na uwezo wa kuendesha mipango yoyote na taratibu shule
na miradi yote ya elimu ikafifia na mwishowe kufa kabisa. Hivi ndivyo
halikadhalika moto wa Waislam uliowashwa kwa kupatikana kwa uhuru waliopigania
hadi ukapatikana ulivyokufa. Moto huu ulikuja ukawaka tena, lakini hiki ni kisa
kingine. Insha Allah Mwenyezi Mungu akipenda tutakuja kukieleza.''
No comments:
Post a Comment