Wednesday, 14 December 2016

KUTOKA JF: SHEIKH PONDA



Mtimbo,
Kuhusu Sheikh Ponda kujihusisha na siasa.
Uhuru wa Tanganyika umepiganiwa kwa kiasi kikubwa na masheikh.

Inawezekana hujui vipi TANU iliundwa na kujengwa hadi uhuru wa
Tanganyika ukapatikana mwaka wa 1961.

Katika Tanganyika African Association (TAA) ambayo ndiyo iliyokuja
kuwa TANU mwaka wa 1954 kulikuwa na kamati inaitwa TAA - Political
Subcommiittee.

Ndani ya hiyo kamati kulikuwa na masheikh wawili.

Sheikh Hassan bin Amir ambae ndiye alikuwa Mufti wa Tanganyika
na Sheikh Said Chaurembo aliyekuwa Liwali katika Mahakama ya
mwanzo Kariakoo, Dar es Salaam.

Wajumbe wengine katika kamati hii walikuwa: Abdul Sykes, Dr.
Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, Stephen Mhando
 na John
Rupia.

Kamati hii iliundwa mwaka wa 1950 na ndiyo iliyokuja kuunda TANU
1954.

TANU ilipoundwa ndani yake kulikuwa na Baraza la Wazee wa TANU na
baraza hili lilikuwa na masheikh wengi sana na maarufu sana ni Sheikh
Muhammad Ramia, Sheikh Issa Nasir, Sheikh Suleiman Takadir,
Sheikh Haidar Mwinyimvua 
kuwataja wachache.

Mwekahazina wa kwanza wa TANU alikuwa Sheikh Idd Faiz Mafungo
na huyu ndiye alikuwa mratibu wa safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere
UNO 1955.

Hawa masheikh wote walikuwa wanasiasa na wapigania uhuru.

Ningeweza kukupa mifano lukuki Tanga ambako kulikuwa na masheikh
wengikatika TANU maarufu akiwa Sheikh Abdallah Rashid Sembe na
Lindi kulikuwa na Sheikh Muhammad Yusuf Badi,

Sheikh Hassan bin Amir alikuwa akiuza kadi za TANU msikitini.
Hakuna aliyesimama kuwaambia masheikh hawa wachague dini au siasa.

Hii Wanamajlis ndiyo historia ya nchi yetu.

Mtimbo,
Umegusia kuhusu mali za Waislam na BAKWATA.
Unaweza kusoma hayo hapa chini:
Mohamed Said: HISTORIA YA EAMWS NA JINSI KABIDHI WASII ALIVYOKABIDHI MALI ZA WAISLAM KWA BAKWATA 1968


[​IMG]

[​IMG]

No comments: