Utangulizi
Hili lililotokea Zanzibar la kutukanwa Mtume SAW halijapata kutokea Zanzibar na kwa hakika limeshtua watu wengi. Matusi haya yalienea kwa haraka katika mitandao ya kijamii na haikuchukua muda dunia nzima ya wasemaji wa Kiswahili wakawa wamefikiwa na taarifa hizi za kusikitisha. Kwa kipindi fulani pakawa na mgoNgano wa fikra kuhusu hiyo clip ya matusi kama inajuzu kuwa inazungushwa na watu kuyasikia matusi hayo. Lakini baya zaidi ni kuwa clip hiyo ya matusi ilikuwa imeambatana na picha ya mtukanaji akiwa na kiongozi mkubwa katika CCM na serikali. Waislam walitegemea kuwa huyu mtukanaji atakamatwa haraka lakini hili halijatendeka. Siku ya pili yake ikawekwa clip nyingine mtukanajI akiomba radhi kwa matusi aliyotukana jana yake. Mengi yamesemwa lakini mimi nimeona niweke tamko hili lililosambwazwa na Elimu ni Nuru Group ili wasomaji wangu wajue kilichotokea Zanzibar.
➡ Amezuka mtu Amekufuru kwa kumtukana Mtume Muhammad Rehma na Amani Ziwe Juu Yake (SAW) anaijulikana kwa jina la Abdalla inasemekana amesomea Udaktari Urusi, ni Daktari wa Hospitali ya Mnazi Mmoja na hospitali nyengine binafsi hapa Zanzibar.
➡ Ametoa Video na kurushwa katika mitandao mbalimbali baina ya jana na leo tarehe 25/26 December 2016.
➡ Video hiyo amewatukana watu wengi akiwemo Mtume wetu na kipenzi chetu Mtukufu wa Darja na Habib wa MwenyeziMungu. Matusi ambayo hatuwezi hata kuyasimulia hapa kwani kusimulia tu ni katika Utovu wa Adabu
➡ Kwa ufupi amemnasibishia Mtume Muhammad (SAW) na mambo machafu waziwazi
➡ Amerekodiwa kwa picha na sauti na akiwa mzima wa akili na hata hakulewa kinyume na alivyokuja kudai baadae. Akiyasema hayo akiwa anajuwa analolifanya.
➡ Uchunguzi mdogo uliofanywa umegundua kuwa mtu huyo ni kawaida yake kukufuru hata mbele za watu na wapo watu wanaomfahamu wamethibitisha hilo, hayo ameyafanya alipokuwa Uiengereza akayarudi Unguja na Pemba kabla ya hio Clip ya Tarehe 25 na 26 December 2016
➡ Kutokana na hayo:
Tunalaani kitendo chake hicho cha Kumtukana Mtume wetu Muhammad Rehma na Amani Ziwe Juu Yake, bali tunamlaani na yeye aliyetamka maneno hayo.
➡ Amesema MweyeziMungu katika suratul Ahzab aya ya 57 : "Kwa yakini wale wanaomuudhi MwenyeziMungu na Mtume wake, MwenyeziMungu amewalaani katika dunia na Akhera na amewaandalia adhabu ifedheheshayo"
➡ Enyi wapenzi wa Mtume Muhammad (SAW) pazeni sauti zetu usikie Ulimwengu mzima kumlaani Mtu huyo asiekuwa na adabu aliyekwisha LAANIWA na Mola wetu.
➡ Hata kama amedai ameomba samahani ajuwe hilo ni baina yake na Mola wake. Tujualo sisi ni kuwajaribu Waislamu na kuwachokoza na kwa kujuwa hatofanywa kitu.
➡ Tunatowa wito kwa kila Muislamu mwenye wivu na ghera ya Mtume wake na dini yake, amlaani mtu huyo na kukatwa kijamii hadi ithibitike kweli kweli tawba yake.
➡ Wito kwa wanaohusika na Hospitali ya MnaziMmoja na zile anazofanya kazi, mtimueni mtu huyo kwani kumbakisha kuwa daktari katika hospitali zenu kunaonesha kuridhishwa kwenu kwa hayo aliyoyafanya.
➡ Wito kwa vyombo vya Kiislamu vya Serikali yetu na khassa OFISI YA MUFTI ZANZIBAR.*
Apewe adhabu mtu huyo inayostahiki na kuwa funzo kwa watakaokuja baadae. Na lipewe jambo hili Umuhimu wake kama alivyodai Bi Salama Utume na Ofisi yetu Tukufu ya Mufti ikamchukulia hatua haraka sana.
➡ Wito kwa Polisi Zanzibar mdhibitini mtu huyo haraka sana kwani anahatarisha Usalama wa wananchi kwa kumtukana Mtume wetu jambo ambalo hatuwezi Waislamu kulivumilia hata chembe.
➡ Wito kwa Waislamu wote kuwa makini na watu wa aina kama hii. Huyu kartaddi bila ya khilafu. Na amemdhalilisha Mtume wetu Muhammad (SAW).
➡ Kulaani huku hakuhusishi wale watu wengine aliowatukana. Sisi anaetuhusu ni Mtume wetu Muhammad Rehma na Amani Ziwe Juu Yake.
LAANA YA MOLA IMSHUKIE MTU HUYU AITWAYE ABDALLA ANAEFANYA KAZI HOSPITALI YA MNAZI MMOJA.
IMETOLEWA NA WAPENZI WA MTUME MUHAMMAD (SAW) na WAISLAMU WENYE GHERA NA UISLAMU WAO
Utume Ujumbe huu kama unayo ghera kwa Mtume wako kipenzi cha Mola wako.
No comments:
Post a Comment