Kamati Tendaji ya JUMAZA ilikaa katika kikao chake cha dharura
tarehe 27 Disemba, 2016 kujadili na kutafakari video iliyosambazwa katika
mitandao yote ya kijamii ikmuonesha Dk. Abdalla Saleh akimkufuru Allaah (S.W)
pamoja na kumtukana matusi makubwa sana mpaka ya nguoni na kumdhalilisha Mtume
wetu Mtukufu kipenzi cha umma Muhammad Salla Allaahu Alayhi wa Sallam. Baada ya
kujadili kwa undani JUMAZA inatamka ifuatavyo:-
1.
Kwa taarifa
ambazo JUMAZA imezipata Dk. Abdalla Saleh Abdalla anatoka katika familia ya
Kiislamu huko Wete Pemba lakini aliamua kurtadi muda mrefu sasa wakati akiwa
nje ya Zanzibar.
2.
Kwa kumbukumbu
zilizopo hii si mara ya kwanza kwa kijana Abdalla kutoa matusi, kashfa na kufru
kwa Allaah, Mtume Salla Allaahu Alayhi wa Sallam na Uislamu kwa jumla.
Madaktari na wafanyakazi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja ambapo kijana huyo
anafanya kazi walishamuonya mara kadhaa kuhusu tabia yake hiyo. Hata hivyo, huwa
hasikii hupuuza na kufanya kibri. Hivyo ni wazi kuwa vitendo anavyofanya anafanya
makusudi kwa malengo anayoyajua yeye mwenyewe.
3.
JUMAZA,
Waislamu wa Zanzibar pamoja na Waislamu wa Dunia kwa ujumla hawako tayari
kuvumilia hata kidogo kitendo cha kumtukana na kumdhalilisha Mtume wao Salla
Allaahu Alayhi wa Sallam kama alivyofanya kijana Abdalla. Aidha, aelewe kijana
huyu Waislamu wako tayari wakati wowote kujitoa muhanga kama ilivyotokea katika
historia ya Maswahaba Watukufu ili kulinda hadhi na heshima ya Mtume wao Salla
Allaahu Alayhi wa Sallam.
4.
JUMAZA
inaungana na Mufti wa Zanzibar na Waislamu wote kulaani kwa nguvu zake zote
kitendo hiki cha uchochezi na kuiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kumkamata haraka, kumdhibiti na kumchukulia hatua za kisheria. JUMAZA inatoa
ushauri huu kwa nia njema ili kulinda amani ya nchi na utulivu na hasa kwa
kuzingatia kuwa raia wake wengi ni Waislamu wanaoumwa sana na Dini yao.
5. JUMAZA
inaungana na Mufti wa Zanzibar kuvitaka vyombo vinavyohusika kumchukulia hatua
mara moja kijana Abdalla, kumfungulia mashtaka na kumpandisha mahakamani ili
sheria ifuate mkondo wake. Hii ni kwasababu sisi tunaamini kuwa kitendo
alichokifanya kijana Abdalla kinakiuka moja kwa moja Sheria za Zanzibar.
6.
JUMAZA na
Waislamu wote wana imani kuwa hukumu ya kiuadalifu itatolewa kwa kijana huyu
ili Waislamu waendelee kuwa na imani na viongozi wao na Serikali yao kwa
ujumla. Aidha, JUMAZA inaonya kuwa hatua yoyote ya kudharau kuchukua hatua kali
dhidi ya kijana Abdalla inaweza kupelekea matokeo ambayo si mazuri katika nchi yetu. Hivyo, kuwajibika ipasavyo
kwa vyombo vinavyohusika ndio njia pekee ya kuepusha uwezekano wa Waislamu
kuchukua hatua mikononi mwao.
7.
JUMAZA inakumbusha tena kuwa kosa alilolifanya
kijana Abdalla tena kwa makusudi na kibri ni kosa zito sana na hukumu yake
katika Sheria za Kiislamu kama alivyosema Mufti ni kukatwa kichwa. Hatahivyo,
kwa kuwa Zanzibar haifuati Sheria za Kiislamu basi itumie sheria zake za
kiserikali dhidi ya kijana huyu ili kulinda heshima yake kama nchi inayojali
utawala bora pamoja na kulinda heshima kwa Dini zote.
8.
JUMAZA inawaomba
Waislamu wote kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na kuvipa nafasi vyombo
vinavyohusika kuchukua hatua zake dhidi ya kijana Abdalla. Hata hivyo,
inawaomba Waislamu kulifuatilia suala hili kwa karibu zaidi ili kujua hatma
yake.
9.
Mola wetu Mtukufu
tunakuomba uinusuru Dini yako na Waislamu kwa jumla dhidi ya maadui wa ndani na
nje. Amiin.
Ahsanteni
Muhiddin Zubeir Muhiddin
KATIBU MTENDAJI
JUMAZA
ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment