Mwangaza Oktoba 5, 1956
Utangulizi
Rafiki yangu Abubakar Shani kaweka katika group letu ''Kumbukumbu,'' kipande cha gazeti la Mwangaza la Oktoba 5, 1956 ikimuonyesha Liwali wa Dar es Salaam wa wakati ule Ahmed Saleh akiwa na Sheikh Said Chaurembo ambae alikuwa hakimu katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo akihukumu kwa mujibu wa sheria za Kiislam. Wote hawa wawili walikuwa watu maarufu na mimi katika utafiti wa kitabu changu, ''The Life and Times of Abdulwahis Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' wote nimekutananao katika nyaraza za Sykes na katika simulizi mbili. Simulizi ya kwanza kutoka kwa Tewa Said Tewa na ya pili kutoka kwa Ali Mwinyi Tambwe ambae yeye mwenyewe nimemkuta katika nyaraka hizo za Sykes. Naweka hapa chini yale niliyoandika kuhusu Liwali Ahmed Saleh na nitahitimisha In Shaa Allah kwa habari za Sheikh Said Chaurembo:
''...Si
mambo yote yalikwenda shwari katika kuiendesha shule ile. Mwaka 1940 Ahmed
Saleh alichaguliwa kuwa liwali wa
Al
Jamiatul Islamiyya kwa wakati ule ilikuwa ikishughulika na kuendesha shule na
kusoma maulidi ya kila mfungo sita. Ofisi ya liwali ilikuwa ikishughulika na
mambo yote yaliyokuwa yanahusu sharia na mambo mengine ya Kiislam. Kwa miaka
mingi maulidi yalikuwa na kamati yake maalum mbali kabisa na shughuli za ofisi
ya liwali. Liwali Saleh hakupendezewa na mpango huu, yeye aliona kuwa kamati ya
maulidi iwe chini yake. Liwali Saleh akaanza kutoa makosa jinsi maulidi
yalivyokuwa yakisomwa na kusheherekewa. Alipinga mchanganyiko wa wanafunzi wa
kike na wa kiume kuchanganyika na kupanda kwenye member na kusoma kasida. Jambo
la kusikitisha katika mgogoro huu ni kuwa chanzo hasa cha kuwaleta wale
wasichana kusoma mbele ya wazee wao ilikuwa ni kutafuta pongezi kutoka kwa
wazazi. Al Jamiatul Islamiyya ilikuwa imenzisha shule ya wasichana wa Kiislam.
Uongozi wa shule katika kutaka kuonyesha kazi nzuri iliyokuwa ikifanywa na
shule iliona ifanye onyesho
Kwa
kuzingatia sharia hasa, hiyo inaweza kuchukuliwa kuwa Liwali Saleh alikuwa sawa
kutokana na mafundisho ya Kiislam, lakini ukitazama kwa mtazamo mwingine,
unaweza ukasema kuwa wale walikuwa watoto wadogo wasiokuwa balehe na kwa hivyo
basi kulikuwa hakuna ubaya wowote kwa wao kujitokeza mbele ya halaiki ya watu.
Lakini ingawa kwa sura ya nje alionekana Liwali Saleh
Al
Jamiatul Islamiyya ikagawanyika katika kambi mbili hasimu. Kambi moja ikawa ni
ile ya wale waliojulikana
Wanachama
wa Al Jamiatul Islamiyya wakaitisha mkutano nyumbani kwa Mwarabu mmoja tajiri
aliyekuwa na biashara ya kuuza duka, jina
Mkutano
ule ulipendekeza jina la Ali Mwinyi Tambwe kushika nafasi ya Kleist. Sheikh Ali
Saleh Imam wa Msikiti wa Kitumbini aliunga mkono uteuzi ule na Ali Mwinyi
akashika wadhifa wa katibu wa Al Jamiatul Islamiyya na akapewa maelekezo ya kuandika barua kwa
PC. Ali Mwinyi alikuwa mfanyakazi wa serikali akifanya kazi katika ofisi ya
Kabidhi Wasii. Ali Mwinyi hakumuandikia PC moja kwa moja, la hasha. Alikwenda
kwa mwanasheria mmoja wa Kiasia, Rajabali Bhalo Verani akamuhadithia mkasa
mzima uliopelekea kufungiwa kwa shule ya Waislam. Al Jamitul ilikuwa haina
fedha za kumlipa lakini Verani akasema yeye ataichukua kesi ile bila ya malipo
yoyote kwa kuwa ilikuwa kesi ya kudai haki kwa hiyo hakukuwa sababu ya kuwatoza
watu wanaodhulumiwa. Verani akamuandikia PC na kumuamuru afungue shule ya
Waislam katika saa arobaini na nane ama sivyo hatua za kisheria zitachukuliwa
dhidi yake.
Mara
moja PC akauita uongozi mzima wa Al Jamitul Islamiyya ofisini kwake ili
kujadili tatizo la kufungwa shule. Ali Mwinyi akenda kumueleza Verani kuhusu
mwito wa PC. Verani akamuambia Ali Mwinyi kuwa amfahamishe PC kwamba,
makubaliano yoyote yatakayofikiwa katika mazungumzo kati yake na uongozi wa Al
Jamiatul Islamiyya shurti yaidhinishwe na yeye kama mwanasheria wa Al Jamiatul
Islamiyya; na vilevile ajaribu kutafuta sulhu kati ya Wanubi na Wamanyema
waliokuwa wamefarikiana na Wazaramo na Warufiji. Wanubi na Wamanyema, wote
wakiwa kizazi cha pili cha wazee waliotoka Belgian
PC
aliwaeleza wanachama wa Al Jamiatul Islamiyya kuwa amewaita ili wazungumze
kuhusu kufungwa kwa shule na kupatanisha baadhi mbili zilizokuwa zimehasimiana
kwa muda. PC alitaka kujua ni wanachama wapi wanalipa ada zao. Sasa ikawa baada
ya mgogoro ule Wazaramo na Warufiji na watalamizi wao wakaacha kulipa ada zao
za uanachama. PC akawafahamisha kuwa
kwa kutolipa michango
Baada
ya Liwali Saleh kufanikiwa kuchukua uongozi wa Waislam ëwenyejií alihakikisha
kuwa shughuli zote za Kiislam zinatendeka chini ya uongozi na maelekezo ya
serikali ya kikoloni. Kwa ajili hii aliunda kamati yake ya Maulidi na Sala ya
Idd yeye mwenyewe akiwa mwenyekiti wa kamati hizo. Liwali Ahmed Saleh alitumia
kamati hizo kwa kujikomba kwa Waingereza. Katika kila hafla ya Kiislam ama iwe
kwenye Baraza la Idd au Maulid, yeye alikuwa akiwaalika viongozi wa serikali
Wazungu, kuja kutoa matamshi ya kukatisha tamaa harakati za Waislam za kupinga
ukoloni kwa kuwaambia Waislam waache fujo na serikali ya kikoloni itawaletea
maendeleo. Hali ilikuwa hivi hadi miaka ya 1950 mwishoni alipojiuzulu kutoka
uliwali wa
Kamati Ndogo ya Siasa Ndani ya TAA, 1951
Hakuna
nyaraka zozote zinazoonyesha kama African Association ilikuwa imetayarisha
mpango wa kushughulikia hali ya siasa.
Kuelewa mwelekeo wa siasa kama wakati ule inabidi mtu atazame mwenendo
wa viongozi wa TAA na jinsi walivyokuwa wakiyashughulikia mambo tofauti
yaliyokuwa yakiwadhili wananchi. Jambo la kwanza alilofanya Abdulwahid mara tu
baada ya kuingia madarakani ni kuunda TAA Political Subcommittee (Kamati Ndogo
ya Siasa ya TAA) iliyomjumuisha yeye
mwenyewe Abdulwahid, Sheikh Hassan bin Amir kama mufti wa Tanganyika; Dr.
Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, Said Chaurembo aliyekuwa liwali wa mahakama ya
Kariakoo; John Rupia na Stephen Mhando. Kazi ya kamati hii ilikuwa ni kushughulika
na masuala yote ya siasa katika Tanganyika. Kuundwa kwake ndiyo hasa ulikuwa
mwanzo wa siasa za dhahiri katika Tanganyika na mwanzo wa harakati za kudai
uhuru wa Mtanganyika.
|
Wednesday, 28 December 2016
LIWALI AHMED SALEH NA SHEIKH SAID CHAUREMBO
About Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment