Thursday, 29 December 2016

MAALIM BAHIA WATOTO ALIOWAFUNDISHA QUR'AN HAWAHESABIKI

Photo: MAALIM BAHIA AND DAUGHTER

Maalim Bahia Mke wa Sheikh Mzee Ali Comorian na Mama yake Sheikh Ali Mzee Comorian

Ifuatayo ni makala kutoka kwa msomaji:
[29/12, 6:18 p.m.] ‪+255 719 214 421: Allah amuhifadh mzee wetu huyu na amjaalie mwisho uliomwema mie tokea nakua na muona huyu mama mwalimu wa madrasa anafunɗisha na miongoni mwa wanazuoni nimtoto wake marehemu Shk Ally Mzee Comoriani na marehememu mume wake Shk Mzee Ally Comorian alikua mwanazuoni ktk jiji la Dar na alikua miongoni mwawazee walijitolea kufunɗisha dini na kushiriki harakati za siasa za uhuru wa nchi hii na madrasa ipo nyumɓani kwake Karikoo na Likoma na Jangwani

[29/12, 631 p.m.] ‪+255 719 214 421: Madrasatu Abbasia ni miongoni mwa madrasa iliotoa mchango mkuɓwa wa kufundisha dini jijini ɗar kwa wanazuoni wakuɓwa tu ilikua ya marehemu Shk Ramadhani Abbas Allah ampe malazi mema huko alipo mɓele ya haqq madrasa anaienɗeleza mtoto wake Abass Ramadhan Abbass huwa anasalisha Masjid Mtoro ɓahadhi ya siku na mwezi wa Ramaɗhani yeye nɗie anaongoza duua ɓaada ya sala kwa nyiradi za utaratiɓu waliojiwekea hapo msikitini na marehemu Mzee Ramaɗhani Abass mama yangu amenihadithia siku ya mazishi yake ulikua umma mkuɓwa sanaa alikaɗhalika Shk Mzee Comorian pia ilikua hivyo na madrasa abasia ipo Mtaa Mkunguni na Mzizima na Bonɗe.


No comments: