Utangulizi
Picha hizi zinatoka
katika Maktaba ya Said Tewa mtoto wa marehemu Tewa Said Tewa ambae kwa miaka
mingi amekuwa akiishi Denmark. Said anasema ameniletea picha hizi baada ya
kuona juhudi zangu katika kuhifadhi historia ya Tanzania na viongozi wake baba yake akiwa mmoja wao iliyokuwa
karibu ipotee. Hayo maandishi, ‘’caption,’’ katika baadhi ya picha ni mwandiko
wake mwenyewe Mzee Tewa. Picha nilizopokea ni nyingi sana zikimwonyesha Tewa Said Tewa katika mengi lakini nimeona nichukue hizi chache ambacho zitamuunganisha yeye na matokeo muhimu zaidi katika historia ya Tanzania na katika nafasi yake kama kiongozi wa Waislam akiwa Rais wa East African Muslim Welfare Society upande wa Tanzania. Binafsi nimejifunza mengi kutoka kwa Mzee Tewa tukiwa tumekaa sisi wawili tu nyumbani kwake Magomeni Mikumi akinihadithia historia ya uhuru wa Tanganyika.
Msikilize Mzee Tewa:
Msikilize Mzee Tewa:
Tewa
Said anakumbuka siku kabla ya uchaguzi pale Ukumbi wa Arnatouglo, Abdulwahid Sykes alikwenda nyumbani kwake jioni. Wakati huo Tewa alikuwa akikaa mtaa huo huo wa
Aggrey na Swahili, si mbali sana kutoka nyumbani kwa Abdulwahid. Abdulwahid
alimwambia Tewa maneno haya kuhusu mabadiliko ya uongozi ambayo waliamua
kuyafanya katika TAA:
‘’Tewa,
kesho tunakwenda kumpa huyu mtu, Nyerere, mamlaka ya kuendesha nchi hii.
Kuanzia hapo, mara tu tutakapomchagua kutuongoza hakuna namna tena ya
kumnyangĂanya madaraka tuliyompa. Hatumfahamu vizuri sana lakini natumaini kila
kitu kitakwenda sawa.’’
Mengi kuhusu Tewa Said Tewa unaweza kuyasoma hapo chini:
http://www.mohammedsaid.com/2013/12/tewa-said-tewa-mmoja-wa-waasisi-wa-tanu.html
http://www.mohammedsaid.com/2013/12/tewa-said-tewa-mmoja-wa-waasisi-wa-tanu.html
Said Tewa Said |
Tewa Said Tewa alipokuwa mwanasiasa kijana katika harakati za Wednesday Tea Club Dar es Salaam ya 1950s |
Tewa Said Tewa na Chief Abdallah Said Fundikira na baadhi ya viongozi wa EAMWS |
Kushoto wa pili Tewa Said Tewa na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Nyerere uliokuwa katika ziara ya China 1965 |
Kushoto Abdulrahman Babu, (pass), Oscar Kambona, Tewa Said na Nyerere Nyuma walosimama mwenye miwani ni Aboud Jumbe China 1965 |
Balozi Tewa Said Tewa na Mwenyekti wa Chama Cha Kikomunisti Cha China, Peking 1965 |
Tewa Said Tewa katika Hijja mwaka wa 1991 |
No comments:
Post a Comment