Utangulizi
Kila unapoitafiti
historia ya Zanzibar ndipo inapozidi kukushangaza na kukustaajabisha khasa
katika muingiliano wa Zanzibar na Oman na udugu uliojengeka kwa miaka isiyo na
hesabu. Rais mmoja wa Tanzania akiwa Unguja kwenye mkutano wa hadhara kama
ilivyo ada ili kunogesha hotuba yake na kuwafurahisha wanamapinduzi alitoa
maneno ya kuwakashisifu, ''Waarabu wa Omani.'' Akisema huku shingo ametoa kuwa
waliopinduliwa wamsikie anachosema.
Ghafla nyuma yake walipokaa waheshimiwa wote wa serikali Chama Cha
Mapinduzi na Memba wa Baraza la Mapinduzi wengi wakawa wamejiinamia wameshika
vichwa kwa fadhaa. Wamefadhaika kwa kuwa maneno yale yalikuwa moja kwa moja
yawamagusa wazazi wote, babu, baba mama waliotangulia mbele ya haki na kwa
kwengine wakwe zao ambao kwa hakika wana asili ya Oman wala hili halina shaka kwani
ukiwatazama tu wanaonyesha kuwa wamechanganya damu. Hotuba ile haikuwa muafaka
kwa wakati huu kwani mengi yalikuwa yamepita. Watoto wa mahasimu walikuwa
kwengine mke na mume na walikuwa jukwaani katika orodha ya waheshimiwa sana
wakimsikiliza Rais akihutubia akiwakejeli wazee wao waliowazaa na kuwaleta
duniani lakini kwa rehma za Allah ingawa wazee wao walikuwa ‘’maadui,’’ wao wakaja
kuwa wapenzi kiasi cha kuoana na kujenga familia. Leo wako katika serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kama viongozi wakuu na wake zao wake wa viongozi. Hawa
hawakuwa tena ‘’maadui wa mapinduzi.’’ Hawa sasa ni ni wakwe, mababu na mabibi
wa watoto zao majumbani na wazazi hawa wanafanya juhudi kubwa sana kuwakinga
watoto wao na historia ya kuhuzunisha kuwa babu zao kiumeni na kikeni walikuwa
maadui wa kufikia ukomo wa kutoana roho. Iweje leo Rais wa Tanzania awe jukwaani anakwangua
makovu yaliyokuwa yamepona na kuanza kusahaulika kwa koo zilizokuwa hasimu
watoto wao kuoana na Allah kujaalia wajukuu watakaounda Zanzibar mpya ijayo?
Kwenye chakula cha jioni Ikulu mmoja wa waheshimiwa akamnong'oneza
Rais kwa kumwambia kuwa katika hotuba yake mchana kamuumiza sana mwenzake na kumtia
fadhaa ''First Lady,'' kwani vijembe vile vimewahusu baadhi ya wazazi wa
viongozi wa juu katika serikali ya mapinduzi. Rais akadai maelezo. Alipoelezwa zile
nasaba aliinamisha kichwa aliponyanyua
kichwa chake juu alisema kwa Kiingereza, ''I will never come to understand you
Zanzibaris.''
Mheshiwa akamwambia Rais, ‘’Shida yenu nyie watu wa Bara hamtaki
kabisa kutujua wala kuijua historia yetu. Sisi sote hapa utuonavyo ni ndugu.’’
Angalia nasaba ya Waziri wa Elimu wa Oman Dr. Rawya Saud Al Busaid hapo chini kama iliyoelezwa na Ummie Mahfoudha Alley Hamid ambae yeye mwenyewe ni kitukuu cha Tip Tip:
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(kulia) akizungumza na Waziri wa Elimu
ya Juu wa Nchini Oman, Dk.Rawya Saud Al Busaid, Ikulu Mjini Zanzibar
Dr. Rawya Albusaidy ni kitukuu cha Tip Tip.
Mama yake Marhuma Bi Samira ni mjukuu wa Tip Tip. aliyezaliwa na Marhum Nassor Lamky mtoto wa Marhuma Fatma bint Hamed Bin Mohammed bin Juma Almarjeby
(TipTip).
No comments:
Post a Comment