Tuanze na hili la mwisho unapowapa indhar Azam TV waache kunikaribisha kwa
mahojiano.
Mimi si mgeni kwa Azam TV.
Nimefanyanao vipindi vingi sana na na naamini wananikaribisha kwa kuwa kuna faida
inapatikana kwa watazamaji wao.
Mimi nimezungumza kutoshinda uchaguzi CCM Zanzibar naamini na wewe umekusidia
hivyo hivyo pia ingawa katika bandiko lako unetaja CCM nadhani ukimaanisha CCM
Tanzania nzima.
.
Mwaka wa 1995 CCM Zanzibar ilishindwa na ikakataa kushindwa kupitia barua ya Ali
Ameir.
Ningeweza kuendelea lakini tuishie hapa kwanza ili urudi kufanya utafiti kuhusu hii
barua ya Ali Ameir.
Mimi sitoki hapa nakusubiri urejee na maelezo ya barua hiyo.
Ndiyo siku zote huwa nashauri kuwa kabla hajakuja jamvini kuchangia angalau basi
mtu afanye utafiti mdogo ili apate kujua ukweli katik hicho anachochangia.
Hayo yote uchaguzi na mapinduzi yanauhusiano mkubwa sana labda ikiwe huijui
historia ya Zanzibar.
Baadhi ya vipindi nilivyofanya na Azam TV:
Mohamed Said: AZAM TV KIPINDI MAALUM CHA MASHUJAA WA UHURU WA TANGANYIKA
Mohamed Said: WASIFU WA ABEID AMANI KARUME AZAM TV 2015
Mohamed Said: KIPINDI AZAM TV KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI ZANZIBAR 2016
Mohamed Said: AZAM TV: MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUTOKA KUMBUKUMBU ZILIZOZIKWA
Mohamed Said: Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere -Azam TV
Mohamed Said: KUMBU KUMBU YA MIAKA 54 YA UHURU - AZAM TV 02
Mohamed Said: AZAM TV KIPINDI MAALUM CHA SABASABA KUASISIWA KWA TANU 1954
Mohamed Said: AZAM TV KARUME DAY: ABEID AMANI KARUME - "THE MASTERMIND" MAHOJIANO NA IRENE KILENGA
No comments:
Post a Comment