Bandiko hili limeshawahi kuletwa hapa na nilieleza kuwa kuna makosa mengi.
Inaelekea mwandishi hakubali kuwa kuna makosa.
Kazi ya kisomi inahitaji rejea ili kuthibitisha kinachoelezwa.
Walimu wetu siku zile Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wakituasa kutoandika
''barua,'' yaani kuandika mada ya kisomi bila rejea.
Hicho hapo juu ni ''barua,'' siyo mada ya kisomi.
African Association haikuasisiwa 1927 bali 1929.
Anaweza kufanya rejea katika, ''Modern Tanzanians,'' John Iliffe (Ed) makala
ya Daisy Sykes Buruku, ''Kleist Sykes The Townsman,'' akipenda hata amsome
Mohamed Said, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968)...''Kleist
Sykes: Pioneer and Man of Ideas 1894 - 1949.''
Akipenda zaidi anaweza kuingia katika Dictionary of Africa Biography, Oxford
University Press 2011, aangalie Kleist Sykes.
Anasema African Association iliassisiwa Stanley Street si kweli kwani wakati huo
1920s hiyo nyumba ya harakati za siasa ya Kleist hapo mtaani ilikuwa bado kabisa
haijajengwa.
Nyumba hiyo ilijengwa 1942.
AA iliasisiwa Mission Quarter nyumbani kwa Cecil Matola Mtaa wa Masasi, nyumba
hii baadae ilinunuliwa na John Rupia.
Kuna mengi ya kutunga mfano wa Nyerere kukusanya ''vijana wenzake wa Kariakoo,''
nk. nk. hakuna ukweli wowote Nyerere hakupatapo kuishi Kariakoo ila kwa muda
mfupi sana 1955 alipokaa nyumbani kwa Abdul Sykes Stanley Street baada ya kuacha
kazi ya ualimu.
Atakae kujua TANU iliasisiwa vipi sharti kwanza aijue Kamati ya Siasa katika TAA.
Waliokuwa katika kamati ya ndani ya kuasisi TANU ni wajumbe wa TAA Political Subcommittee
wajumbe walikuwa Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Said Chaurembo, Abdulwahid
Sykes, Dr. Vedasto Kyaruzi, Steven Mhando, Hamza Mwapachu na John Rupia.
Safari ya Mwalimu Nyerere ya kwanza 1955 ilighariimiwa na TANU yenyewe na mratibu
wa safari ile aliyekuwa akikusanya fedha alikuwa Idd Faiz Mafongo aliyekuwa mweka
hazina wa TANU na Al Jamiatuli Islamiyya fi Tanganyika.
Hebu kwanza tusimame hapa.
Lakini kwa kulisaidia jamvi lau kwa ukumbusho kwa kuwa mada hii ilishajadiliwa miaka mingi
iliyopita nawaomba waingie hapo chini wasome niliyopata kuandika kuhusu historia ya
Tanganyika:
Mohamed Said: LIWALI AHMED SALEH NA SHEIKH SAID CHAUREMBO
Mohamed Said: KUTOKA JF: MAMA DAISY NA HISTORIA YA CHIEF DAVID KIDAHA MAKWAIA
Mohamed Said: KUMBUKUMBU ZA IDDI TOSIRI MWANACHAMA WA TANU KADI NO. 24
Mohamed Said: LAMECK BUGOHE MUASISI WA TANU 1954 KAFARIKI NA KUZIKWA KIMYA KIMYA
Mohamed Said: ZUBERI MWINSHEHE MANGA MTEMVU MZALENDO ALIYEKUWA NA MSIMAMO MKALI WA “AFRIKA KWA WAAFRIKA”
Mohamed Said: Abbas Kleist Sykes 1929 -
Mohamed Said: Idd Faiz Mafongo Mweka Hazina wa Safari ya Nyerere UNO 1955
Mohamed Said: MCHANGO WA MUFTI SHEIKH HASSAN BIN AMEIR KATIKA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA MAHOJIANO KATI YA SHEIKH RASHID SALIM NA MOHAMED SAID RADIO NUR ZANZIBAR
Mohamed Said: KUTOKA FB: VITUKO VYA YERICKO ''NYERERE''
Mohamed Said: KUTOKA JF: HISTORIA YA TANU - DK. VEDASTO KYARUZI, KASELLA BANTU NA JULIUS NYERERE
Mohamed Said: Ijue Historia ya Kweli ya Kuasisiwa kwa TANU
Mohamed Said: KUMBUKUMBU YA MASHUJAA WA UHURU WA TANGANYIKA RASHID ALI MELI
Mohamed Said: AZAM TV KIPINDI MAALUM CHA MASHUJAA WA UHURU WA TANGANYIKA
Mohamed Said: KUTOKA JF: SHEIKH HASSAN BIN AMIR ALIVYOIONGOZA TANU KUWA CHAMA CHA KISEKULA
Mohamed Said: KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK
Wanamajlis,
Hizo hapo juu ni zaidi ya kurasa 100 za kusoma pamoja na audio za kusikiliza
na video za kuangalia.
Si lazima upitie zote chagua moja mbili tatu utakuwa ushajifunza kitu.
Waswahili tuna msemo na Mzee Ali Hassan Mwinyi akipenda kuutumia,
''Muongo muongoze.''
Chembelecho Maalim Faiza: Elimu bila Khiyana.
- MUSLIM NATIONALISTS IN TANGANYIKA: The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924–1968): The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika. By MOHAMED SAID. London: Minerva Press, 1998. Pp. 358. £11.99, paperback (ISBN 0-75410-223-8). -
- JONATHON GLASSMAN
- Published online: 01 March 2001, pp. 117-172
Evanston, Chicago alinialika nikazungumze chuoni kwake juu ya historia ya
TANU na uhuru wa Tanganyika.
Nilizungumza katika Ukumbi wa Eduardo Mondlane.
Glassman alifanya pitioa la kitabu changu katika Cambridge Journal of African
History Vol. 42 Issue 1 March 2001 halikadhalika John Iliffe.
No comments:
Post a Comment