Monday, 13 February 2017

KUTOKA JF: CHIRAU ALI MWAKWERE ALIPOMUADHIMISHA HAMZA MWAPACHU KWALE



[​IMG]
Chirau Ali Mwakwere na Rais Jakaya Kikwete nyuma ni Balozi Mohamed Maharage Juma​ Mdigo wa Gombero

[9:45 PM, 2/13/2017] +255 687 500 699: Huyu Ali Mwakwere ni Mdigo wa Kwale.

Siku alipokutana na Juma Mwapachu wakati ule Juma Mwapachu Secretary General EAC wakajuana kuwa wote ni Wadigo.

Juma akamuhadithia Mwakwere historia ya baba yake Hamza Kibwana Mwapachu alisoma Makerere pamoja nä Julius Nyerere.

Hamza akiwa Mdigo wa kwanza kuingia Makerere.

Mwakwere aliporejea Kwale akaiomba Council ya Kwale umpe mtaa Hamza Mwapachu kwa kuheshimu kuingia Makerere kwa Mdigo wa kwanza.

Ukienda Kwale utakuta huu mtaa - Hamza Mwapachu Street.

[9:45 PM, 2/13/2017] +255 687 500 699: Mimi nilikutana na Ali Mwakwere kwenye Maulid ya Lamu.☝

[9:45 PM, 2/13/2017] +255 687 500 699: Hapa nyumbani Hamza Mwapachu hajapewa mtaa hata kwao Tanga.

Nilimuuliza Guled Meya wa Tanga hivi nyie hamuoni vibaya kuweka jina "Maua" katikati ya mji ilhali mna mashujaa waliopigania uhuru kutoka Tanga?

Nikampa majina - Hamisi Heri, Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Mohamed Kajembe ...

No comments: