Muulize, kama kawaida yake atakupa michapo.
Huwa nnazowa mengi sana kwake.
I think I should start to record him.
Mohamed SaidVerified User ✅
HNIC,
Nimesafiri na Tamim kwingi.
Nimekuwa na Tamim Kenyatta University, University of Johannesburg, University
of Ibadan na kwengine kwingi kama Mzumbe, University of Dar es Salaam na
kwengineko.
Ikiwa Tamim ataamua kunyanyua kalamu kuandika yote ayajuayo kuhusu nchi yetu
hicho kitabu kitakuwa rejea ya maana sana.
Nakuwekea picha hiyo hapo chini ambayo tulipiga nyumbani kwangu 1995 wakati
tunaingia katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi.
Waliokaa kushoto: Tamim Faraj, Faraj Mohamed, Prof. Haruna
Lipumba na Dr. Ramadhani Dau. Nyuma kushoto ni Juma Kilaghai
na Mwandishi
Mohamed SaidVerified User ✅
Maalim Faiza,
Nilimheshimu Tamim katika mgogoro wa Zanzibar kuingia katika
Organisation of Islamic Conference (OIC) mwaka wa 1993.
Rais Ali Hassan Mwinyi na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Hassan
Diria walikuwa katika wakati mgumu sana.
Kanisa lilisimama vikali kupinga, magazeti yote yalikuwa yanashambulia
ili muradi Zanzibar ilikuwa mashakani pamoja na Rais Mwinyi na Waziri
Diria.
BAKWATA haikuwa na watu ambao wangeliweza hata kwa mbali kusaidia.
''Enter the Dragon...''
Tamim kila tukikaa kutafakari hali ya nchi yetu anaeleza masikitiko yake
jinsi vyombo vya habari pamoja na magazeti ya CCM na serikali yalivyokosa
adabu kiasi hata cha kumshambulia MwenyeikitI wa CCM Rais Mwinyi.
Kila tukikaa hatuna mazungumzo ila hayo.
Nikikutananae namkuta mwenzangu kesha soma magazeti yote ya siku hadi
''gutter press,'' ananipa ''briefing.''
Ghafla likatokea jambo limezuka vuuu!
Wakati ukifika In Shaa Allah nitalieleza hili la kuzuka.
Ndipo Tamim akaja na kitabu kutoka Nigeria, ''The Two Headed Dragon,''
kitabu kilichokuwa kinaelezea fitna yote ya OIC.
Tamim anakonda panapokuwa hakuna kitu cha kuhangaisha bongo lake
na ananenepa katika, ''crisis.''
''Hawa tunawafungulia front mbili za mapambano tupime ubavu wao.
Tunabisha hodi huko huko kwenye kichaka chao...kisha tunawaleta huku
kwetu wapambane na askari wenda kwa miguu chakula chao biskuti za
chumvi na maji.''
Tamim huyo anakuja na ''strategy,'' ya mapambano.
Bunge lilipigwa na mshangao na barua walizokuwa wanapokea kuhusu
tatizo la Zanzibar kujiunga na OIC kiasi iliulizwa hawa ni akina nani wenye
kalamu kama hii?
Ghafla hali ya hewa Dar es Salaam ikabadilika na Rais Mwinyi akawa kapata
utetezi na watetezi.
Waliokuwa wanamshambulia Rais Mwinyi wakaingiwa na hofu.
Hawakuwa na uwezo wa kufungua, ''front,'' ya pili kuja kulikabili jeshi la,
''infantry.''
Lugha yao ikaanza kubadilika kulikuwa na maneno ya, ''impeachment.''
Msamiati huu ukatoweka ikawa sasa wanasema, ''Baba wa Taifa asaidie.''
''The eagle has landed...''
Ingia hapo chini usome ilikuwaje:
Mohamed Said: Zanzibar Membership to Organisation of Islamic Conference (OIC) and Islam in Africa Organisation (IAO)
FaizaFoxy said: ↑
Hilo nalikubali kabisa.
Tumekaa mimi, Tamim, Hamza Njozi na Prof. Mazrui Kampala Nile Hilton.
Tulikuwa kwenye mkutano na wenyeji wetu wametuweka hapo.
Tamim akawa anavipitia vitabu vya Prof. Mazrui moja baada ya kingine taratibu.
Prof. ''all ears,'' anamsikiza kwa makini.
Tamim akaingia katika kitabu cha Prof. ''The Trial of Christopher Okigbo.''
Prof. akamuuliza, ''Umependa nini katika kitabui kile?''
Bila kupepesa jicho Tamim akamwambia Ali Mazrui, ''They come at midnight...''
Prof. Mazrui alicheka.
Kushoto: Tamim Faraj, Prof. Ali Mazrui na Mwandishi Kampala 2003
Muandishi akimkabidhi Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi kitabu cha Sykes nakala ya Kiingereza na Kiswahili |
No comments:
Post a Comment