Utangulizi
Wapenzi wasomaji nimekuta ujumbe huu katika group moja katika Whatsapp na nimeupenda. Nimeona niuweke hapa kwa faida yetu sote. Ndani ya ujumbe huu kuna mengi ya kuzingatia na pia kushukuru kuwa leo tunaweza tukawakumbuka masultani waliotawala Zanzibar kwa kheri na kisha tukawaombe dua kwa Allah.Maziko ya Sultan Sayyid Khalifa bin Haroub |
Haya ni mazishi ya
Mfalme wa Zanzibar Sayyid Khalifa bin Haroub Albusaidy aliyefariki 1960
alitawala muda wa miaka 49 ilibakia mwaka mmoja tu afanyiwe Diamond Jubilee.
Alikuwa Mfalme mpole
mwenye huruma akiwapenda sana wananchi wake akiwatembelea kwa miguu na akiwahi
kuwaamkia kabla yeye hajaamkiwa akipita pahala watu wote husimama kwa kumlahiki
kwa furaha kubwa wakati anasalimiana nao.
Alipokuwa Uingereza
aliulizwa, "Je nchini kwako kuna siasa za vyama vingi vinavyoshindana si
huenda wale wakagombana wasiwafikiane?
Akajibu, "Habana
hawa ni ndugu hawagombani wanazungumza tu maendeleo ya nchi yao
watawafikiana."
Alikuwa hapendi
ugomvi wala mivutano, alipenda kuona watu wake wanaishi kwa raha.
Siku za Maulidi ya
Mtume SAW watu wa Maulidi ya Home na dhikri wa mashamba wakifika Forodhani
Sultan Palace wakimsomea maulidi na dhikri na yeye akiwapikia biriani nzuri
sana na sharbati ikisha akishuka na marashi akitia marashi kwa mkono wake kisha
akiwatunza pesa na Ahli dhikri na Ahlul Maulidi wakifurahi kwa taadhima na heshima
hiyo kubwa wanayopewa na Sayyid Sultan.
Allah amuweke peponi
pamoja na Mtume wetu Muhammad SAW na Allah atupe baraka zake na madad yake na
Allah aijalie Zanzibar iwe nchi ya amani upendo huruma na mshikamano baina ya
wananchi wake na viongozi wao Amin Amin.
No comments:
Post a Comment