Utangulizi
Hamza Rijal baada ya kusoma niliyoandika kutokana na shajara yangu ya mwaka wa 1991 kuhusu Abdulrahman Babu ameniandikia kitu kwa faragha lakini nimemuomba nikiweke hadharani ili sote tunufaike.
MS
Mwaka wa 1994 nikiwa natokea mji wa
Aberdeen nalifika London kujitaarisha kurudi nyumbani na kuamua kabla sijarudi
nyumbani nifike Sweden kumtembelea dada yangu.
Nilipofika London nilikuwa na siku
mbili zilizofwatana mwanana, siku ya Alkhamisi nilifika kwa Sheikh Mohammed
Abubakar kulikuwa na Mawlid ya Samti Dura na nilikutana na jamaa wengi hapo,
nikaambiwa bada ya miaka kuwa hadhara hio mara Imam Hamza Yusuf wa California
huibuka, yrati ningekutana naye.
Nilikutana na kijana wa Malaysia alio
Radical mawazo yake yalikuwa makali mno juu ya Ulimwengu wa Uislamu na njia ya
kupenya, alikuwa na fikra sambamba na za Waziri Mkuu wake Dr. Mohammed
Mahathir.
Siku iliofwatia ilikuwa Ijumaa ikawa
kwenda kumjulia hali Abdulrahman Mohammed Babu, tuliofika hapo alikuwa Ahmed
Rajab, Abdulaltif Abdalla, Adanani na mie.
Ukweli khulqa ya Babu ni tafauti sana
na watu waliofika makamo yake yeye, kwani mie nilitaka kumsikia anazungumzia
mambo mengi kama nilivyokuwa namsoma, lakini Babu alikuwa mara zote akinirushia
masuala kutaka kujua fikra zangu juu ya nyumbani na kuelekea Uchaguzi wa 1995
aidha alikuwa akitaka kufahamu msimamo wangu juu ya Ghadafi na ninamuonaje
katika harakati zake za Umajumui wa Kiafrika. Ukweli siku hiiio nilipatikana
kwani mambo yalikwenda kinyume na matarajio yangu, ila Babu mbali ya tabia hio
aliokuwa nayo kutaka kusikiliza rai za watu wengine aidha alikuwa anataka
kufahamu fikra za mtu kama mie niliosma Libya kisha nikaja kuyaona maisha ya
Uiengereza fikra zangu zikoje?
Nilijititimua kuzielezea afkar zangu
na bara letu linavyokuwa na muelekeo na mawazo yangu mengi yalijengeka kutokana
na Maktaba ya Jamia Gharyounus iliopo Benghazi, Maktaba hio katika upenyu wa
vitabu vya Siasa na African studies ilikuwa ni wewe tu uwezo wako, mfano
vitabu vya Franz's Fanon alivyoandika yeye na wale waliomzungumza vyote
utavikuta, vitabu juu ya Che Guevera, vitabu juu ya Nkurumah, Maktaba hio
ilikuwa hata kama umelala kifikra basi utaamaka tu.
Aidha nilipokuwa Aberdeen University,
Queen Mary Library nayo sio kalili, hapo hasa hubeba vitabu vya nje ya
Takhasusi yangu siku ya Ijumamosi na Ijumapili nikajisomea, saa nyengine
hujisemesha mwenyewe, ewe hapa hujaja kusoma History na Political Science, lako
ni Ecology.
Siku hio ilikuwa masaa mawili kwangu
na Babu ni kama dakika 15, nalipenda nipate fursa ya kuwa naye zaidi.
Bada ya hapo nilikuwa nina hamu sana
nikutane na Al-Marhum Ali Muhsin Barwany, nikitaka nipate fursa nizungumze naye
na yaliopita Zanzibar, juu ya Tafsiri yake ya Quran, maisha yake ya Jela huko
Bara na maisha ya Sheikh Muhsin Barwany, kwani wakati huo nimerudi nyumbani
nikiandika juu ya Masheikhe waliopita, sijabahatika kukutana na Sheikh Ali
Muhsin, nilikuwa nikutane naye kisha nimrudie Babu nimsikie yake atayasemaje?
Babu sijawahi kumuuliza kwanini
alitoka ZNP na kunda Umma Party lakini nilitaka nimuulize Sheikh Ali Muhsin
ilikuwaje Babu kuhama Chama? Ningekutana na Sheikh Ali kisha Babu kwa mara
nyengine ningekuwa na mengi katika ya kuyaelezea.
Nilibahahatika kuwa nikikaa baraza
mmojana Al Marhum Maalim Aboud Maalim katika mtaa wa Kisimajongoo, kila
akija Unguja iliuwa hufika kwenda kupiga soga, Maalim Aboud amenieleza mengi na
nimefahamu mengi ambayo yananisaidia kufahamu siasa za Tanzania na Ulimwengu wa
Kiislamu kwa jumla.
No comments:
Post a Comment