Saturday 25 March 2017

COSY CAFE DAR ES SALAAM ''KIJIWE'' CHA JULIUS NYERERE NA ZUBERI MTEMVU 1950s


Cosy Cafe

Ilikuwa Julius Nyerere akiwa rais wa TANU ndiye aliyemshawishi Zuberi Mtemvu kuacha kazi na kuwa mtumishi wa kuajiriwa wa TANU. 

Mtemvu akaacha kazi kama Assistant Wlefare Officer na kuwa mtumishi wa TANU kama Secretary General wa kwanza wa TANU. 

KIla siku asubuhi Mwalimu Nyerere na Zuberi Mtevu walikuwa wanakunywa chai pamoja Cosy Café na kupanga ya kufanya kwa siku nzima huku wakistaftahi.

Mtemvu alikuwa akiishi Mtaa wa Somali Gerezani na Nyerere alikuwa akiishi Magomeni Maduka Sita. 

Miaka hiyo ya 1950 Cosy Café ilikuwa moja ya hoteli zenye hadhi yake. 

Jengo hili hadi leo bado lipo Mtaa wa Mkwepu, Dar es Salaam. 

Kwa hakika Cosy Cafe ni moja ya sehemu ya kumbukumbu katika historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Kulia: Zuberi Mtemvu, Julius Nyerere na John Rupia
Nyuma  ni Kundi la Bantu Group waliokuwa wanatoa ulinzi kwa viongozi wa TANU angalia silaha za jadi walizobeba wakati ule Nyerere akivuta sigara angalia kiberiti mkononi kwake na pakiti ya sigara kwenye meza. Picha hii ilipigwa 1955 kwenye tawi la TANU alilofungua Ali Msham nyumbani kwake Magomeni Mapipa na Ali Msham ni huyo aliosimama kulia mwenye shati jeupe.

No comments: