Sunday, 19 March 2017

KATIKA JUHUDI YA KUWATENGENEZA TON TON MACOUTE WETU


Ndugu zanguni kuna mtu akiitwa Papa Doc akitawala Haiti...huyu jamaa alikuwa na stori nzuri sana za kusisimua kama we ni msikilizaji isiwe mkasa uko kwako...alikuwa na rafiki zake wanaitwa Ton Ton Macoute...hawa jamaa walikuwa mabingwa sana kwa hakika walikuwa wataalamu...      
                 
Ton Ton yaliyokuwa yanatisha wananchi si yale marungu yao au bunduki au nondo zao za  chuma kigumu la hasha. Ton Ton wakitisha kwa zile, ''sun glasses,'' yaani miwani ya jua waliyokuwa wakivaa hadi usiku...

Hawa jamaa wakijua kazi yao...

Maana wananchi hawagwai kwa zile silaha za moto au vitu vyenye ncha kali...aaa...wao wanaogopa miwani ya jua...
                       
Usisikie bwana Afrika sisi mabingwa wa kuiga...tukikuusudu tunakuiga. 

Komando Hamza Kalala waimbaji wamesimama kuimba wameachia ala zitembee. 

Komando Hamza  Kalala anatia gita la Franco na vyombo vyote wanashusha mipigo ya TP OK Jazz. 

Unakuja kujua kuwa si OK Jazz pale utakaposikia mwimbaji anaita, "Oh! Kalala we!" 
Sasa siku nyingi tumeanza kuiga vitu vya ki-Ton Ton Macoute...kitu Zombies hivi...

Fela Kuti alitunga nyimbo kuhusu hawa jamaa...

Kuna Dally Kimoko...mtoto ana balaa na gita la Maestro Lwambo...ukimsikiliza unasema ndiye mwenyewe Franco kafufuka...

Tunakwenda vizuri ila itabidi kuboresha kidogo kwa kuvaa miwani ya jua...
Ton Ton Macoute wanapendeza sana kwenye picha wakiwa ndani ya ''sun glasses.''

No comments: