Tuesday, 28 March 2017

KUTOKA WHATSAPP GROUP: MAALIM SEIF NA PROF. LIPUMBA UCHAGUZI WA ZANZIBAR 1995





Mtoro: Sheikh Mohamed Said ; on your opinion what is the ultimate of CUF ?                       
Nimekuandika kisha nimefuta...naogopa hata kusema kaka.
Umeweza kusoma mwandiko wangu?
1995 Uchaguzi Mkuu siku chache kabla ya ‘’D Day,’’ taarifa zilizotufikia tukiwa Zanzibar ni kuwa CCM wameelekezwa wakapige kura mapema sana halafu maskani watafanya vurugu CCM ikiwa inaongoza na ''riot police,'' wataingia na vituo vitafungwa CCM wakiwa wanaongoza mbele ya CUF.

Hizi ndizo taarifa tulizokuwanazo.

Kwa nini iwe hivyo?

Dalili zote zilikuwa zinaonyesha kuwa CUF itashinda uchaguzi sasa njia ya ku-''pre empty,'' ni CCM kuwahi mapema kupiga kura kisha vurugu.

Vumbi litakapotulia na kuanza kuhesabu kura itaonekana CUF walikuwa wanashindwa uchaguzi wakaamua kufanya fujo.

Lakini CUF ni chama kina mshikamano na nidhamu ya ajabu.

Wanachama wameambiwa baada ya Salat Fajr unatoa salamu ya upande mmoja unanyanyuka unakwenda kituoni kupiga kura.

Hakuna kuvuta uradi. Uradi utavuta njiani.

Siku hii ya Jumamosi 21 Oktoba 1995 Prof. Lipumba akaunguruma Kibanda Maiti akasema kumwambia Rais Ali Hassan Mwinyi yeye kama, ''Commander in Chief,'' ana nguvu ya kuzuia damu isimwagike Zanzibar katika uchaguzi.

Hotuba hii ilinyanyua nyoyo za CUF Zanzibar.

Sheikh Mtoro mimi nipo, ''on the ground,'' naona kila kitu kwa macho yangu tena, ''at 0 distance.''

Naam matokeo Tume ya Uchaguzi Zanzibar wameshindwa kuyatoa wanaingia na kutoka hawajui nini wafanye. Ukweli umewadhihirikia...

Maalim kashinda?

Matokeo yale mimi hadi leo ninayo na naweza nikayaweka In Shaa Allah mkayasoma kama somo la historia.

Ali Ameir akaandika barua Tume kukataa matokeo ya Uchaguzi wa 1995 Zanzibar.

Leo ninaposikia kuwa Prof. Lipumba kamfukuza Maalim Seif nafasi ya Katibu Mkuu CUF kwangu mimi mengi yanarejea kwenye fikra zangu...

Hakika siasa ni mchezo mchafu!

No comments: