Kushoto
ni Rajab Diwani Kamanda wa Vijana wa TANU.
Kulia ni mama yake Nyerere Bi. Mugaya.
Rajab Diwani alikuwa
fundi seremala Mtaa wa Congo ilipokuja TANU akawa mstari wa mbele na alikuwa
mtu wake sana Mwalimu na kamfanyia mengi hii picha ni Karimjee hapa Dar es
Salaam.
Hapo
karibu ya Nyerere lakini haonekani katika picha hii yuko Sheikh Issa Nassir
kutoka Bagamoyo.
Huyu
alikuwa bingwa mtaalamu wa falak na majini.
TANU
ilisheheni wajuzi kaka usifanye maskhara.
Ukitaka
lugha ya Kiingereza utapambana na Steven Mhando, Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na
Julius Nyerere.
Ukitaka
wababe wasioogopa mtu utamkuta Ally Sykes.
Ukitaka
bingwa wa kuwasimanga Waingereza wasio na kwao kung'ang'ania nchi za wenzao
utamkuta Bi. Titi.
Ukitaka
wahamasishaji utapambana na Rashid Sisso na Bantu Group.
Watu wa
‘’Intelligence,’’ utamkuta kaka yangu Hassan Upeka na Kitwana Zangira.
Ukitaka
watu wenye noti zisizo na kikomo
utamkuta John Rupia, ‘’The Bank,’’ Waziri Dossa Aziz, Abdul na Ally Sykes kisha
wazee wao wa mjini Mwinjuma Mwinyikambi, Max Mbwana na Mshume Kiyate wazee
karim hujapatapo kuona.
Ukiwataka
masheikh wa sifa utakutana na Mufti Sheikh Hassan bin Amir na mwanafunzi wake
Abdallah Chaurembo.
Walikuwepo
pia waliopungukiwa na akili...wanataka kesho Nyerere atangaze Mau Mau...
Ukitaka
wabishi wapo Zuberi Mtemvu Dar es Salaam na Ali Migeyo Bukoba
No comments:
Post a Comment