Thursday 25 May 2017

KITWANA KONDO ALIPOMFICHUA MPELELEZI WA WAINGEREZA NDANI YA TANU 1




Leo katika maziko ya Mzee Kitwana Kondo niliombwa nizungumze maneno machache kuhusu mzee wangu huyu. Ukweli ni kuwa nilikuwa nimeshtukizwa kwani sikutaarifiwa kabla kuwa niko katika orodha ya wazungumzaji. Lakini mtu ukitumwa na waliokupita makamo huna khiyari ila kutii. Ndipo nilipozungumza yale yaliyopitika baina yangu na Mzee Kondo tarehe 12 Septemba 2012 nilipokwenda kufanya mahojiano na yeye kwa ajili ya kipindi changu cha TV Imaan, ‘’Walioacha Alama Katika Historia.’’ Siku ile wakati vijana wa picha na sauti walipokuwa wanajitayarisha kurekodi ghafla Mzee Kondo akaniita akanambia nikakae pembeni yake ana jambo anataka kuniambia. Ndipo akanieleza haya ambayo ninayeleza hapo chini bila kutaja jina la mpelelezi yule, jina ambalo Mzee Kondo alinitajia na akaniambia nisieleze historia hii hadi yeye atakapokuwa ameondoka duniani.



Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Abdulrahmani Kinana

Mzee Ngombale Mwiru akitoa rambirambi

Kleist Abdulwahid Sykes katika mazishi ya Mzee Kondo
Edward Lowassa

No comments: