SAUL BERENSONSenior Member
Leo ilikuwa ni KHITMA kwenye club yetu SAIGON social club, kurehemu wazee na ndugu zetu wa Kariakoo waliotangulia kwa Mwenyeenzi. Mungu aendelee kutusitiri kwa rehma zake, Amin
Attached Files:
SAUL BERENSONSenior Member
KHITMA SAIGON Club leo hiii
kayamanJF-Expert Member
kwanini function zenu zinafanyika kwa kufuata tamaduni za kiislam?
Je unaona mnawatendea haki wanachama wenu walio na imani tofauti?Mohamed SaidVerified User ✅
Saigon asili yake ni Everton na tukivaa jezi za bluu kama Everton
ya Liverpool, Uingereza.
Katika miaka ya 1960 tukiwa watoto wadogo wa Karikaoo wastani
wa umri wetu ulikuwa kiasi miaka 12 mchezo ukiokuwa mashuhuri
kwa watoto wa Kariakoo ilikuwa ni mpira.
Kama unavyojua hii Karikaoo waliokuwa wanaishi hapo walikuwa
Waislam.
Hii club ya Saigon hadi leo unavyoiona wanachama ni walewale
watoto wa 1960 ambao sasa tumekuwa watu wazima.
Sasa sisi ni Waislam na tumeenea katika club yote ingawa hatubagui
wanachama wa dini nyingine kwani wamekuwapo siku zote.
Kuwarehemu wanachama na wazee wetu waliotangulia mbele ya haki
hii ni ada yetu na haikuanza leo ni kitu kipo katika mila na utamaduni
wetu ambao kwa kuwa sisi ni Waislam basi inabidi tufanye shughuli
yetu kama ada yetu ilivyo.
Ndugu zetu wasio Waislam si kama wanajumuika nasi katika hili bali
wanatoa michango ya hali na mali kufanikisha hii dua tuifanyayo kila
mwaka.
Imekuwa hivi miaka yote na wala hawajaonyesha dalili za kukereka.
Waungwana ndivyo walivyo.
Si hili ti bali hata Mwezi Mtukufu wa Ramadhani tunafanya futari na
sote tunakuwa pamoja katika kufuturu.
Hii ndiyo, ''spirit,'' ya Saigon na haijawa tatizo sasa inakaribia nusu
karne.
Inashangaza kuwa wewe si mwanachama lakini roho inakuuma na
unakuja na fitna.
Fitna ni mbaya kuliko kuua.
Fitna inaigawa jamii.Mohamed SaidVerified User ✅
Ahsante kwa kutuadhimisha.
Sunday, 7 May 2017
KUTOKA JF: JF WAIZUNGUMZA KHITMA YA SAIGON 2017
About Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment