Monday 22 May 2017

KUTOKA JF: WANAULIZA BILAL REHANI WAIKELA NI NANI KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA?

  1. https://www.jamiiforums.com/threads/bilal-waikela-ni-nani.422442/page-3#post-21245023
    Peter maickoMember

    #1
    Mar 23, 2013
    Joined: Jul 21, 2012
    Messages: 12
     
    Likes Received: 1
     
    Trophy Points: 0














    Katika ile kesi inayomkabili sheikh ponda ambayo kwa sasa inaendelea kwa kutoa utetezi kwa upande wa washitakiwa,juzi alisimama mzee mmoja aitwae bilal waikela ktk kutoa ushahidi kwa upande wa mshitakiwa.

    Mzee huyo mwenye mvi zenyekuonesha kiasi ya chumvi aliyokula alielezea historia fupi juu ya kiwanja cha chang"ombe na bakwata.

    Pia alimuelezea mwalimu nyerere juu harakati zake za kuivunja EAST AFRICA MUSLIM SOCIAL WELFARE na kuunda BAKWATAA kama chombo cha Waislamu tz.kwa ufupi ameelezea mengi kuhusu bakwata,serikali na Nyerere.

    Nahisi ni bora tukamjua ni nani,anamchango ganiktk kutafuta uhuru na undani ndani wa uwepo wa bakwata na wanachodai waislam juu ya mchango wao ktk uhuru wa nchi wa shutuma zao juu ya serikali zote zilizopita tangu ukolon mpaka uhuru.

    Swali la msingi NI NANI BILaL WAIKELA
  2. expirience man

    expirience manSenior Member

    #21
    Today at 10:27 AM
    Joined: Nov 16, 2013
    Messages: 141
     
    Likes Received: 29
     
    Trophy Points: 45




























    Mimi namuelewa mzee MOHAMEDI SAID lkn hebu sasa eleza usahihi wa kile unachokijua wewe, Mzee wangu Mohamedi yeye hicho unchotaka akiseme hakijui eleza wewe hiyo historia itakayoutenga uislm ma harakati za uhuru. Historia yetu inayowaficha wapigania uhuru ingewaficha wote basi na sio hao akina waikela peke yao. Na kama waliofichwa na watu wanaolekea kuwa na mlengo mmoja tu wakiitikadi basi tuseme huyo mgen alikuwa na ajenda yake ya dini na ndicho kinchopelekea kuleta huo mkanganyiko.
  3. Mohamed Said

    Mohamed SaidVerified User 

    #22
    Today at 10:46 AM
    Joined: Nov 2, 2008
    Messages: 9,859
     
    Likes Received: 4,262
     
    Trophy Points: 280




























    Kokola,
    Wala sitakulaumu kwa kuona neno ''upuuzu,'' si tusi na mara nyingi
    lugha mfano na hii yako nakutananayo hapa jamvini.

    Kwetu siye hilo ni tusi.

    Ingekuwa mimi ningeweza kuandikia sentesi hiyo hiyo bila ya kutumia
    neno, ''upuuzi.''

    Tofauti kati yangu mimi na wewe ni kuwa mimi kwanza ingawa hii nini
    historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kubwa ni kuwa historia hii
    imewahusu wazee wangu.

    Kwa ajili hii basi mimi nayajua mengi ambayo wewe huyajui.

    Ukweli ni kuwa palikuwapo na bado ipo njama ya kuifuta historia hii
    na laiti kama nisingeliandika historia hii mengi yasingejulikana.

    Hili la Uislam katika historia ya TANU huwezi kuliepuka hata ukifanya
    nini kwa kuwa ndiyo historia yenyewe ilivyokuwa na mifano iko wala
    si ya kutafuta.

    Waasisi wa African Association 1929 ndiyo hao walioasisi Al Jamiatul
    Islamiyya Fi Tanganyika 1933.

    Al Jamiatul Islamiyya ndiyo iliyotoa viongozi wa mwanzo wa TANU na
    wanachama wake.

    Mimi sijaona ubaya wowote katika kuandika historia hii.

    Idd Faiz Mafungo kadi yake ya TANU ni No. 25 na yeye ndiye alikuwa
    mweka hazina wa Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika na pia mweka
    hazina wa TANU.

    Idd Faiz ndiye aliyekuwa mkusanyaji wa fedha za kumpeleka Nyerere UNO
    mwaka wa 1955.

    Umepata popote kumsikia akitajwa?
  4. K

    KokolaSenior Member

    #23
    Today at 11:01 AM
    Joined: Sep 5, 2015
    Messages: 131
     
    Likes Received: 71
     
    Trophy Points: 45




























    Ndugu Expirience man nachotaka kusema nishasema labda hujakielewa hilo moja, pili kama hao wageni walikuwa na ajenda ya kidini je sisi katika kurekebisha makosa yao ndio tuegemee kwenye ajenda ya udini pia..? Hekima hiyo unavyoona wewe!!! Na haswa ukizingatia udini huo unachangia kutugawa na hivyo kutudhoofisha..?!!
  5. Mwanamageuko

    MwanamageukoJF-Expert Member

    #24
    Today at 11:16 AM
    Joined: Oct 31, 2010
    Messages: 2,114
     
    Likes Received: 194
     
    Trophy Points: 160




























    Mkuu, Heshima kwako. Kikawaida Historia inapogusa mambo ambayo wengi hatuyapendi huwa inaleta ukakasi hata katika kuisoma. Yupo soko la mitumba Manzese mwanae Mzee Waikela anaitwa Ramadhani Waikela Pasco anaweza kumtafuta atapata anayoyataka maana Mzee Waikela hakuwa na khofu kuusimulia ukweli kwa yeyote maisha yake yote.
    SIGNATURE













  6. Mwanamageuko

    MwanamageukoJF-Expert Member

    #25
    Today at 11:21 AM
    Joined: Oct 31, 2010
    Messages: 2,114
     
    Likes Received: 194
     
    Trophy Points: 160




























    Mkuu udini Tanzania haukwepeki kama Kompyuta zilivyokosea katika kufelisha waislamu!! Mkuu Ukabila pia haukwepeki kama bado tunabaguana kwa makabila "hawa wa kaskazini hawafai kuongoza... hawa vibalagashia hawakusoma nk!!"
    SIGNATURE













  7. expirience man

    expirience manSenior Member

    #26
    Today at 11:57 AM
    Joined: Nov 16, 2013
    Messages: 141
     
    Likes Received: 29
     
    Trophy Points: 45




























    unakwepaje historia ya uislam ktk uhuru wakat hata hao wapigania uhuru mwanzo walikutana kwenye hizo taasisi za dini na kuanzia harakati huko hapa ipo taasisi kama JAMIIATUL ISLAMIYA FI TANGANYIKA. Najua historia ikiongea mambo usoyapenda utapinga tu lkn ndo inabaki kuwa historia tu. Hata mtu akikambia baba yako mzazi aliyekuzaa alikua mlevi hutopenda kusikia historia hiyo. hebu mfuate bilalal waikera anaijua historia kuliko wewe ulioyosoma ya magogoni ya kuinjinia hiyo!!
  8. expirience man

    expirience manSenior Member

    #27
    Today at 12:00 PM
    Joined: Nov 16, 2013
    Messages: 141
     
    Likes Received: 29
     
    Trophy Points: 45




























  9. expirience man

    expirience manSenior Member

    #28
    Today at 12:00 PM
    Joined: Nov 16, 2013
    Messages: 141
     
    Likes Received: 29
     
    Trophy Points: 45




























  10. T

    tuneneNew Member

    #29
    Today at 12:35 PM
    Joined: Mar 14, 2017
    Messages: 3
     
    Likes Received: 6
     
    Trophy Points: 5




























    Hili suala naona watu mnalipeleka kwenye udini.kwani kama waislamu walishiriki kupigania Uhuru wetu,je kulikuwa na makubaliano waliyowekeana kwamba baada ya Uhuru waislamu wapewe upendeleo na nchi hii iwe na sheria za kiislamu?
    Kama hakukuwa na makubaliano lawama za waislamu zinatoka wapi.tukumbuke pia harakati za Uhuru sio kweli kwamba wakristo hawakushiriki kabisa walishiriki mfano ni Mwl Nyerere.
    Wakati tunapata Uhuru kanisa la wasabato Tanzania ndilo lililokuwa na mashule mengi kuliko makanisa yote hapa Tanzania wakati huu.
    Serkali chini ya mwalimu Nyerere ikazitaifisha shule zote za kanisa LA wasabato na kuzifanya za serkali.mbona wasabato hawalalamiki kwamba wanaonewa na serkali. Ebu tuweke utaifa Mbele tuache udini
  11. G

    golden prideMember

    #30
    Today at 1:00 PM
    Joined: Oct 24, 2014
    Messages: 76
     
    Likes Received: 1
     
    Trophy Points: 15














    duh
  12. A

    Al-WatanJF-Expert Member

    #31
    Today at 1:13 PM
    Joined: Apr 16, 2009
    Messages: 2,060
     
    Likes Received: 2,056
     
    Trophy Points: 280




























    Tena dini zenyewe bora hata zingekuwa zetu kweli.

    Zote za kuletewa na meli.

    Zote zina mambo tofauti sana na tamaduni zetu.

    Na tumezibugia kama mtu mwenye njaa kwenye dhifa.
  13. Mohamed Said

    Mohamed SaidVerified User 

    #32
    Today at 2:10 PM
    Joined: Nov 2, 2008
    Messages: 9,859
     
    Likes Received: 4,262
     
    Trophy Points: 280




























    Experience...
    Sheikh Hassan bin Amir ndiye alikuwa Mufti wa Tanganyika katika
    miaka ile ya 1950.

    Mwaka wa 1950 TAA ndani yake ilianzisha kamati iloiyopewa jina la
    TAA Political Sub Committee.

    Sheikh Hassan bin Amir alikuwa mmoja wa wanakamati hii, wengie
    ni Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Steven Mhando, John Rupia,
    Sheikh Said Chaurembo.

    Kamati hii ndiyo iliyoweka mipango ya kuunda TANU na TANU ilipoasisiwa
    mwaka 1954, Sheikh Hassan bin Amir akawa anauza kadi za TANU
    msikitini.

    Mtoro Rehani aliuziwa kadi ya TANU na Sheikh Hassan bin Amir ndani
    ya msikiti.

    Haiwezekani ukaandika historia ya TANU na haya yakawa hayapo.
    Hii ndiyo historia yenyewe ya TANU.
  14. Mohamed Said

    Mohamed SaidVerified User 

    #33
    Today at 2:15 PM
    Joined: Nov 2, 2008
    Messages: 9,859
     
    Likes Received: 4,262
     
    Trophy Points: 280




























  15. N

    ngozimbiliJF-Expert Member

    #34
    Today at 2:20 PM
    Joined: Jul 28, 2011
    Messages: 719
     
    Likes Received: 146
     
    Trophy Points: 60




























    Ukweli haudhoofishi bali utatufanya tuwe imara zaidi kama Marekani pamoja historia ya utumwa, bado weupe na weusi wanajenga nchi yao
  16. Mohamed Said

    Mohamed SaidVerified User 

    #35
    Today at 2:22 PM
    Joined: Nov 2, 2008
    Messages: 9,859
     
    Likes Received: 4,262
     
    Trophy Points: 280




























    Tunene,
    Hili la makubaliano umelitoa wapi?
    Wapi imesemwa kuwa Waislam wanataka upendeleo?

    Wapi zimelelezwa habari za Wasabato na shule zao?

    Hapa mimi nimeeleza historia ya Bilal Rehani Waikela.
    Ikiwa unataka tujadili kutaifishwa kwa shuke basi fungua
    uzi mwingine.
  17. skfull

    skfullJF-Expert Member

    #36
    Today at 2:33 PM
    Joined: Dec 24, 2013
    Messages: 1,101
     
    Likes Received: 270
     
    Trophy Points: 180




























    Nimejikuta roho imeniuma sana kusoma ukurasa huu sijui kwann, dah mungu unusuru uisilam na watu madhalimu
  18. A

    Al-WatanJF-Expert Member

    #37
    Today at 2:39 PM
    Joined: Apr 16, 2009
    Messages: 2,060
     
    Likes Received: 2,056
     
    Trophy Points: 280




























    Hujaandika kwa msisitizo wa habari za Waislamu?

    Kwa nini uislamu uwe muhimu sana?
  19. Mohamed Said

    Mohamed SaidVerified User 

    #38
    Today at 2:48 PM
    Joined: Nov 2, 2008
    Messages: 9,859
     
    Likes Received: 4,262
     
    Trophy Points: 280




























    Al Watan nimeandika kitabu kizima ambacho kinaitwa, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes the Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika." Umuhimu wake ni kuwa walijitolea kupambana na ukoloni.


  20. A

    Al-WatanJF-Expert Member

    #39
    Today at 2:56 PM
    Joined: Apr 16, 2009
    Messages: 2,060
     
    Likes Received: 2,056
     
    Trophy Points: 280



























    Kwa watu wanaotaka kujenga umoja wa kitaifa, kuanza kuwagawa Watanganyika kwa mafungu ya kidini ni kuharibu umoja wa kitaifa.

    Unawaambia wao si wamoja. Kuna waislamu na wakristo.

    Sasa hapo kwenye waislamu napo aje mtu aandike kuhusu mchango wa Shia. Wa Shia nao watuambie Wa Ismaili na Zaydi nao walikuwa na mchangi wao tofauti.

    Mimi naamini katika kuandika historia, maadam kilichoandikwa ninkweli, lakini naamini pia kwamba unaweza kuandika historia ikaleta kupinda ukweli.

    Hususan kama historua yenyewe imekitwa kwenye hizi "imagined realities" za dini za kutungwa.

    Hapo ndipo mnapowapa msemo wale watu wanaosema kwamba nia ya Uislamu ni kutawala dunia na popote pale ambapo uislamu haujatawala, utataka kunung'unika na kuua mpaka utawale.

    Kwamba mnanung'unika sio kwa sababu mmeonewa (Wasabato wameonewa, makanisa yamenyang'anywa shule etc lakini hatuwasikii wakilalamika kama nyinyi) ila mnalalamika kwa sababu mmefundishwa kuchukua nchibkwa upanga na kueneza dini dunia nzima kama ilivyoenea kutoka Uarabuni mpaka Spain.

    1. Al-WatanJF-Expert Member

      #41
      Today at 3:18 PM
      Joined: Apr 16, 2009
      Messages: 2,062
       
      Likes Received: 2,056
       
      Trophy Points: 280




















      Mbona sasa hutaji Waislamu?

      Utapigania vipi uhuru wa Tanganyika na kukumbatia dini inayokutia utumwa kwa kukuambia ukisali lazima uisujudie Maka?

      Ukikubali masharti ya hiyo dini wewe Muafrika utakuwa huru kimawazo kweli?

      Uislamu ni utumwa. Neno "Islam" linakutaka uwe mtumwa wa Allah.

      Allah hayupo. Ni Mungu katungwa tu na waarabu.

      Kwa maana nyingine ukikubali kuwa Muislamu, unakubali kuwa mtumwa wa utamaduni wa Waarabu.

      Ndiyo maana watu wanasomeshwa Quran Kiarabu hata hawaelewi wanasoma nini.

      Ndiyo maana Waislamu wanasali wakielekea Maka.

      Sasa utasemaje watu wamepigania uhuru wa Tanganyika ili tu kuubadilisha na uhuru huu na utumwa mbaya sana wa kimawazo wa Uislamu?

      Muislamu si mtu huru. Ni mtumwa siku zote.

      Jina tu "Islam" maana yake ni kukubali kuwa mtumwa. You submit yourself to another.
    2. T

      tuneneNew Member

      #42
      Today at 3:43 PM
      Joined: Mar 14, 2017
      Messages: 3
       
      Likes Received: 6
       
      Trophy Points: 5










      Mazungumzo yale na Mzee Waikela ndiyo yaliyotengeneza sehemu ya tatu katika
      kitabu cha Abdul Sykes na sehemu hiyo nikaipa jina, ''Njama Dhidi ya Uislam (1961 -
      1970).''[/QUOTE] mleta hoja unachobisha ni nini watu tunakuambia hapa unatuletea udini unabisha .kama hoja yako ilikuwa ni kutujulisha wanaharakati waliopigania sisi kupata Uhuru,basi hoja yako ungejikita kutuelezea wasifu wao na namna alivyochangia katika harakati.
      Ajabu unatuletea habari za mpigania Uhuru huku hoja yako imebezi kwenye uislamu.tena unadiriki kuandika kabisa akaniambia andika uwambie waislamu.nawe ukaandika kitabu njama dhidi ya uislamu.
      Alafu unatuambia nilikuwa huzungumzii udini je ulipoandika "njama dhidi ya uislamu " ulikuwa unamanisha nini.kama sio kupandikiza chuki za udini kwa waislamu kwamba mmedhurumiwa sana tangu kudai Uhuru.
      Umechemka sana usiwe unatuletea porojo porojo zako hapa za udini ukidai ni harakati za uhuru.unadhani hatuijui fasihi



    3. Mohamed Said

      Mohamed SaidVerified User 

      #43
      53 minutes ago
      Joined: Nov 2, 2008
      Messages: 9,859
       
      Likes Received: 4,262
       
      Trophy Points: 280




















      Al Watan nimekusoma.
      Ahsante.
       tunene said: 








      mleta hoja unachobisha ni nini watu tunakuambia hapa unatuletea udini unabisha .kama hoja yako ilikuwa ni kutujulisha wanaharakati waliopigania sisi kupata Uhuru,basi hoja yako ungejikita kutuelezea wasifu wao na namna alivyochangia katika harakati.
      Ajabu unatuletea habari za mpigania Uhuru huku hoja yako imebezi kwenye uislamu.tena unadiriki kuandika kabisa akaniambia andika uwambie waislamu.nawe ukaandika kitabu njama dhidi ya uislamu.
      Alafu unatuambia nilikuwa huzungumzii udini je ulipoandika "njama dhidi ya uislamu " ulikuwa unamanisha nini.kama sio kupandikiza chuki za udini kwa waislamu kwamba mmedhurumiwa sana tangu kudai Uhuru.
      Umechemka sana usiwe unatuletea porojo porojo zako hapa za udini ukidai ni harakati za uhuru.unadhani hatuijui fasihi[/QUOTE]

    4. Tunene,
      Hakika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika imejaa Waislam kila kona.
      Ukijaribu kuwaondoa utakuwa umetoa sehemu kubwa ya historia ya kweli.



    5. Kitabu cha Abdul Sykes kilipochapwa London mwaka wa 1998 kilipofika Dar
      es Salaam kishindo kilikuwa kikubwa.

      Walipigwa na butwaa wale waliokuwa wanaijua historia ya uhuru kupitia
      historia rasmi iliyoandikwa na Chuo Cha Kivukoni mwaka wa 1981.

      Ndani ya kitabu cha Kivukoni historia ya TANU ilikuwa imefuta majina mengi
      ambayo ndiyo haya sasa mnayasoma hapa ya akina Sheikh Hassan bin Amir,
      Bilai Rehani Waikela na kubwa matatizo yaliyotokea baada ya uhuru moja
      ikiwa ni hili la kufuta historia ya kweli na kuweka nyingine.

      Kuwa mimi nimeandika historia ya Waislam wala sikatai.
      Hiyo ndiyo ilikuwa nia yangu khasa.

      Kuwa palikuwa na njama dhidi ya Uislam baada ya uhuru ni historia ya uhuru
      wa Tanganyika atakae anaweza akasoma akajua kilitokea nini na nani walikuwa
      wahusika wakuu.

      Ikiwa kuna mtu anakerwa na kuandikwa kwa historia hii hiyo ni bahati mbaya
      kwake.

      Ikiwa utaona hizi ni ''porojo,'' una uhuru wa mawazo yako siwezi kukuingilia.

      Unaweza hata ukakataa kuamini kama kulikuwa na Abdul Sykes na nduguye
      Ally wakaunda TANU kutoka African Association aliyoasisi baba yao mwaka wa 
      1929 wakiwa na Nyerere na vijana wengine waliokuwa Dar es Salaam ya 1950s.

      Uhuru ni wako.
      Nakuona umeghadhibika.

      Hili ni katika jambo moja ambalo mimi sikulitegemea wakati naandika historia
      hii.

      Sikutegemea hata siku moja kuwa historia hii ya wazee wangu itawaumiza
      baadhi ya watu.






    Peter...
    Tatizo kubwa sana ninalokutananalo hapa Majilis ni kuwa wengi wenu hamuijui
    historia ya uhuru wa Tanganyika.

    Ingekuwa waasisi wa harakati hizi za kudai uhuru wangejikita katika maslahi ya
    dini zao hali ingekuwa ngumu sana kwa TANU.

    Kabla Abdul Sykes hajakutana na Nyerere 1952 yeye alikuwa na mpango wa
    kumtia Chief Kidaha Makwaia katika TAA kisha waunde TANU na kudai uhuru
    na Chief Kidaha aje kuwa Waziri Mkuu wa kwanza.

    Chief Kidaha hakuwa Muislam na anaetaka kumleta katika TAA Abdul Sykes yeye
    alikuwa katika Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika chama alichoasisi baba yake
    1933 (elewa pia kuwa hata hiyio TAA aliasisi baba yake Abdul, Kleist Sykes 1929
    na akajenga hiyo ofisi ambayo ilikuja kuzaliwa TANU 1954).

    Lakini Hamza Mwapachu yeye alipendelea Abdul amtie Nyerere katika uongozi wa
    TAA kisha ndiyo waunde TANU.

    Nyerere hakuwa Muislam na wanaotaka achukue uongozi wa TAA na kuunda TANU
    ni Abdul Sykes na Hamza Mwapachu, wote Waislam.

    Kabla ya haya mwaka wa 1950 aliyesimama kwa juhudi kubwa kumtia Dr. Vedasto
    Kyaruzi 
    katika uongozi wa TAA kama rais alikuwa Schneider Abdillah Plantan.

    Kabla ya uchaguzi wa mwaka wa TAA 1953 kuchagua rais wake Abdul Sykes na Ali
    Mwinyi Tambwe walisafiri hadi Nansio kwa Hamza MwapachuAbdul akitaka
    kupata kauli ya mwisho ya Mwapachu kuhusu Nyerere kuachiwa na Abdul kiti cha
    urais wa TAA.

    Huyu Ali Mwinyi Tambwe ndiye kwa wakati ule 1950s alikuwa katibu wa Al Jamiatul
    Islamiyya Fi Tanganyika.

    Mwapachu alimwambia Abdul kuwa wakiasisi TANU na yeye Abdul ndiye rais na kudai uhuru harakati zile zitaonekana za Waislam.

    Mwapachu akasema lakini harakati akiongoza Nyerere Mkristo Waingereza watatulia.
  21. Bilal Rehani Waikela hakupata hata siku moja kwenda kinyume na msimamo wa
  22. kiongozi wake Sheikh Hassan bin Amir ambae yeye alimuunga mkono Nyerere toka
    siku ya kwanza alipopelekwa kwake na Abdul Sykes na Dossa Aziz.

  23. Sheikh Hassan bin Amir ndiye aliyefanya juhudi ya kuifanya TANU isionekana kama

    chama cha Waislam katika mkutano wa siri alioitisha usiku Mtaa wa Pemba 1955.

    Hii ilikuwa 1953.

    Bila kuijua historia hii ya uhuru wa Tangnayika mtu atahangaika katika kiza na kujikwaa
    ovyo.
  24. [6:01 PM, 5/23/2017] +255 687 500 699: boywise said: ↑
    Naomba kujua kutoka kwako mlengo wa Mwl Nyerere ambao ulisalimika na "udini" ukiutofautisha na mlengo wa Mzee Bilal Waikela ambao kwa "kudhani" kwako ulitopea kwenye "udini"
    Boywise,
    Nimeeleza kila kitu kuhusu Bilal Waikela katika kitabu cha Abdul Sykes.

    Nitakujibu hapa swali lako lakini kwa kuelewa historia nzima ya TANU
    na uhuru wa Tanganyika ni muhimu sana tena sana ukasome kitabu hiki.

    Farka baina ya Waikela na Nyerere ilitokea mwaka wa 1963 katika mkutano
    wa EAMWS uliofanyika Dar es Salaam Waikela alipomsomea Nyerere risala
    ya Waislam kuhusu chokochoko zilizokuwa zimejitokeza kwa serikali kutaka
    ivunjwe EAMWS wakati walikuwa na mipango ya kujenga Chuo Kikuu.

    Risala hii haijapatapo mwenzake sasa nusu karne imepita.

    Waikela akimtazama Nyerere usoni alimkumbusha juhudi za Waislam katika
    kupigania uhuru wa Tanganyika ili watu wawe huru kutokana na dhulma zote.

    Ukitoa ugomvi wa 1958 baina ya Sheikh Suleiman Takadir na Nyerere hii
    risala ya Waikela ilikuwa inawarudisha Waislam nyuma kutafakari upya hali
    yao ya baadae katika Tanganyika huru.

    Historia ya uhuru wa Tanganyika ina mambo mengi sana ya kusisimua.

    Anaependa kuijua historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika asome kitabu cha
    Abdul Sykes.                        

    Mjadala huu upo hapa:https://www.jamiiforums.com/threads/bilal-waikela-ni-nani.422442/page-4#post-21261467

No comments: