Thursday, 4 May 2017

TAAZIA: SHEIKH ISSA AUSI ''SMART BOY'' KIPENZI CHA KILA MTU NA SALUM MATIMBWA


Sheikh Issa Ausi

Hakika tumeondokewa na kigogo wa Dsaalam aneijua Dsalaam na wana Dsalaam! Mara ya mwisho nimekutana na Mzee Issa Ausi mwezi wa jana ktk mazishi ya Mzee Iddi Sungura Makaburi ya Kisutu.

Akaniita kwa majina yangu yote kwa ufasaha kabisa!

Salum bin Abdallah Salum Matimbwa nikaitika laabek!

Akanishika mkono nimsaidie kuinuka,ili aweze kusogea kaburini na kuweka udongo ktk kaburi la Mzee mwenziwe!

Wakati niko tunatembea taratibu ananiuliza uko wapi Baba siku hizi mbona hatuonani!?

Nikamjibu Baba nipo ila shughuli za kidunia zimetuzonga tu! Akaendelea kuniambia Baba sisi ndiyo tunakwisha hivi, simameni imara ktk mji wenu!

Maskini sikujuwa ndiyo tunaagana na maneno yale ni wasia ananiachia!

Mzee Issa tumemzika leo ktk makaburi ya Ndugumbi Magomeni ndiyo ameondoka kama alivyoniambia! Tunakwisha!!

Mzee Issa ni miongoni mwa wazee wachache ambao waliobakia hai wanomjua vyema Mzazi wangu!

Yeye akimwita Baba yangu ni kaka yake! Baba alifariki 1983 akiwa na umri zaidi ya miaka 90! 

Wote ni Wandengereko! Na siku zote nikukutana nae wakti wa uhai wake haachi kukumbusha mambo mbali mbali ya zamani kuhusu Mzee wangu ambayo mimi siyafahamu kabisa!

Maskini wapi na nani wa kunipa usia wa mjini baada ya kifo cha Mzee huyu!

Hakika tumeondokewa hapa Dsalaam!"TUMEKWISHA" Ndiyo maneno yake ya mwisho kwangu na wana Dsalaam kwa ujumla!!

Buriani Baba yetu Mzee Issa Athumani Ausi "Smart boy"

Mwenyezi Mungu ampe daftari lake kwa mkono wa kulia, amsameh makosa yake! 
Alifanye kaburi lake kuwa moja ya bustani za peponi!!

No comments: