Saturday 17 June 2017

UCHA MUNGU WA MAALIM NA UTAKATIFU NA UENYE KHERI WA MWALIMU BABA WA TAIFA


Utangulizi

Uzuri wa wa mitandao ya kijamii ni kuwa kila ajuaye kuandika na kutumia kompyuta ana nafasi ya yeye kusema alitakalo na wakati mwingine kuwajibu wale ambao hapo kale walikuwa na neno la mwisho. 

Gazeti moja limekerwa na kauli ya Mheshimiwa Riziki Shahari Mngwali Mbunge wa Mafia CUF na kiongozi wa wabunge wa CUF Bungeni na mmoja wa viongozi wa UKAWA kumweleza Maalim pamoja na sifa nyingine kuwa ni Mcha Mungu, wakati akichangia bajeti ya serikali. 

Hili la Ucha Mungu wa Maalim limewakera. 

Wanataka kujua wapi katoa nguvu hiyo ya kumpa sifa kubwa kama hiyo Maalim, Mheshimiwa Riziki kaitoa wapi. 

Swali langu ni kuwa ikiwa gazeti limekerwa na kauli tu ya Ucha Mungu wa Maalim wanasemaje kuhusu utakatifu na uenye kheri wa Mwalimu? 

Wamewahi kuhoji utakatifu na uenye kheri wa Mwalimu kama unavyotangazwa na Kanisa Katoliki au ndiyo kisa kile maarufu cha Baniani?  Onea buji ogopa gombe?





Msikilize Mh. Riziki hapo chini:
http://www.mohammedsaid.com/2017/06/mheshimiwa-riziki-shahari-mngwali-viti.html

No comments: