Saturday 30 September 2017

MBARAKA MWINSHEHE MWARUKA KWA UFUPI

Soloist International Mbaraka Mwinshehe Mwaruka. 

1970 aliporudi kutoka Expo akakuta maneno Dar es Salaam kuwa Morogoro Jazz imependelewa kuchaguliwa kwenda Osaka. Mbaraka akawaambia wenzake kuwa lazima warekodi nyimbo moja kama majibu kisha waende nyumbani Moro. 

Wakarekodi katika studio za TBC ''Maonyesho Japani.''

Mle ndani Mbaraka was at his best guitar alilotia mle na ''melody'' yake si vitu vya kawaida. 

Bahati mbaya sana ni kuwa recording ya TBC ilikuwa nzuri lakini ya Polydor ambayo ndiyo santuri yenyewe haikutoka vyema.

Kuna kitu katika muziki kinaitwa, ''chromatics,'' hii ni kama kupiga danadana katika soka. Ukijua danadana utakuwa na ''ball control,'' nzuri. Sasa sikiliza hiyo ''chromatics.'' pale Mbaraka anaposema. ''Leo nalala Japan...'' nk. 

Si wapigaji wengi wanaweza kusema huku vidole vikitembea kwenye, ''fret.'' 

Nilikuwa na hamu ya kuandika maisha ya Mbaraka na nilianza, ''interview,'' na marehemu Kurwa Salum, saxophonist wake na mtunzi wa nyimbo nyingi za Mbaraka ingawa jina lililotokea lilikuwa la Mbaraka. 

Kurwa Salum alikuwa kila akija Dar es Salaam kutoka Morogoro alikuwa akija kunitembelea ofisini. Wakati ule Kurwa Salum alikuwa kaacha muziki na akiuza mitumba Morogoro Sokoni. 

Roho ilikuwa ikiniuma sana nilipokuwa nikimuona katika hali ile lya unyonge lakini alikuwa sala haimpiti. Nilikuwa nikimstaajabisha sana nilipokuwa nikimwimbia ''chromatics,'' za saxophone lake kwenye nyimbo kama ile waliyoisifia timu ya Morogoro iliyochukua Taifa Cup, ''Twawapongeza Wanasoka Wetu. 

Basi akicheka sana... Sikumaliza hii kazi nikaanza kitabu cha Abdul Sykes...In Shaa Allah atatokea mtafiti ataandika historia za hawa mabingwa wetu wa mindule. Hadi leo Morogoro hawajawapa Mtaa Salum Abdallah wala Kurwa Salum. 

Katika band boys wa Morogoro Jazz kulikuwa na rafiki yangu wa utotoni Maneno Gisha.
Sijamtia machoni sasa lbada nusu karne na sijui kama yu hai au vipi. 

Kurwa Salum ni Mmanyema.
Nataka Salum Matimbwa asikilize hyo saxophone ya Mmanyema...





No comments: