Saturday 30 September 2017

NILIYOMFAHAMISHA PROF. ASARIA MBUGHUNI KUHUSU DR. WILBARD MWANJISI


Mohamed Said Asaria nakuwekea hii ili uone jinsi nilivyokutana na Dr. Mwanjisi katika Nyaraza za Sykes na In Shaa Allah nitakwenda hivi kwa wazalendo wengine ambao si wengi wanajua michango yao katika TANU na kupigania uhuru wa nchi yetu. Haya ni katika mijadala mikali nilikiyokuwa nifanya na jamaa katika JF:

Reply1 hr
Manage
Mohamed Said Alfa Mwijumbe said: ↑
SYKESIOLOGY
Alfa...
Hakika umesema kweli.

Kisa chake kilianza na makala aliyoandika Joseph Kasella Bantu na ikachapwa
na New African (London) March na May 1985.

Katika makala ya Kasella Bantu iliyochapwa mwezi March na gazeti hili alisema
kuwa yeye aliisaidia TAA na TANU kwa kutoa fedha zake mfukoni kuendesha
mambo.

Mimi niliposoma ile makala nikaona kuwa kama suala la fedha wapo waliotoa fedha
nyingi kuendesha TAA na TANU na kubwa ni kuasisi na hivyo vyama vyenyewe African
Association 1929 na TANU 1954.

Mbona wazee wangu hawa siku zote hizi wako kimya hadi anakuja Kasella Bantu
kutaka kuidai sifa ambayo si yake kamwe?

Ikiwa Kasella Bantu anafikia kujinasibu hivi, Abdul Sykes angesema nini ingekuwa
katika uhai wake angeamua kuzungumza au Ally Sykes mwenyewe angezungumza?

[​IMG]

Nikaandika makala kujibu makala ya Kasella Bantu ambayo ilichapwa mwezi May.

Lakini mhariri wa gazeti akaniandikia ujumbe kuniomba nimpe picha yangu kwa
kuwa makala yangu kaipenda sana angependa aichape na picha yangu.

Nilimpelekea picha yangu na ikatoka pamoja na makala ile.

Katika makala ile niliishambulia picha ya waasisi wa TANU ambayo Kasella Bantu
kwenye picha ''original,'' iliyochapwa na makala yake hakuwepo katika picha lakini
akaja kuitia picha halisi mkono kwa kuingiza picha yake.

Katika picha halisi watu watatu walijitoa kwa hofu ya kufukuzwa kazi na serikali kwa
kuasisi chama cha siasa.

Hawalikuwa Ally Sykes, Tewa Said Tewa na Kasella Bantu.

Kwa ufupi katika ile makala nilisema mengi ambayo wengi wakati ule hawakuwa na
ujasiri wa kuyasema ingawa waliyajua.

Ally Sykes aliposoma makala ile aliniita ofisini kwake.
Hapo ndipo mimi nikamwambia kuwa ninataka sana kuandika historia ya kaka yake.

Ally Sykes akaniambia kuwa ana safe imejaa nyaraka nyingi sana za wakati wa
kudai uhuru katika 1950s lakini hajui funguo zake ziko wapi.

Akaniambia nirudi baada ya siku tatu na ikiwa hajaziona funguo hizo ataivunja ile ''safe.''

Nilipokwenda alikuwa kazipata funguo na akanikabidhi kilima cha mafaili na nyaraka
nyingine.

Akanambia, ''Mohamed kasome kisha rejea tuzungumze.''

Hizi nyaraka hakuna mtafiti yeyote kabla yangu aliepata kuziona na zilikuwa ndani ya
''safe,'' kwa karibu miaka 30.

Sikuweza kuamini macho yangu kwa kile nilichokuta katika majalada yale.

Barua kutoka kwa Rashid Kawawa, Julius Nyerere, Chief Marealle, Kenneth 
Kaunda, Zuberi Mtemvu, Peter Colmore, Lady Judith Listowel, Dr. Michael 
Lugazia, Dr. Wilbard Mwanjisi, Kasella Bantu, Japhet Kirilo...

Nilikesha nikisoma yale mafaili na nilikuwa kama mwendawazimu kwa mshawasha
niliokuwanao kila nyaraka ilikuwa ni kisa tosha cha kuandika sura nzima.

Vipi babu yake Sykes Mbuwane alivyotoka Mozambique kuja Tanganyika kama
mamluki wa Wajerumani chini ya Herman Von Wissman, vipi walikutana na
Julius Nyerere 1952, mambo lukuki ya kusisimua.

[​IMG]
Moja ya Nyaraka za Sykes nilizowapa Kavazi la Mwalimu Nyerere

Nyaraka hizi, na mahojiano na wazee wangu niliowahoji kwingi na yale niiyoyajua kwa
kuzaliwa Dar es Salaam, Gerezani ndiyo yaliyoniwezesha kuandika historia hii ya TANU.

Kitu kimoja hakikunipitikia nilipokuwa naandika kitabu kile.
Sikutegemea kama kalamu yangu itachoma nyoyo za wengi.

[​IMG]

Alfa,
Nina mengi ambayo ningeweza kuhadithia lakini haya yanatosha kwa sasa.


Reply1 hr
Manage
Mohamed Said Hapo chini Ally Sykes na Julius Nyerere nyumbani kwa Nyerere Magomeni, 1958:

Reply1 hr
Manage
Mohamed Said Moja ya Nyaraka za Sykes nilizowapa Kavazi la Mwalimu Nyerere:

Reply1 hr
Manage
Mohamed Said Asaria tuendelee na Dr. Mwanjisi kama nilivyomsoma katika Nyaraka za Sykes...:

Reply25 mins
Manage
Mohamed Said Ralph...
Kwangu mimi Chief Kidaha ni baba ya rafiki yangu wa utotoni Edward Makwaia 
ambae tulisoma darasa moja St. Joseph's Convent na ilikuwa kupitia Edward ambae tukipenda kumwita Ted ndipo nilipata bahati ya kukutana na mzee wetu huyu.

Huu ulikuwa mwaka wa 1967 au 1968.
Wakati huo akiishi Nairobi.

Ted ndiye Chief wa Siha hivi sasa baada ya kifo cha baba yake.

Katika utafiti wangu wa kuandika maisha ya Abdu Sykes nilikutana na Chief Kidaha
katika Nyaraka za Sykes kupitia barua aliyoandika Dr. Wilbard Mwanjisi mwaka wa
1950 akimsifia Chief Kidawa kuwa ni mwanasiasi makini kwa michango yake ndani ya
Legco.


Reply25 mins
Manage
Mohamed Said Tuendelee na Dr. Mwanjisi:

Reply19 mins
Manage
Mohamed Said ''It pricks the heart like a cruel dagger.''
Historia hii inachoma nyoyo...

''Barua hii ya Mzee Kawawa kwa Ally Sykes ilikuwa ikimfahamisha Ally Sykes hali ya siasa Kanda ya Ziwa.

Hii barua hadi leo ipo katika nyaraka za akina Sykes.

Nilipokaa na Ally Sykes kutaka maelezo ya barua ile aliyoandikiwa na Kawawa, Ally Sykes alinipa kisa hiki:

''Mwaka 1951 nilichaguliwa kuwa katibu mkuu wa Tanganyika African Government Servants Association (TAGSA).

Chama hiki kiliundwa mwaka wa 1927 kwa lengo la kuendeleza maelewano mazuri baina ya Serikali ya Malkia na sisi watumishi Waafrika.

Rashid Kawawa alikuwa mwana kamati.
Mimi nilichaguliwa pamoja na Thomas Marealle kama rais wa TAGSA.

Katiba ya TAGSA iliamuru uchaguzi wa kila mwaka, na mimi nilirudishwa madarakani kama katibu mara nne hadi Oktoba, 1954 nilipojiuzulu baada ya kuhamishwa kwenda Korogwe kama adhabu kwa kuwa miongoni mwa wale wanachama 17 waliounda TANU.

Watu kadhaa walishika urais.

Stephen Mhando na Dr. Wilbard Mwanjisi wote hao waliwahi kuchaguliwa kuwa marais wa TAGSA.

Miongoni mwa wanachama watendaji wa TAGSA walikuwa Dr. Michael Lugazia na Rashid Kawawa ambao alichaguliwa kuwa katibu baada ya mimi kujiuzulu.

Kupitia TAGSA, Kawawa alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Tanganyika Federation of Labour (TFL).''


Reply18 mins
Manage
Mohamed Said Tunaendelea na Dr. Mwanjisi:

Reply13 mins
Manage
Mohamed Said Kashata,
Historia hii si ya akina Sykes peke yao.

Unajua katika historia ya uhuru na historia ya asili ya vyama vya siasa
Tanganyika huwezi ukaitafiti na kuandika kwa uhakika bila kuitaja AA.

Huwezi kuitaja African Association bila kumtaja Kleist Sykes.

Huwezi kumataja Kleist bila kuwataja watoto wake kwa kuwa wote
walishiriki katika uongozi wa African Association na kisha kuasisi TANU.

Lakini pia ukiwaleta hawa wanae itakubidi uwalete vijana wenzao wa
wakati wao waliokuwa katika siasa kama Hamza Mwapachu, Dr. 
Kyaruzi,Tewa Said Tewa, Zuberi Mtemvu, Dr. Michael Lugazia, 
Dossa Azizi, Dr. Wilbard Mwanjisi, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dustan
Omari, Dr. Luciano Tsere, Kasella Bantu kutaja majina machache.

Lakini tena na hili lina nafasi ya peke yake hutoweza kuwafikia wazee
kama Jumbe Tambaza, Mwinjuma Mwinyikambi, Mshume Kiyate, 
Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Bi. Tatu
biti Mzee, Bi. Titi Mohamed na wengineo bila kupita kwa Abdul Sykes.

Haya yote ni kwa kuwa kwa wakati ule Tanganyika inaamka katika siasa
za utaifa hawa ndiyo walikuwa katika uongozi wa TAA na walikuwa watu
maarufu katika mji wa Dar es Salaam.

Dar es Salaam ya wakati ule Uislam ulikuwa na nguvu sana mgeni yoyote
asingeweza kufanya lolote bila ya kuungwa mkono na watu hawa.

Ukweli ni kuwa bila Abdul, Nyerere asingepokelewa.
Nitakupa mifano miwili.

[​IMG]
Erika Fiah

Mwaka wa 1933 Kleist aligombana na Erika Fiah katika uongozi wa AA
na Kleist akajiuzulu uongozi na Fiah akachukua nafasi ya Kleist ya katibu.

Rais alikuwa Mzee bin Sudi.

African Association haikuweza kufanya kazi kwa ufanisi na Mzee bin Sudi
ilibidi amwandikia Kleist barua kumsihi arudi katika uongozi.

Barua hii ya mwaka wa 1933 mimi nimeisoma na Mzee bin Sudi ameandika
kwa kuanza na ''Bismillah Rahman Rahim.''

Kleist alirudi katika uongozi.

Mwaka wa 1953 Nyerere alipochukua uongozi wa TAA kutoka kwa Abdul 
Sykes chama kilikufa ikabidi juhudi zifanyike kukiweka chama katika hali
madhubuti hadi kufikia kuunda TANU.

Kwa kuhitimisha.

Chuo Cha Kivukoni kilipoandika historia ya TANU haya waliyajua na ndiyo
maana kitabu kizima Abdul Sykes alikwepwa kutajwa na historia ikaanza na
Nyerere kwani walitambua wakimtaja Abdul na kueleza historia yake itabidi
wamtaje na baba yake na wengine wote kama nilivyoeleza.

Hili hawakulitaka.


Reply13 mins
Manage
Mohamed Said Ngongo,
Hilo ulosema kuhusu mchango wa Mwalimu Nyerere katika historia ya 
Tanzania si mie wala yeyote yule anaweza kukupinga.

Hakika ni Mwalimu Nyerere aliyeongoza harakati za uhuru wa Tanganyika.
Lakini peke yake asingeweza.

Unasema sina jipya.

Hapana si kweli kwenye kipindi cha leo nilimleta Chief Kidaha Makwaia, 
Dr. Wilbard Mwanjisi, Paul Bomani, Sheikh Yusuf Badi, Yusuf Olotu, Ali
Mwinyi Tambwe, Ali Jumbe Kiro, Mwalimu Sakina Arab na wengineo na
nikaeleza michango yao katika kupigania uhuru wa Tanganyika. 

Mimi si mtu wa porojo.

Ushahidi kuwa mimi si mtu wa porojo ni kuwa miaka michache tu ilopita
nilishirikishwa katika kuandika Dictionary of African Biography (DAB) mradi
wa Harvard University na Oxford University Press, New York.

Kazi imekamilika na hilo kamusi lipo sokoni.
Hii si porojo.

Ngongo,
Angalia hii picha hapo chini:

[​IMG]

Wa pili kushoto na mwanamke pekee ni Mwalimu Sakina Arab. Mwalimu Nyerere huyo katikati
ruka mtu mmoja huyo anaefuatia ni Ali Jumbe Kiro kiongozi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika,
Oscar Kambona na Ali Mwinyi Tambwe. Tambwe alikuwa katibu wa Al Jamiatul Islamiyya na mmoja
wa wanachama wa mwanzo wa TANU.


Reply10 mins
Manage
Mohamed Said Tunaendelea na Dr. Mwanjisi:

Reply6 mins
Manage
Mohamed Said Ila leo katika mengi nimekuja na somo jipya,''Dhana ya Uongozi wa Harakati
za Uhuru.''

Hili lilikuwa moja katika niliyozungumza leo.

Hapa nilipitia michango ya Chief Kidaha Makwaia, Hamza Mwapachu, Abdul
Sykes na Paul Bomani katika juhudi ya kupambana na ukoloni kabla TANU
haijaasisiwa 1954.

Nilifanya rejea za wenyewe kwa wenyewe wanasiasa Waafrika walivyokuwa 
wakionana katika siasa za Tanganyika mwaka 1950 wakati wakiwa TAA na sasa
wanata kuunda chama cha siasa kudai uhuru.

Nilimweleza Chief Kidaha kutoka kalamu ya Dr. Wilbard Mwanjisi jinsi yeye
alivyomuona kuwa ni kiongozi anaefaa kuongoza harakati.

Hapa nilikuwa nasoma kutoka barua iliyokuwa katika Nyaraka za Sykes ambayo
aliiandika Dr. Mwanjisi akikusudia ichapwe kwenye jarida la Tanganyika Government 
Servant Association (TAGSA).

Kisha nikamweleza Hamza Mwapachu kama nilivyomtafiti na nikafanya rejea ya 
barua yake akieleza mchango wa Paul Bomani na jinsi alivyomuona kuwa ni
kiongozi atakawafaa Waafrika wa Tanganyika na chama cha TAA.

Nikahitimisha na Abdul Sykes.

Ngongo,
Ikiwa historia hii inachoma moyo wako huna haja ya kujitesa bure.
Kila ukiona bandiko langu likwepe usilisome.

Utasalimika.


Reply6 mins
Manage
Mohamed Said Asaria kwa sasa tuhitimishe kwa hiyo hapo chini:

Reply1 min
Manage
Mohamed Said Kandukamo1,
Subiri itafika wakati In Sha Allah tutamgumza Dr. Mwanjisi.
Nduguye Roland Mwanjisi ameandika "paper," kuhusu kaka yake.

"Paper," hii alimpelekea mzee wangu mmoja baada ya yeye Roland kusoma
kitabu cha Abdul Sykes.

In Sha Allah iko siku nitakuwekeeni hapa.

Sasa mnaanza kunishangaza mbona ghafla watu wanataka kujua historia hii?
Ilhali hapa hapa wako walioita historia hii ni ngano za Mohamed Said?

Nini kimezidi?


ReplyJust now

No comments: