''Allah ni Mjuzi Allah na ni Mbora wa kulipa.
Sheikh Ponda utayakuta malipo yako kwa Allah yakiwa makubwa kwa subra na ustahamilivu kwa ajili ya dini yake.
Hukuwa tayari kuuza uhuru wako kwa matakwa ya wenye kudhulumu.
Muda wote ulitutia moyo mawakili wako kila tulipokutana na vitimbi.
Mara nyingi sisi mawakili tulikuwa kama wateja na wewe ndiye wakili.
Hakika wewe ni kiongozi.
Umma huu wa Waislam wa Tanzania utaishi kwa mfano wako.
Alhamdulilah leo uko huru baada ya miaka miwili na miezi mitatu jela ukiwa na jeraha kubwa la risasi.
Umma huu wa Waislam wa Tanzania utaishi kwa mfano wako.
Alhamdulilah leo uko huru baada ya miaka miwili na miezi mitatu jela ukiwa na jeraha kubwa la risasi.
Allah anayo siri kubwa katika maisha yako Sheikh Ponda.
Allah akuhifadhi kiongozi wetu.
Amin.''
Wakili Juma Nassoro
Sheikh Ponda na Wakili Juma Nassoro wakiwa Mahakamani |
![]() |
Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa katika pingu Mahakamani |
Ilikuwa katika semina ya
Vijana wa Kiislam Tanzania mwaka wa 1988 ndipo kwa mara ya kwanza
nilipofahamiana na Sheikh Issa Ponda. Ninachokumbuka kwa Sheikh Ponda ni kuwa
alitusalisha sala moja na niliusikia usomaji wake mzuri wa Qur'an. Nilimpenda
kutoka siku hiyo. Semina hii ilikuja baada ya mambo mengi dhidi ya Uislam
kutokea nchini. Kulikuwa na sakata la Sophia Kawawa kutaka Qur'an ibadilishwe.
Hii ilitokea mwezi Mei 1988. Baada ya kauli hiyo palifanyika maandamano makubwa
Zanzibar kumpinga Sophia Kawawa na Waislam walishambuliwa, baadhi wakauliwa na
wengine wakapata ulemavu wa maisha. Sheikh Said Gwiji mshtakiwa namba moja na
wenzake walishitakiwa na wakafungwa jela miezi 18. Kosa lao likiwa ni kuihami
Qur'an ya Allah isichezewe. Kulikuwa na vita vikipigwa dhidi ya vazi la hijab
na kesi maarufu ilikuwa ya Fikira Omari mfanyakazi wa Kiltex. Kulikuwa na kesi
ya Kurwa Shauri aliyeshitakiwa kwa ''uchochezi'' na mambo mengine. Katika
hayo kulikuwa na tatizo la Mchungaji Christopher Mtikila aliyekuwa akimbughudhi
Rais Mwinyi na kuwashambulia Waislam hasa wenye asili ya Kiasia na Kiarabu.
Kulikuwa na pia na ''Christian Lobby,'' mtandao wa siri katika vyombo vya
habari vilivyokuwa vikiwapiga vita Waislam waliokuwa katika serikali ya Rais
Mwinyi achilia mbali kuupiga vita Uislam wenyewe wakitumia nafasi zao katika
vyombo hivyo.
Historia ya Waislam wa Tanzania itakapokuja kuandikwa jina la Sheikh Ponda Issa Ponda litaunganishwa na jina la Mufti Sheikh Hassan bin Amir kwa kitu kimoja nacho ni ardhi ya Chang'ombe Dar es Salaam ambako Waislam chini ya uongozi wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) walikusudia kujenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968. Katika uwanja huu ndipo Rais wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere akishuhudiwa na Tewa Said Tewa na Mufti Sheikh Hassan bin Amir aliweka jiwe la msingi la chuo hicho. Chuo hakikujengwa na EAMWS ikapigwa marufuku na serikali. Mambo hayakuishia hapo. Sheikh Hassan bin Amir akakamatwa na kufukuzwa nchini akarudishwa ''kwao'' Zanzibar. Serikali ikaunda BAKWATA na Chuo Kikuu cha Waislam hakikujengwa. Nini kilisababisha nakma hii? Waliokuwa karibu na Sheikh Hassan bin Amir wanasema katika siku zake za mwisho kila alipotajiwa ule mradi wa chuo kikuu alikuwa akilia na kusema ilikuwa hamu yake kujenga chuo Kikuu kama Azhar ya Misri na akifika hapo alikuwa akibubujikwa na machozi. Wakati ule Sheikh Hassan bin alikuwa na miaka zaidi ya 90 na aliishi na simanzi hizi hadi alipokufa mwaka 1979. Huu uwanja wa Waislam ndiyo Sheikh Ponda alipouchukua kuurudisha mikononi kwa Waislam ndipo alipokusudia kujenga msikiti na kuupa jina la Sheikh Hassan bin Amir.

Kulia Sheikh Ponda Issa Ponda, Wakili Juma Nasoro na Rajab Katimba
Mahakama Kuu baada ya ushindi wa kesi ya rufaa
![]() |
Sheikh Ponda akifunguliwa pingu na Askari Magereza Mahakamani |
Historia ya uhuru wa Tanganyika ina mashujaa wengi katika
siasa ambao walikuwa
masheikh tena wa sifa na kutajika.
Hawa walikuwa mstari wa mbele katika kupambana na dhulma za wakoloni na ndiyo
walikuwa bega kwa bega na Baba wa Taifa.
masheikh tena wa sifa na kutajika.
Hawa walikuwa mstari wa mbele katika kupambana na dhulma za wakoloni na ndiyo
walikuwa bega kwa bega na Baba wa Taifa.
Kulikuwa na Sheikh Hassan bin Amir na Sheikh Said Chaurembo katika
TAA - Political Subcommittee.
![]() |
Kushoto: Sheikh Hassan bin Amir, Julius Nyerere, Sheikh Abdallah Chaurembo, Rashid Kawawa na Tewa Said Tewa |
Hii ilikuwa 1950.
Kulikuwa na Sheikh Mohamed Ramiyya wa Bagamoyo katika TAA na TANU.
Kulikuwa na Sheikh Mohamed Ramiyya wa Bagamoyo katika TAA na TANU.
Kushoto: Idd Faiz Mfungo, Sheikh Mohamed Ramiyya, Julius Nyerere, Saadani Abdu Kandoro,Haruna Taratibu Dodoma 1956 |
Kulikuwa na Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa
TANU.
Kulikuwa na Sheikh Yusuf Badi wa Lindi katika TANU.
Kulikuwa na Sheikh Rashid Sembe shujaa wa Kura Tatu katika mkutano wa
TANU kujadili Uchaguzi Mkuu wa mwaka wa 1958.
TANU.
Kulia: Bi. Titi Mohamed, Clement Mohamed Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Waliosimama nyuma kulia ni John Rupia, Rajab Diwani na Mama Maria Nyerere |
Kulikuwa na Sheikh Rashid Sembe shujaa wa Kura Tatu katika mkutano wa
TANU kujadili Uchaguzi Mkuu wa mwaka wa 1958.
![]() |
Sheikh Abdallah Rashid Sembe |
Tanganyika itakudhihirikia kuwa masheikh siku zote wamekuwa mstari wa mbele
katika kupambana na dhulma ya aina yoyote katika jamii.
![]() |
Ulinzi Mahakamani Morogoro katika kesi ya Sheikh Ponda |
Askari wakilinda usalama wakati Waislam wa Morogoro wakitoka mahakamani |
Waislam akina mama Morogoro wakitoka katika kesi ya Sheikh Ponda |
Waislam wa Morogoro wakitoka kusikiliza kesi ya Sheikh Ponda Mahakama ya Morogoro |
![]() |
Sheikh Ponda na Mzee Bilal Rehani Waikela nyumbani kwa Mzee Waikela Tabora |
Kushoto: Mzee Bilal Rehani Waikela na Mwandishi Mahakamani Morogoro |
Sheikh Ponda katikati ya mawakili wake Mahakamani Morogoro |
Sheikh Ponda Akipelekwa Mahabusi Mwanzo wa Kesi Dar es Salaam |
No comments:
Post a Comment