Friday 8 December 2017

UHURU DAY: TUWAKUMBUKE MASHUJAA WA UHURU WA TANGANYIKA


Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
(1922 - 1999)

MASHUJAA WALIONYANYUA SILAHA

Bushiri Bin Harith

Sultani Abdulrauf Songea Mbano
Shujaa wa Maji Maji
Selemani Mamba
Shujaa wa Maji Maji




MISINGI YA UTAIFA ILIYOWEKWA NA AFRICAN ASSOCIATION 
1929 - 1954

Kushoto aliyesimama ni Ally Kleist Sykes, na kulia kwake ni
Abdulwahid Kleist Sykes, mbele kushoto ni Kleist Sykes 
Mbuwane na Abbas Kleist Sykes. Katika hawa aliye hai ni Abbas
Ukoo huu umeacha kumbukumbu nyingi kwa maandishi katika harakati za
kuunda African Association 1929 na kuunda TANU 1954. Picha hii imepigwa
mwaka wa 1942 Abdul aliporudi Dar es Salaam kutoka Lower Kabete Kenya
alipokuwa akipata mafunzo ya kijeshi katika King's African Rifles kabla
hajakwenda Burma kujiunga na Burma Infantry. Angalia utaona Abdul amevaa 
sare ya Jeshi la Mfalme wa Uingereza. Ilikuwa akiwa Burma Vita Vya Pili Vya Dunia
(1938 - 1945) ndipo alipoamua kuwa 6th Battalion iliyokuwa na askari kutoka 
Tanganyika waunde TANU wakirudi Tanganyika kudai uhuru.


WAZALENDO WAPIGANIA UHURU KATIKA TANU
1954 - 1961

Waasisi wa TANU 7 Julai 1954

Baraza la Wazee wa TANU

Photo: Resignation Letter JKN
Barua ya kujiuzulu kazi ya Mwalimu Julius Nyerere, 1955

Hamza Kibwana Mwapachu
(1913 - 1962)
Abdul Sykes
(1924 - 1968)

Kushoto: Dossa Aziz, Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes na Lawi Sijaona
katika dhifa ya kumuaga Nyerere safari ya pili UNO 1957

Kushoto: Bi. Chiku bint Said Kisusa, wa tatu Julius Kambaraga Nyerere wa tano Bi. Titi Mohamed na Bi. Tatu bint Mzee wanamsindikiza Mwalimu Nyerere Uwanja wa Ndege safari ya UNO 1955

Kulia: Bi. Titi Mohamed, Clement Mohamed Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir, Julius Nyerere
Nyuma kulia: John Rupia, Rajab Diwani na Mama Maria Nyerere

UPINZANI WA SHEIKH HUSSEIN JUMA (UTP) 1956 
NA
 ZUBERI MTEMVU (ANC) 1958

Sheikh Hussein Juma
Vice President United Tanganyika Party (UTP)

Zuberi Mtemvu
President African National Congress (ANC)



MIKUTANO YA TANU MNAZI MMOJA NA JANGWANI 1954/55



Mwalimu Julius Nyerere na Bi. Titi Mohamed katika mkutano wa hadhara Viwanja Vya Jangwani

Idd Faiz Mafungo (Mweka Hazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya) Mratibu wa safari ya Baba wa Taifa UNO 1955,
Sheikh Mohamed Ramiyya wa Bagamoyo, Julius Kambarage Nyerere, Abdu Kandoro na Haruna Taratibu Dodoma 1956

BANTU GROUP WAHAMASISHAJI NA WALINZI WA VIONGOZI 1955


Kulia: Zuberi Mtemvu, Julius Nyerere na John Rupia waki wa na Bantu Group


Robert Makange mwandishi wa gazeti la Mwafrika

KUMBUKUMBU YA MIAKA 20 YA TANU 1974


KUMBUKUMBU YA MIAKA 50 YA UHURU 2011

Ofisi Ndogo ya CCM Sherehe ya Miaka 50 ya Uhuru 9 December, 2011

Jengo Jipya la CCM Lumumba Avenue Dar es Salaam

UHURU 1961

Mwalimu Nyerere na Bi. Titi Mohamed

Kulia: Sheikh Issa Nasir, Oscar Kambona, Bi. Mugaya Nyang'ombe kulia kwa Mwalimu Nyerere Rajab Diwani
Karimjee Hall



Baraza la Kwanza la Mawaziri 1961
PICHA MCHANGANYIKO



Dome Okochi Budohi


No comments: