Sultani Abdulrauf Songea Mbano
Kibao kimeandika jina lake kama ''Lwafu'' Nduna Mbano
Kaburi la Sultani Abdulrauf Songea Mbano |
Kwa
miaka mingi sana na hadi leo jina la Sultani wa Wangoni Abdulrauf Songea Mbano Jemedari wa Wangoni katika Vita ya Majimaji, jina lake la ‘’Abdulrauf’’ moja ya sifa za Allah ikiwa na maana ‘’Mwenye
Huruma,’’ lilikuwa halifahamiki kwa wengi na wanahistoria kwa sababu zao
hawakutaka kulisema lijulikane kama vile wengi hawajui kuwa Sultani Mkwawa jina
lake ni ''Abdallah.''
Tukija katika historia ya miaka ya karibuni zaidi si wengi wenye kujua kuwa Kleist Sykes jina lake ni Abdallah, au Schneider Plantan jina lake ni ''Abdillah.''
Tunaweza tukasema kuwa haya yote ni matatizo ya ukoloni.
Lakini swali linakuja iweje hata baada ya ukoloni kutoweka ikabakia historia
yetu hatuiweki sawa?
Leo gazeti la ''Habari Leo,'' (28 Februari, 2018) ukurasa wa mbele imetoka picha ya kaburi la Sultani Abdulrauf Songea Mbano jina linalosomeka katika kaburi hilo ambalo ni la Kiislam ni ‘’Songea Mbano,’’ na jina lake halisi ''Abdulrauf,'' halipo.
Laiti kama Sultani Abdulrauf asingezikwa katika kaburi la Kiislam mengi katika historia ya Majimaji yasingelipata ushahidi madhubuti ukizingatia kuwa katika wale majemedari walionyongwa na Wajerumani, majina yao ya Kiislam yalifutwa yakawekwa mengine.
Atakae kusoma zaidi kuhusu historia hii aingie hapo chini:
Tukija katika historia ya miaka ya karibuni zaidi si wengi wenye kujua kuwa Kleist Sykes jina lake ni Abdallah, au Schneider Plantan jina lake ni ''Abdillah.''
Kaburi la Kleist Sykes |
Leo gazeti la ''Habari Leo,'' (28 Februari, 2018) ukurasa wa mbele imetoka picha ya kaburi la Sultani Abdulrauf Songea Mbano jina linalosomeka katika kaburi hilo ambalo ni la Kiislam ni ‘’Songea Mbano,’’ na jina lake halisi ''Abdulrauf,'' halipo.
Laiti kama Sultani Abdulrauf asingezikwa katika kaburi la Kiislam mengi katika historia ya Majimaji yasingelipata ushahidi madhubuti ukizingatia kuwa katika wale majemedari walionyongwa na Wajerumani, majina yao ya Kiislam yalifutwa yakawekwa mengine.
Atakae kusoma zaidi kuhusu historia hii aingie hapo chini:
- http://www.mohammedsaid.com/2016/06/chief-abdul-rauf-bin-songea-mmoja-wa.html
- http://www.mohammedsaid.com/2015/03/kutoka-jf-majemadari-wa-vita-vya-maji.html
- http://www.mohammedsaid.com/2015/03/kutoka-jf-uchakachuaji-wa-majina-ya.html
- http://www.mohammedsaid.com/2015/02/marehemu-sheikh-ilunga-hassan-kapungu.html
No comments:
Post a Comment