Khoja FC |
Khoja Football Club ni timu ya soka ya watoto wa
madras wanaoishi Mtaa wa Khoja Magomeni Mapipa na wanasoma katika vyuo tofauti
vinavyozunguka Masjid Nur.
Umti wao wastani haujazidi miaka 13 na wote ni
wanafunzi wa shule za msingi.
Picha
hii nimewapiga vijana wangu wa Khoja Streert FC mchana huu walikuwa wanafanya
mazoezi mtaani na mpira wao wa makaratasi. Huwaambia kuwa mimi katika umri wao
nikicheza mpira wenyewe ''gozi,'' tukijaza upepo kwa AK Nanji Tandamti na
Sikukukuu.
Sasa kweli kwa matayarisho haya nchi hii itapanda chati katika soka?
Lakini hawa vijana usiwaone hivi.
Wako hapo waliokunywa juzuu moja hadi nne...
No comments:
Post a Comment