Utangulizi
Sheikh
Abdillahi Nasir ni Sheikh msomi wa sifa katika Afrika ya Mashariki na je ya
mipaka hii. Sheikh Abdillahi Nasir ni mwanafunzi wa Sheikh Said Omar Abdallah
maarufu Mwinyi Baraka. Sheikh Abdillahi anasema kubwa alilopata kwa Mwinyi
Baraka kama mwalimu wake ni kule kumsikia mwalimu wake akiunganisha Qur’an na ukweli
ulioko ndani ya sayansi, elimu ambayo kwa wakati ule haikuwa maarufu sana. Sheikh Abdillah anaeleza pia vipi mwalimu wake
Sheikh Ghazal alivyomsaidia katika mabadilko yake katika kuendea masuala
makubwa ya madhehebu na kufanikiwa. Katika mazungumzo haya Sheikh Abdillah
anaeleza kwa ufupi maisha yake kama mwanasiasa na vipi siasa imemsaidia kuwa
kiongozi anaekubalika katika jamii kitu
ambacho pia kimesaidia katika kusomesha Uislam.
Sheikh Said Omar Abdallah (Mwinyibaraka) |
No comments:
Post a Comment