Abdu Nondo |
Kijana huyu Abdul Mahmoud Omar
Athuman Kagobe, (Abdu Nondo) ni mjukuu wa Omar Athuman
Kagobe, ambaye ni veteran wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1914 – 1918), na baadae
alijiunga na Jeshi la Polisi na kuacha kazi baada ya uhuru, mwaka 1961.
Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe
ndiye aliyeileta TANU Ujiji na nyumbani kwa Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe ndio
pia alipofikia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Bibi Titi na
Sheikh Suleiman Taqadir mara mbili kwenye harakati za kupigania uhuru na mahali
hapo ndio TANU imejenga Mnara wa Kumbukumbu.
Kwenye nyumba hiyo ndio pia
alipofikia Sheikh Abdallah Saleh Al Farsy mara mbili na Sheikh Hassan bin Ameir.
Dada yake Mzee Omar Athuman
Kagobe ni Zubeda Athuman Kagobe na ndio aliyemzaa Dr. Sherry Taki, msomi wa sayansi
ya siasa kutoka Chuo Kikuu cha Lumumba, Moscow wakati wa Urusi ya Kikomunisti.
Mwanae mwingine ni Mamdu Taki, msomi
wa Tabora School na Makerere alikoma pamoja na akina Timothy Apiyo, na akafanya
kazi Mamlaka ya Tumbaku kwa zaidi ya mianka 20.
Binti yake Nargis Taki aliolewa
na Mpigania uhuru wa Tanganyika Bwana Rashid Kheir Baghdellah, ambaye ametajwa sana
kwenye Kitabu cha Mohmed Said, mwandishi wa kitabu cha ‘’Maisha
na Nyakati ya Abdul Wahid Sykes…’’ Bibi
yake mzaa baba ni Kulthoum Hemed Kiumbe, dada wa Sheikh Khalfan Mohamed Kiumbe,
na Mahmoud Mohamed Kiumbe ambaye alikuwa mwanachama shupavu wa TANU na kabla ya
uhuru Mtaa Maalum ulipewa jina lake huko Ujiji mpaka leo, unaitwa Mwalim Kiumbe
Street.
Babu yake Mzaa mama ni Alhaj Juma Rehani, msomi
kwenye Tarika ya Mwinyi Mkumbati, Twarika ya zamani sana Ujiji iliyoasisiwa na
Mwinyi Kheir Bin Mwinyi Mkuu Al Ghashan, mkubwa wa zamani wa Ujiji akiwakilisha
Dola ya Zanzibar, ikisimamiwa na Sheikh Hamisi Bin Sali, na ikarithiwa na Salim
Bin Mwinyi Kheir, ndiyo ikaja kusimamiwa na Mwinyi Mkumbati.
Akina Sheikh Kiumbe walikunywa ijjaza
kwa Sheikh Khalfan Al Bulush mrithi wa tarika hiyo ambayo ilikuja kurithiwa na
Sheikh Kiumbe na Sheikh Omar Kakolwa na kupata nguvu alipokuja Sheikh Mohamed
Nassor kutoka Zanzibar, babu yake Abdu Nondo na aliendelea kuwa Khalifa wa
Sheikh Mohamed Nassor kwenye Tarika Qadiria hadi umauti.
Kadhia ya Abdu Nondo
inatukumbusha zamani tu baada ya Tanganyika kupata uhuru, mwaka 1968 Mwalim
Kambarage Nyerere alimtuma Aliyekuwa Waziri Wa Mambo ya Ndani Saidi Maswanya,
kuwataka watu wa Kigoma wathibitishe Uraia wao, wakiwemo wanafunzi waliotoka
Mkoa Wa Kigoma popote walipo walirejeshwa makwao kwa ajili ya zoezi hilo,
Kwenye mkutano Bwana Said
Maswanya, aliambiwa na wazee wa Ujiji wakiongozwa na Alhaj Yussuf Tossir na
Mzee Rashid Kazema, akamwite aliyemtuma na mkutano ukavunjika, na hii ndio lilipelekea
Mhesimiwa Manju Msambya na marehemu Aman Walid Kabourou kufanyiwa fitna na
kufukuzwa shule Kigoma Secondary Nyakati hizo.
Ombwe hili ambalo la kibaguzi lingalipo linawaandama wenyeji
wa Kigoma mpaka sasa.
No comments:
Post a Comment