Kulia ni Maalim Sakina Arab |
Hapo chini ni mazungumzo
katika whatsapp baada ya Sheikh Aziz kuweka picha ya Maalim Sakina Arab:
17 years mpendwa wetu Maalim Sakina Mohammed Arab mungu amrehemu
Sheikh Azizi naona
umeweka picha ya Mwalimu wetu!
Aziz Ahsante
kwa kumbukumbu hii. Huyo mwingine ni nani?
Mjukuu wake
upande wa Maalim Fatna mdogo wake Maalim Sakina
Sheikh Aziz
Salim unawakumbusha mbali wanafunzi wake, Maalim Sakina Mohamed al Arab,
Mwenyezi Mungu amrehemu kwa hidaya yake ya Elimu alioiacha duniani kwa
wanafunzi alio wasomesha.
Aamin.
Nami nikaandika hayo hapo chini kuhusu Malim Sakina kwa faida y:a wale
ambao hawakupata kumjua:
‘’Maalim Sakina kafanya makubwa katika kupigania uhuru wa
Tanganyika na ni katika akina mama wa mwanzo kabisa kumpokea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na mkewe Mama
Maria yeye na nduguye Mwalimu Fatna na mama yao Bi Chiku Kikusa mke wa Shariff
Abdallah Attas. Aliyewafikisha kwa watu hawa alikuwa marehemu Abdulwahid Sykes.
Mama Maria 1955 akafungua
biashara ya kuuza mafuta ya taa pale Mtaa wa Mchikichi alipokuwa akiishi Maalim
Fatna.
Shariff Abdallah Attas |
Iko siku nitakuwekeeni kisa
hiki kwa kirefu.
Hawa walisoma wote Al
Jamiatul Islamiyya Muslim School pamoja na baba yangu. Baba akijuana vizuri na
Mustafa Al Arab kaka yake Maalimu Sakina.
Allah awaweke pema peponi
wazee wetu hawa.
Niko ndani ya ndege nakwenda
South Africa nikaingia katika mazungumzo na Mzungu mmoja mwenyeji wa Johannesburg
nikamtaja Bailey na nikamweleza kuwa ni rafiki yangu.
Yule Mzungu akanambia
Bailey ni jirani yake na amefariki mwezi uliopita.
Picha hiyo hapo juu na zingine za miaka ya nyuma zilikuwa hazionekani
popote katika historia ya TANU.
Kulia Bi Titi Mohamed, Clement Mohamed Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir na Julius Nyerere. Nyuma kulia John Rupia, Rajab Duwani na Mama Maria Nyerere katika mkutano wa TANU Mnazi Mmoja 1954/1955. |
Hizi picha alinipa Jim Bailey ambae
nilijulishwa kwake na Ally Sykes. Huyu ni Kaburu kutoka Afrika Kusini na ndiye
alikuwa akimiliki gazeti la DRUM.
Jim Bailey alinipa kazi ya kuhariri kitabu
cha Baba wa Taifa na kutafuta publisher. Kazi hii nilifanya Alhamdulillah na
kitabu kikachapwa kinaitwa "Nyerere of Tanzania."
Jim Bailey ndipo katika haya akanipa
mapicha haya kutoka Jim Bailey African Collection Johannesburg.
Bailey akanipa na picha ya
Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU akiwa jukwaani na
Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.''
Mahojiano na Bi. Maunda
Plantan mjukuu wa Afande Plantan Kamanda wa German Constabulary Dar es
Salaam 1890s nyumbani kwake Magomeni Mikumi. Afande Plantan alikuja
Tanganyika na jeshi la Wazulu chini Mjerumani Herman von Wissman kuja kupambana
na Abushiri bin Salim Al Harith na Chief Mkwawa. Katika jeshi hilo la Wazulu
alikuwamo Sykes Mbuwane.''
No comments:
Post a Comment