Mwandishi amesimama Lincoln Memorial aliposimama Dr. Martin Luther King alipotoa hotuba yake, ''I Have a Dream.'' |
Siku
kama ya leo Martin Luther King aliuliwa Memphis kwa kupigwa risasi na hii leo imetimia miaka 50 toka Martin Luther King auliwe mwaka wa 1968.
Martin Luther
King alikuwa mpigania haki za watu weusi Marekani.
Kumbukumbu
hizi zinanirudisha mimi miaka 50 nyuma nikiwa kijana mdogo nina umri wa miaka 18
na mwanafunzi wa St. Joseph’s Convent, Dar es Salaam.
Shule
yetu ilikuwa katikati ya mji karibu na Bahari ya Hindi, Bridge Street.
Kutoka
shule ilipokuwapo na nyumbani kwetu Libya Street ilikuwa inanichukua kama
dakika 20 au zaidi kidogo kufika shule.
Nyumba yetu ilikuwa no. 10 na kwa ajili hii tukaipa jina No. 10 Dawning Street, makazi ya Waziri Mkuu wa Uingereza.
Nyumba yetu ilikuwa no. 10 na kwa ajili hii tukaipa jina No. 10 Dawning Street, makazi ya Waziri Mkuu wa Uingereza.
MIaka
ile ya 1960 Wamarekani walikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa sisi vijana na safari
ya Mwalimu Nyerere Amerika mwaka wa 1963 wakati wa John Kennedy akiwa rais wa
Marekani ilizidisha pia uhusiano mwema
katika ya Marekani na Tanganyika.
Miaka hii
ya 1960 Waingereza wakiita, ‘’Roaring 60s’’ kwetu vijana katika ‘’teens.’’ hasa
wa Dar es Salaam hakika ilikuwa miaka ya wazimu khasa na tukiiga kila kitu cha
Kimarekani, kuanzia mavazi hadi muziki wake.
Hizi
zilikuwa enzi za ‘’Soul Music’’ na Apollo Theatre, Harlem, New York na Broadway tukizijua kwa kuzisoma na kuangalia picha.
Kuwa iko siku Allah atanifkisha huko kote ilikuwa ndoto ya mbali sana.
''Soul,'' ulikuwa muziki maalum na makhsusi kwa watu weusi wa Marekani na nje yake.
Kuwa iko siku Allah atanifkisha huko kote ilikuwa ndoto ya mbali sana.
''Soul,'' ulikuwa muziki maalum na makhsusi kwa watu weusi wa Marekani na nje yake.
Apollo Theatre, Harlem, New York |
Lakini
ilikuwa pia enzi za miziki ya jazz ya wapigaji kama Duke Ellington na waimbaji bingwa
kama Nat King Cole, Frank Sinatra, Louis Armstrong,muziki uliokuwa ukipendwa na watu ''sophisticated,'' wenye umri wa kati, na hapa sitaki kuwagusa wanamuziki kutoka Uingereza kama The Beatles, Eric Burdon and The Animals, Erick Clapton kwa kuwataja wachache.
Magazeti
tuliyokuwa tukipenda kusoma yalikuwa Newsweek, Time na Ebony gazeti la watu weusi
Marekani.
Wengi
wetu nami nikiwa katika kundi hilo tulikuwa na ndoto kuwa iko siku tutakwenda
Marekani kusoma katika moja ya vyuo vikuu vya huko na wako ambao ndoto zao
zikaja kuwa kweli na tuko pia ndoto zikabakia ndoto.
Wamarekani
walikuwa na kituo chao cha utamaduni katikati ya mji ambacho ndani mlikuwa na maktaba ya vitabu, muziki na ‘’theatre,’’
sehemu wakionyesha filamu.
Kwa kuwa
na vitu hivi Wamarekani walituteka na mimi nilinasa katika dema lile kwani
nilikuwa mwanachama wa maktaba ile na nilipofikia makamu ya kuwa naandika
katika magazeti ya Uingereza kama Africa Events na New African Mkurugenzi wa United
States Information Service (USIS) alinipa uanachama wa Library of Congress, Washington
nikiweza kuazima kitabu au jarida kutoka huko na nikaletewa Dar es Salaam.
Mwandishi akiwa Library of Congress, Washington DC |
Sasa
tuje kwa Martin Luther King na mimi.
Mwalimu
wangu wa English Language alikuwa mama mmoja wa Kingereza jina lake Mrs. Grant.
Mume
wake alikuwa anaitwa Grant na wote walikuja Tanzania katika mpango wa British
Council wa kusomesha Kiingereza.
Bwana
Grant alikuwa alikuwa akisomesha Chuo Cha Ualimu Chang’ombe.
Mrs.
Grant sijui kwa vipi lakini alikuwa mwalimu aliyenipenda labda kwa kuwa
nilikuwa na mapenzi makubwa na somo lake lililokuwa linaitwa, ‘’Reading Labaratory,’’
tukifunzwa kusoma kwa haraka, yaani kwa ‘’speed,’’ akiweka, ‘’time clock,’’
kupima unasoma maneno mangapi kwa dakika ngapi kisha kuna maswali unajibu
kuonyesha kuwa umeelewa ulichosoma.
Nilisoma mahali kuwa John Kennedy alikuwa ''fast reader,'' akisoma wastani wa maneno 300 kwa dakika, basi nami nikataka kuwa kama yeye.
Class of 1970 Nyuma ni St. Joseph's Cathedral Mwandishi waliosimma wa kwnaza kulia |
Nilisoma mahali kuwa John Kennedy alikuwa ''fast reader,'' akisoma wastani wa maneno 300 kwa dakika, basi nami nikataka kuwa kama yeye.
Kulikuwa
na mashindano ya Elocution Kiingereza na Kiswahili kwa shule zote za Dar es
Salam na shule yetu kila mwaka ikishinda katika English Elocution na kuna mwaka
tuliwahi kushinda kwa pamoja English na Swahili Elocution.
Mrs. Grant
akaniambia kuwa mwaka ule nitafute ''passage,'' yeyote niihifadhi kichwani niingie
katika mashindano ya English Elocution.
Mwaka
wa 1963 ndiyo mwaka ambao Martin Luther King alitoa hotuba yake maarufu, ‘’I Have a Dream,’’ Lincoln Memorial, Washington DC.
Lincoln Memorial Washington DC |
Nilikuwa
nimehifadhi mengi kutoka michezo ya William Shakespeare kama ‘’Julius Caesar,’’
‘’Merchant of Venice,’’ ambayo wala nisingehitaji kujifunza kwani tayari
nilikuwa nimeshahifadhi mengi kutoka vitabu hivyo na ningeweza kusoma wakati wowote hata nikiamshwa usiku wa manane.
Lakini
haya yalikuwa mashindano na nilitaka niingie katika mashindano yale na mtu mashuhuri
kama Martin Luther King siyo na Cassius katika ‘’Julius Caesar,’’ au Shylock
katika ‘’Merchant of Venice,’’
Niliamua
kumsoma Martin Luther King na hotuba yake ‘’I Have a Dream.’’
Nikitoka
nyumbani asubuhi nakwenda shule njia nzima naisoma kimya kimya hotuba hiyo na
tulikuwa wanafunzi wengi tunawania nafasi hiyo ya kuwakilisha shule na kila mtu kachukua chake
anachotaka kusoma na sote tutasoma mbele ya mwalimu wetu na mbele ya wanafunzi
wenzetu na yule aliye bora ndiye atakaewakilisha shule latika mashindano yale.
Nilishindwa
kwa hiyo sikuweza kuiwakilisha St. Joseph’s Convent katika English Elocution.
Kwa nini
nilishindwa?
Wenzangu
walikuwa wanasema Kiingereza kwa ‘’accent,’’ nzuri ya Kiingereza wengi wao wakiwa wameanza kusoma Kiingereza toka darasa la kwanza katika shule kama Salvatorian, St. Xavier na wengine kutoka hapo hapo St. Joseph's. Mimi Mswahili
wa Kariakoo niliyesoma shule ya kawaida, ‘’accent,’’ yangu haikuwa imetulia ndicho kilichonifanya nishindwe.
Lakini ile tu kukubali kupambana na wenzangu wale ilihitaji kidogo ushujaa na ubishi wa Kimanyema.
Lakini ile tu kukubali kupambana na wenzangu wale ilihitaji kidogo ushujaa na ubishi wa Kimanyema.
Miaka
mingi imepita na leo huwa wakati mwingine nacheka kimoyomoyo nikiwasikia
wanangu wanazungumza Kiingereza kwa mbwembwe nyingi na wakati mwingine
nashindwa kabisa kuziweka mahali hizo ‘’accent’’ zao au hata kuzitambua.
Lakini
kwangu mimi ile kuchagua ile hotuba, ‘’I Have a Dream,’’ hotuba ile na ujumbe
uliobebwa mle ndani uliniathiri sana.
Kila
nilipokuwa napita katika mistari ya hotuna ile nilikuwa kama vile nawaona
Wamarekani Weusi siku zile wakiitwa, ‘’Negros,’’ wanavyoteswa na Wamarekani
Weupe.
Nilikuwa
kama vile naisikia moja ya nyimbo maarufu katika ‘’Negro Spirituals,’’ nyimbo
ambayo ukiisikilizaza inakutia huzuni, ‘’Go Down Moses Let My People Go,’’
iliyopigwa na Louis Armstrong.
Ilikuwapo na nyimbo nyingeni ya Sam Cooke, '' A Change is Gonna Come,'' ikiimbwa pia kwa maombolezo na mategemeo kuwa iko siku ubaguzi utaondoka Amerika na hali za watu weusi zitakuwa bora.
Hakuna mtu katika miaka ile aliyewaza hata kwa mbali kuwa iko siku mtu mweusi atatawala Amerika.
Ilikuwapo na nyimbo nyingeni ya Sam Cooke, '' A Change is Gonna Come,'' ikiimbwa pia kwa maombolezo na mategemeo kuwa iko siku ubaguzi utaondoka Amerika na hali za watu weusi zitakuwa bora.
Hakuna mtu katika miaka ile aliyewaza hata kwa mbali kuwa iko siku mtu mweusi atatawala Amerika.
Hotuba ya Martin Luther King na muziki wa Louis Armstrong vilikuwa vikinitoa katika mji wa Dar es Salaam na kunipeleka Marekani ya karne ya 18, Deep South ambako utumwa ulikuwa umeshamiri na Wanegro wakifanyishwa kazi wakiwa watumwa katika mashamba ya pamba.
Wakati mwingine ndoto na mawazo yanayotawala akili huwa kweli ingawa si mara nyingi.
NIlisafiri kwa barabara ndani ya gari ya rafiki yangu James Brennan tukitoka Iowa City akinileta Chicago kupanda ndege kuelekea New York.
Tulipita Mississippi ambayo mto wenye jina hilo ulinikumbusha Tom Sawyer na Huckleberry Finn, ''characters,'' niliowapenda wakati nikiwa mtoto mdogo nikiwasoma katika kitabu cha Mark Twain - ''Tom Sawyer and Huckleberry Finn.''
Hawa walikuwa marafiki wawili waliokuwa watu wa mikasa mingi na kupitia watoto hawa wawili niliweza kujua maisha ya shamba Amerika ile ya Deep South yakoje.
Wakati ule wala haikunipitikia kuwa nitakuja kuisoma historia ya America nikiwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam nikisomeshwa na bingwa wa historia Prof, Fredrick Kaijage, mwalimu aliyenifunza mengi na nina deni kubwa kwake.
Wala haikunipitia kuwa nitakuja kuiona kwa macho yangu Mississippi River niliyoijua zaidi kwa mikasa ya Tom Sawyer and Huckleberry Finn.
Miaka ya 1960 haikuwa tena miaka ya watumwa kulimishwa pamba bali ilikuwa miaka ya James Meredith aliyekataliwa kuingia Chuo Kikuu Cha Mississipi na Gavana mbaguzi wa Alabama, George Wallace kwa kuwa tu alikuwa na ngozi nyeusi.
Sasa
mimi ni mtu mzima na wakati mwingine huwa nazungumza na wanangu kuhusu raha na
elimu inayopatikana ndani ya kitabu.
Huwa
nawaambia kuwa nilipokuwa mtoto nilikuwa nikifika Tanganyika Library siku hizo
iko Mtaa wa Mkwepu nilikuwa nikiinamia kitabu kusoma basi huwa naondoka kabisa
Dar es Salaam.
Ikiwa ni kitabu cha Spaniards wanaikata Bahari ya Atlantic kwenda Amerika ya Kusini katika nchi ya Aztec mimi nakuwa mmoja wa mabaharia wale nasafiri na wao ndani ya meli yao nafanya yale wanayofanya.
Katika
hali hii ya raha nikinyanyua kichwa jua limezama na nje taa zinawaka, Maghrib
imeshaingia.
Naondoka
maktaba narudi nyumbani, Libya Street mwendo mfupi tu kutoka Mkwepu Street.
Nawaambia wanangu kuwa hawatoweza kuyapata haya hadi wahame kwenye kuangalia DVDs waje kwenye kusoma kitabu.
Huwa
nahitimisha nasaha zangu siku zote kwa kuwaambia, ‘’Nothing can replace the
book.’’
Kama sik kusoma vitabu nisingeijua haya niliyokuja kuyajua.
Kama sik kusoma vitabu nisingeijua haya niliyokuja kuyajua.
MIaka
ikaenda nikafika Washington DC Lincoln Memorial nikiwa na mwenyeji wangu Dr.
Harith Ghassany mwandishi wa kitabu mashuhuri kuhusu historia ya mapinduzi Zanzibar, ''Kwheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' ambae katika kunionyesha mji akanipeleka Lincoln Memorial.
Mwaka
wa 2011 nikiwa Lincloln Memorial nilisimama pale aliposimama Martin Luther King miaka 48 iliyopita na
kutoa hotuba yake maarufu, ‘’I have a Dream,’’ akiwa kijana mbichi wa miaka 34.
Nikiwa pale fikra zangu zikirudi nyuma kwa haraka nikiwa nami nimesimama mbele ya darasa nikiwahutubia wanafunzi wenzangu, ‘’I Have a Dream,’’ Mrs. Grant mwalimu wangu wa Kiingereza akinisikiliza.
Nikiwa pale fikra zangu zikirudi nyuma kwa haraka nikiwa nami nimesimama mbele ya darasa nikiwahutubia wanafunzi wenzangu, ‘’I Have a Dream,’’ Mrs. Grant mwalimu wangu wa Kiingereza akinisikiliza.
No comments:
Post a Comment