Kuhusu uhusiano wa Kabaka na Masultani wa Zanzibar watu wengi
wameniandikia kutaka ati mimi niseme kitu. Sijaweza kwa kuwa najua Sayyid
Bargash yuko na yeye ni aula zaidi kumsemea babu yake mkuu kuliko mtu yeyote
yule.
Nataka kueleza niliyoshuhudia
Kampala nyumbani kwa mmoja wa maprince katika ukoo wa Kabaka ambao ni Waislam
walipotualika katika chakula cha usiku nami nikiwa mmoja wa wajumbe wa mkutano
uliofanyika hapo Kampala nilipata mwaliko na nilihudhuria.
Kulia Prince Badru Kakungula na Prof. Ali Mazrui |
Nitamueleza Prof. Ali Mazrui nini
alihadithia alipokaribishwa kuzungumza:
''Tukiwa katika mkutano ule tulialikwa chakula
cha jioni nyumbani kwa mmoja wa wajukuu wa Badru Kakungulu na Prof. Ali Mazrui
alipoombwa kuzungumza alieleza uhusiano wake na viongozi wa Uganda na khasa
ukoo wa Kabaka ambao ni mmoja na akina Kakungulu. Alisema kuwa akiwa mtoto
mdogo akikuwa pale Mombasa, Kabaka Mutesa alitembelea Mombasa na katika hadhira
moja Kabaka alizungumza na watu wa Mombasa. Kabaka alitoa hotuba yake kwa
Kiingereza na mkalimani wake alikuwa Ali Mazrui. Prof. Mazrui akaieleza hadhira
ile kuwa Kabaka Mutesa alikuwa akizungumza Kiingereza kwa lafidhi ya Kizungu
khasa kiasi ambacho ikiwa humuoni utadhani anaezungumza ni Muingereza mwenyewe.
Sasa katika mazungumzo na kijana mdogo Ali Mazrui Kabaka alishangazwa sana na
umahiri wa Ali Mazrui katika kusema Kiingereza. Huu ukawa ndiyo mwanzo wake wa
kufahamiana na Kabaka Mutesa na Prince Badru Kakungulu alipokuja Uganda
kusomesha Makerere.''
Prince Badru kakungulu alifanya mengi
wakati wa EAMWS katika kuusukuma mbele Uislam.
Kilichowaunganisha Wazanzibari na
akina Mazrui wa Mombasa ni Uislam na hiki kikiwauma sana baadhi ya watu
Tanganyika. Yaliyokuja kutokea sote tunayajua. Inasikitisha kuwa baadhi yetu
tunafanya haya na mambo ya kuyafanyia maskhara.
Hayo hapo juu yanadhihirisha umuhimu wa Zanzibar katika Afrika ya Mashariki. Prince Kakungulu anaombewa nafasi aje Zanzibar kusoma. Hii ilikuwa 1923. |
The Life of Prince Badru Kakungulu Wasajja na ABK Kasozi |
Kulia kwa Prof. Ali Mazrui Tamim Faraj na Kushoto Kwake ni Mwandishi |
1. Princess Amal bint Khalifa
2. Bi Khola bint Said Al-Busaidiyah
3. Yaya wa Prince Mutabi
4. Prince Sayyid Jamshid bin Abdalla bin Khalifa (Baadae akawa Sultan wa Zanzibar)
5. Sayyida Nunuu bint Ahmed Al-Busaidiyah (Mke wa Sayyid Khalifa bin Harub, Sultan wa Zanzibar)
6. Prince David Ssimbwa, mdogo wake Kabaka Mutesa II. (Prince David amefariki November 2014)
7. Prince Mutebi (he is now Kabaka Ronald Muwenda Mutebi II of Buganda)
8. ADC to the Kabaka Mutesa II
9. Bi Samira bint Salim Al-Maamariyah
10. & 11. Wageni kutoka kwa Kabaka
12. Shaikh Mohammed bin Abeid Al-Hajj
13. Sayyid Soud Ahmed Al-Busaidy
14 Riadh bin Abdalla Al-Busaidy
Kitukuu cha Sayyid Bargash anasema maneno hayo hapo chini:
Sisi hatuandiki kwa mate tunadika kwa wino.
Huyo mtoto ni mwanawe Kabaka wa Buganda na wafuasi wake katika ziara waliokuwa wakifanya Prince Badru Kakungulu ndiye aliyeletwa siku za sherehe za uhuru wa Zanzibar na ndiye aliyenichukua miye kusoma skuli ya Kibuli Kampala katika picha yumo Sayyid Jamshid na Bi. Nunu mke wa Sayyid Khalifa.
No comments:
Post a Comment