Mshume Kiyate na Nyerere Baada ya Maasi ya Wanajeshi 1964 |
Waliosimama wa pili kulia ni Mzee Mshume Kiyate |
Kulia Mshume Kiyate, Julius Nyerere, Max Mbwana na Mwinjuma Mwinyikambi, 1962 |
''Kuna picha mashuhuri ya Mzee Mshume na Baba wa Taifa iliyopigwa Novemba 1962 wakati wa Uchaguzi Mkuu.
Picha hiyo inamuonesha Mzee Mshume akiwa amevaa koti, kanzu na kofia amemshika Baba wa Taifa mkono akimsindikiza kupiga kura.
Karika utawala wa Baba wa Taifa, magazeti ya ''Uhuru'' na ''Daily News,'' yamekuwa yakiitumia picha hii kila baada ya miaka mitano katika uchaguzi wa rais kama njia ya kuwahamasisha watu kupiga kura na kumchagua Baba wa Taifa. ''
Mtaa huu wa Tandamiti ulipewa jina la Mzee Mshume Kiyate kwa ajili ya kutambua mchango wake kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kwa TANU na juhudi zake katika kupigania uhuru wa Tanganyika miongo miwili imepita kibao hakijabadilishwa
|
No comments:
Post a Comment