Monday, 21 April 2014

JAMII FORUMS (JF) MGOGORO WA EAMWS

#368   Report Post    
Mohamed Said's Avatar
JF Senior Expert MemberArray
Join Date : 2nd November 2008
Posts : 5,326
Rep Power : 66113










Likes Received
3554










Likes Given
217

Default Re: Kutoka kofia ya barghashia ya Nyerere 1964 hadi msalaba wa William Lukuvi 2014

Quote By Fundi Mchundo View Post
Kumbe wewe ndio Ngongoseke? Mpunguze basi hizo ID.

Muulize huyo Al Alama Mohamed Said kuhusu mahusiano ya karume na hiyo EAMWS? Na unajua nani alianzisha hiyo EAMWS na kwa nini waswahili katika TANU waliipinga?

Unazungumzia ule msingi uliokuwa Chang'ombe, pesa mkazinywa na baadae mkadhulumiana wenyewe.

Au unazungumzia Chuo Kikuu chenu kinachotia fora mlichopewa baada ya Kafir mmoja kuchukua mali ya umma na kuwapa?

Amandla.....
Fundi Mchundo,
Mimi hupenda kuandika jambo kwa makini na bila mzaha kwa kuwa siko hapa
kufanya mchezo.

Nakusihi unichukulie hivyo ili tuwe na mjadala wa manufaa utakaoelimisha na
labda Allah akipenda kuinusuru nchi yetu.

Katika kitabu changu, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968)
The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism,'' bila hofu
nimezungumza mengi ambayo yalikuwa mwiko kusemwa.

La kwanza ni kuwa Nyerere hakuasisi TANU na muaisisi wa chama kile ikiwa
tutamchukua mtu mmoja katika lile kundi la ile kamati ya ndani basi aliye aula
zaidi ni Abdulwahid Kleist Sykes.

Hili lilizua kishindo kikubwa sana na bado vumbi lake halijatulia kote nipitapo hili
swali lazima litajitokeza.

La pili nililosema ni kuwa kumekuwa na njama ya kuivuruga historia ya uhuru
wa Tangayika.

La tatu na hii ni mwisho wa kitabu nilieleza kuwa Kanisa Katoliki na Nyerere
kutoka uhuru upatikane wamekuwa katika vita dhidi ya Uislam Tanzania na
hapa ndipo unapoingia mgogoro wa EAMWS.

Haya ni maneno mazito na ukiyasema kama nilivyoyasema mie lazima uwe na
ushahidi madhubuti.

Kitabu changu kimejaa ushahidi wa haya.
Kila aliyejaaliwa kukisoma kitabu hiki alibaki kinywa wazi.

Ndiyo maana hadi leo kutoka kitabu kichapwe mwaka 1997 hajatokea mtu
yoyote kukipinga kwa kuandika huo unaosemekana ni ''ukweli.''

Palikuwa na ugomvi kati yangu na mchapaji (publisher) nilianza kitabu kwa
kuanza na maneno haya:''Bismillah Rahmani Rahim,'' akaniuiza kwa nini nataka
kuanza ''an academic work with religious undertones?''

Mhariri wa kitabu hiki alikuwa Prof. mmoja mwanamke wa Kiingereza.

Nilimjibu nikamwambia haya ninayosema nataka Allah ndiye awe shahidi yangu
wasije watu wakasema kuwa mimi ni muongo.

Ushauri wake kwangu ulikuwa kitabu kimejitosheleza hapana haja ya kufanya
hivyo.

Mimi niliamini kuwa eyote amuaminiye Mungu akiona nimemtanguliza katika kauli
yangu atajua kuwa sifanyi mchezo nisemayo ni kweli na kweli tupu.

Sasa kisa cha Nyerere na EAMWS na Karume umtajae ni kisa nakijua vyema
sana.

Katika mkasa huo wa EAMWS Karume alifikia kumkufuru mola wake.

Karume yuko mbele ya Allah itoshe tu kuuombea dua Allah amsamehe madhambi
yake.

Ndiyo maana Nyerere kafa hakutaka anasibishwe na Abdu Sykes wala na mdogo
wake Ally katika kuuunda TANU pamoja na wazalendo wengine takriban sasa wote
wako mbele ya haki.

Katika mazingira kama haya ndiyo maana historia ya TANU haimtaji popote Sheikh
Hassan bin Amir
 wala Sheikh SuleimanTakadir...

Ndiyo maana hadi leo hakuna historia ya uhuru ukitoa kitabu changu ambacho
''publishers'' wote nchini walikiogopa nikaenda kukichapa Uingereza.

Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Haroub Othman na Dk. Kamata walikuja kunihoji
kuhusu Nyerere kwa kuwa wao wanaandika maisha ya Mwalimu Nyerere.

Tulifanya session tatu na mazungumzo yetu yanakaribia dakika 180.

Mimi niliwashauri kuwa waende kwa Mama Maria Nyerere atawaeleza historia
ya TANU kama alivyoishuhudia kwa jicho lake kuanzia mwaka 1953.

Hiyo itajazilia mazungumzo yangu.

Nikawaambia kuwa kwa kuwa siku nyingi zimepita wanaweza kuamsha kumbukumbu
za Mama Maria kwa kumkumbusha mashoga zake wawili Bi Mwamvua bint Masha 
(Mama Daisy) na Mwalimu Sakina bint Arab kwani mengi walifanya pamoja wakati
wa kudai uhuru.

Fundi Mchundo,
EAMWS haikupingwa na Muislam yoyote na ushahidi upo.

Wakati wa mgogoro ule mwaka 1968 hapo TANU New Stret Baraza la Wazee wa
TANU lililokuwa chini ya Mwenyekiti wake Mzee Iddi Tulio lilikuwa lishavunjwa na
Nyerere mwaka 1963 kwa kisingizio cha ''kuchanganya dini na siasa.''

Hawa ndiyo wazee waliompeleka Nyerere Umoja wa Mataifa (UNO) mwaka wa 1955.

Hapakuwa na watu wa maana tena pale.

Yako mengi lakini haya niliokueleza nadhani yameshakupa picha unazungumza na
nani.

Napenda kumaliza kwa kukueleza kuwa jana nilitembelewa na mwanafunzi ambae
anafanya shahada ya uzamili na katika kukamilisha shahada yake anatakiwa aafanye
utafiti.

Alinihoji kuhusu Sheikh Hassan bin Amir.
Nilimwekea mhadhara mmoja niliotoa Zanzibar kuhusu Sheikh Hassan bin Amir.

Ghafla nimemuona kijana kajiinamia machozi yanamlengalenga.

Kushoto Kwenda Kulia: Dr. Kamata, Prof. Saida Othman Yahya
na Prof. Issa Shivji

Kushoto ni Prof. Saida Othman Yahya na Kulia ni Prof.
Issa Shivji na Aliyekaa ni Mwandishi Akifanyiwa Mahojiano
Kuhusu Mwalimu Nyerere


No comments: