Monday, 14 April 2014

USHAHIDI WA KUPOTOSHWA HISTORIA YA ZANZIBAR WATINGA BUNGE MAALUM LA KATIBA DODOMA

Mzee Mohamed Omari Mkwawa Akikionyesha Kitabu ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru''
Kilichoandikwa na Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Harvard, Dk. Harith Ghassany
 Kitabu hiki Ndicho Kinachoeleza Historia ya Kweli ya Zanzibar

Huenda ikaonekana napiga zumari langu mwenyewe au nataka kumkweza rafiki yangu mwandishi wa kitabu, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' Dk. Harith Ghassany...

Lakini ukweli ni kuwa hii leo katika Bunge Maalum la Katiba, Dodoma, Mh. Tundu Lissu kaingia ukumbini na kitabu hicho hapo juu kilichoshikwa na Mzee Mohamed Omar Mkwawa mmoja wa wanamapinduzi kutoka Tanganyika aliyeshirika katika kupindua serikali ya Zanzibar mwaka 1964.

Fatilia hapa kwa taarifa zaidi...

Umefunguliwa uzi Jamii Forums ambao kivutio kikubwa ni Mh. Tundu Lissu ambae katika kuhitimisha mchango wake katiba Bunge Maalum la Katiba kakinyanyua juu ndani ya Bunge kitabu maarufu cha Dk. Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' na akaelezea kuuawa kwa Kassim Hanga na kusema kuwa ukweli wote kuhusu mauaji ya Hanga yamo ndani ya kitabu hicho.

Ingia hapo chini usome hisia za wanajamvi JF kuhusu yale yaliyojiri leo huko Dodoma:

No comments: