NKAMIA KASEMA KWELI:
WAISLAMU TUZUNGUMZE NA MWENYE MBWA
Mwezi
Februari 2007, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Jakaya Mrisho
Kikwete alimteuwa Profesa Idris Kikula kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Dodoma yaani UDOM na Profesa Shaaban Mlacha kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho
kwa upande wa Utawala na Fedha. Aidha Mhe Kikwete alimteuwa Profesa Ludovick Kinabo
kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho kwa upande wa Taaluma. Viongozi hawa
wakubwa watatu wamekuwa wakifanya kazi chini ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma
Mhe. Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada
ya uteuzi wao, viongozi hao walishughulikia kujenga Chuo cha UDOM ambapo
ilipofika mwezi Agosti 2007, wanafunzi wapatao 5,000 walidahiliwa chuoni hapo
na masomo yakaanza.
Mara
tu baada ya chuo kufunguliwa, tuhuma kadhaa zenye hisia kali za kidini zilianza
kuelekezwa kwenye uongozi wa Chuo na hasa kwa Profesa Kikula na Profesa Mlacha.
Baadhi tu ya shutuhuma hizo ni kuwa Chuo cha UDOM kinafungwa kabisa siku za Ijumaa
ili kuwapa nafasi wanafunzi waende kuswali msikitini. Kwa upande wa udahili wa
wanafunzi, shutuma kali zimeelekezwa kwa MaProfesa hawa wawili kuwa wanadahili
wanafunzi wa Kiislamu tu na kuwanyima Wakristo nafasi ya kusoma hapo chuoni.
Shutuma hizo hazikuishia hapo. Wapo watu waliodai kuwa wanafunzi WOTE wa kike wanaosoma Chuoni hapo,
bila kujali dini zao, wanalazimishwa kuvaa “Hijab”, vazi la stara kwa mabinti
wa Kiislamu.
Tuhumu
hizi na nyingine nyingi zimeendelea tokea chuo kianzishwe. Waislamu wamekuwa
wakizipuuza tuhuma hizi kwa sababu ni UWONGO
MTUPU na walidhani kuwa wanaotoa tuhuma hizi ni watu wasiojua kitu. Jambo
la kushangaza na kusitusha sana ni kitendo cha Mhe Joseph Roman Selasini Shao
Mbunge wa Rombo (CHADEMA) alipojiunga na kundi hilo na kutoa kauli Bungeni
zilizoashiria kuwa UDOM kuna udini kwa maana ya kuwa Waislamu wanawakandamiza
Wakristo.
Akichangia
mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu siku ya tarehe 15 Aprili 2013, Mhe
Selasini alitoa shutuma nzito dhidi ya Uongozi wa UDOM kuwa kuna kundi la
wanafunzi na waalimu wa Kiislamu wanaofanya vikao vya siri na kupanga njama
dhidi ya Wakristo. Kwa mapana yake, kauli ya Mhe Selasini ina maana ya kuwa
ukimya unaoonyeshwa na uongozi wa juu wa UDOM kuhusu suala hili, unathibitisha
kuwa uongozi wa Chuo unalijua suala hilo vizuri au unashiriki moja kwa moja
katika njama hizo dhidi wa Wakristo hapo chuoni. Kauli hii inawalenga Profesa
Idris Kikula na Profesa Shaaban Mlacha kwa sababu wao ndio Waislamu.
Shutuma
alizozitoa Mhe Selasini ni nzito na hazifai kupuuzwa. Kwa kulijua hilo, Mhe
Juma Selemani Nkamia Mbunge wa Kondoa Kusini alizingatia ushauri wa Wazaramo
unaosema kuwa “akutukanae kenye pombe, nawe mjibu kwenye pombe”. Akichangia
Bajeti hiyo hiyo, siku hiyo hiyo, Mhe Nkamia alisema kuwa yeye ni mwanafunzi
hapo UDOM na hajawahi kusikia ubaguzi ambao Mhe Selasini anaouzungumzia. Majibu
ya Mhe Nkamia yanazaa maswali kadhaa ambayo ni vyema Waislamu tukajiuliza. Hivi
ni kwa nini shutuma nyingi na hasa za udini zimekuwa zikielekezwa kwenye Taasisi
kubwa ambazo zinaongozwa na Waislamu? Ni kwa nini Wakristo wamekuwa na tabia ya
kuamini na kutaka jamii yote iamini kuwa Muislamu akipewa nafasi ya juu ya
uongozi atakuwa amepewa kwa sababu tu ya Uislamu wake na wala si sifa zake? Ni
kwa nini akiwepo Muislamu zaidi ya mmoja kwenye uongozi wa juu (kama ilivyo
UDOM), Wakristo wanaamini kuwa Waislamu hao wamependelewa na kuwepo kwao hapo
hawatotenda haki kwa Wakristo? Kwa nini Wakristo wakiwa wengi kwenye uongozi wa
juu wa Taasisi yoyote ile wanaamini kuwa hiyo ni haki yao?
Ili
kupata majibu ya baadhi ya maswai haya, tuangalie Jukwaa ambalo Mhe Selasini
amelitumia kutoa shutuma zake. Jukwaa alilolitumia ni Bunge. Mara tu baada ya
Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, Waheshimiwa Wabunge walifanya uchaguzi kuchagua Mhe Spilka,
Mhe Naibu Spika na Waheshimiwa Wenyeviti wa Bunge (Presiding Officers) Watatu.
Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, kati ya Wenyeviti Watatu wa Bunge, mmoja lazima
atoke Zanzibar. Matokeo ya uchaguzi huo ni kuwa viongozi WOTE walikuwa Wakristo! Uongozi ulikuwa kama ifuatavyo:
Spika Anna Makinda Mkristo
Naibu
Spika Job Ndugai Mkristo
Mwenyekiti Jenister Mhagama Mkristo
Mwenyekiti George Simbachawenye (baadae Mhe Zungu) Mkristo
Mwenyekiti Sylvester Massale Mabumba (Dole, Zanzibar) Mkristo
La
kushangaza ni kuwa hata pale alipotakiwa Mbunge kutoka Zanzibar ili awe
Mwenyekiti wa Bunge basi nafasi hiyo pia akapewa Mkristo! Ikumbukwe kuwa Mhe
Mabumba ndio Mbunge PEKEE kutoka
Zanzibar ambaye ni Mkristo! Kwa upande wa Menejimenti, Katibu wa Bunge (Dr
Thomas Kashilila) na Wakuu wa Idara WOTE
ni Wakristo! Je, Mhe Joseph Selasini analionaje hili?
Pamoja
na unyeti wa Taasisi hii, hata mara moja Waislamu hawajalalamika kuwa Bunge
linaongozwa na Wakristo watupu. Wao wamekuwa wakiamini kuwa waliochanguliwa
wamechaguliwa kwa uwezo wao (na sio
vinginevyo) na kwamba watatekeleza majukumu yao kwa haki na kwa faida ya taifa.
Sasa kwa nini mantiki hiyo hiyo haitumiki pale ambapo Waislamu wamechaguliwa au
wameteuliwa kuongoza Taasisi yoyote ya Umma? Kwa nini kuwepo na mashaka kuwa
wamepata nafasi hizo kwa sababu tu ya dini zao?
Kama
Mhe Selasini anaona kuwepo kwa Profesa Kikula na Profesa Mlacha UDOM ni udini,
je ameangalia uongozi wa juu wa Vyuo Vikuu vyote vya Umma hapa nchini? Kwa Mhe
Selasini na wale wanaoitakia mema Tanzania, wafahamu kuwa jumla ya Vyuo Vikuu
vya Umma na Taasisi za Umma za Elimu ya Juu zinazotoa shahada kwa kiwango cha Digirii
hapa nchini ni 19. Ukijumuisha na Tume ya Vyuo Vikuu yaani Tanzania Commission
for Universities (TCU) ambaye ndiye Mdhibiti, jumla zinakuwa Taasisi 20. Kati
ya Vyuo/Taasisi hizo 20, Wakuu wa Vyuo/Taasisi 17 ni Wakristo na Wakuu 3 tu
ndio Waislamu. Kiuwiano hii ni sawa na 85% Wakristo na Waislamu ni 15% tu kama
inavyoonekana hapa:
1.
Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Idris Kikula Muislamu
2.
Chuo Kikuu cha Ardhi Prof.
Idris Mshoro Muislamu
3.
Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dr. Abuu Mvungi Muislamu
4.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.
Rwekaza Mukandala Mkristo
5.
Chuo Kikuu cha Sokoine Prof.
Gerald C Monela Mkristo
6.
Chuo Kikuu cha Tiba M’bili Prof. Kaaya Mkristo
7.
Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof. Joseph
Kuzilwa Mkristo
8.
Chuo Kikuu Huria Prof.
Tolly Mbwette Mkristo
9.
Chuo Kikuu cha Tek. Mbeya Prof. Joseph
Msambichaka Mkristo
10.
Chuo Kikuu cha Katavi ??????? Mkrsto
11.
Chuo cha Moshi MUCCOBS Prof. Faustine K
Bee Mkristo
12.
Chuo cha Elimu DSM (DUCE) Prof. Mfinanga Mkristo
13.
Chuo cha Elimu Mkwawa Prof. Amandina
Lihamba Mkristo
14.
Chuo cha IFM Prof. Godwin
Mjema Mkristo
15.
Taasisi ya Nelson Mandela Prof. Burton
Mwamila Mkristo
16.
Taasisi ya Teknolojia DSM Prof. Kandoro Mkristo
17.
Chuo cha Biashara (CBE) Prof.
Mjema Mkristo
18.
Chuo cha Mwalimu Nyerere Prof.
Magotti Mkristo
19.
Chuo cha Uhasibu Arusha Prof.
Johannes Monyo Mkristo
20.
Tume ya Vyuo Vikuu Prof.
Sifune Mchome Mkristo
Nadhani
wengi watakumbuka kuwa mwaka jana wakati Rais Kikwete ameteuwa wajumbe wa Tume
ya Katiba, Bwana Edwin Mtei aliandika kwenye jamiiforums kupinga uteuzi ule kwa madai kuwa wajumbe wengi ni
Waislamu. Katika kutetea hoja yake, mzee Mtei amedai kuwa katika utendaji wa
kazi si rahisi mtu akaweza kujizuia hisia ya imani (dini) yake isiingilie
utendaji wake. Hivyo basi, mzee Mtei alidai kuwa kwa kuwa Tume ya katiba ina
wajumbe wengi Waislamu, itakuwa rahisi kwa imani ya dini hiyo kupenyezwa katika
Katiba mpya. Kwa kuzingatia hoja ya mze Mtei, kama uongozi wa Vyuo Vikuu na
Taasisi za Elimu ya Juu nchini upo katika sura tuliyoionyesha hapo juu, ni
dhahiri kuwa si rahisi kwa vijana wa Kiislamu kupata Elimu ya Juu na hasa
ukizingatia kuwa Baraza la Mitihani limesheheni Wakristo na tokea liundwe
halijapata HATA MARA MOJA kuongozwa
na Mwislamu.
Hivi
karibuni kumekuwa na malalamiko kuwa Mhe Rais Kikwete anateuwa Waislamu katika
nafasi nyeti za uongozi. Mifano mikubwa ambayo imekuwa ikirudiwa mara kwa mara
ni Mkuu wa Polisi Saidi Mwema, Mkurugenzi wa Usalama Othman Rashid, Jaji Mkuu
Mohamed Chande na Waziri wa Ulinzi Mhe Shamsi Nahodha. Wakati Wakristo
wanalalamikia teuzi hizo mbalimbali ambazo zimezingatia uwezo, ujuzi na uzoefu
wa Walioteuliwa, wanasahau kabisa kuwa kwa kipindi kirefu wakati wa utawala wa
Awamu ya Tatu Viongozi Waandamizi wa Chama na Serikali walikuwa Wakristo lakini
Waislamu hawakuliona kama hilo ni tatizo. Mwaka 1996, mara tu baada ya Serikali
ya Awamu ya Tatu ilipoingia madarakani uongozi ulikuwa hivi:
Serikali
Benjamin William
Mkapa Rais wa Jamhuri ya
Muungano Mkristo
Fredrick T Sumaye Waziri Mkuu Mkristo
Maokola Majogo Waziri wa Ulinzi Mkristo
C. Apson Mkurugenzi wa
Usalama Mkristo
Harun Mahundi Mkuu wa Polisi Mkristo
Jenerali Robert Mboma Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mkristo
Wakristo
wamesahau kuwa katika kipindi hicho Wakuu WOTE
wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na Waziri wa Ulinzi walikuwa Wakristo WATUPU mpaka baadae alipoteuliwa
Mahita. Katika utawala wa Rais Kikwete haijatokea HATA MARA MOJA Wakuu wote wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakawa
Waislamu watupu! Aidha ni vyema tukajikumbusha kuwa wakati WOTE wa utawala wa Rais Kikwete Mkuu wa Majeshi amekuwa ni Mkristo.
Chama
Benjamin William
Mkapa Mwenyekiti Mkristo
John Samwel Malecela Makamu Mwenyekiti Bara Mkristo
Philip Mangula Katibu Mkuu Mkristo
Si
hivyo tu, Wakristo pamoja na Mhe Selasini wamesahau kuwa katika kipindi CHOTE cha Serikali ya Awamu ya Tatu Mihimili
YOTE ya dola ilikuwa inashikwa na
Wakristo kama ifuatavyo:
Benjamin
W Mkapa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mkristo
Pius
Msekwa Spika wa Bunge Mkristo
Francis
Nyalali Jaji Mkuu Mkristo
Barnabas
Samatta Jaji Mkuu Mkristo
Aidha
hali hiyo hiyo ilijitokeza wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Julius
Nyerere wakati yeye alipokuwa Rais, Spika wa Bunge Chifu Erasto Mang’enya na
Jaji Mkuu Agostino Saidi/Francis Nyalali.
La kushangaza ni kuwa kila alipokuwa Rais Mkristo Mihimili yote Mitatu
wa Dola imekuwa chini ya Wakristo. Lakini haikuwahi kutokea hata mara moja
wakati Rais ni Muislamu (kama ilivyokuwa wakati wa Rais Mwinyi na sasa Rais
Kikwete) Mihimili ya Dola kushikwa na Waislamu watupu. Hili halijawahi kutokea
hata mara moja.
Kwa
kuzingatia hoja ya Mhe Selasini na wengine wenye fikra kama zake, uongozi wa
UDOM ni mbovu kwani umeshindwa kudhibiti upendeleo na ukandamizaji unaofanywa
na Waislamu dhidi ya Wakristo. Swali la kumuuliza Mhe Selasini je wakati
Waislamu walipodhulumiwa waziwazi na Dr Joyce Ndalichako Katibu Mtendaji wa
Baraza la Mitihani kwa kufelishwa kwa makusudi kabisa mbona hatukumsikia
kusimama Bungeni kuzungumzia dhulma hii? Wakati Getrude Mongella alipokula pesa
Dola 200,000 za Bunge la Afrika na Serikali akakubali kulipa deni lile, mbona
Mhe Selasini hakusimama Bungeni kupinga hoja hiyo? Au kwa sababu tu Ndalichako
na Mongella ni Wakristo?
Wakati
Dr Charles Kimei Mkurugenzi wa Benki ya CRDB anatoa maagizo kwa Mameneja wake wote
wa Mikoa kuwa watoe Sadaka Kanisani (fungu la 10) kutokana na faida ambayo
Benki imepata, mbona Mhe Selasini hakuhoji Bungeni wizi huu wa sehemu ya fedha
za Umma (kwa sababu Serikali ina hisa 40% CRDB) zinazopelekwa Kanisani? Au kwa sababu Dr Kimei ni Mkristo na anatoka
Rombo kama yeye? Unafiki huu wa Mhe Selasini na watu wa aina yake mpaka lini?
Mwaka
1993 tumeshuhudia utiaji sahihi wa Makubaliano baina ya Serikali na Makanisa
kuhusu Serikali kuwapa fedha Makanisa ili waendeshe huduma za afya katika
hospitali zao ambazo zitatumika kwa wananchi pia. Waislamu walilalamikia sana
utaratibu ule kwa sababu wajibu wa kutoa huduma ya afya ni wa Serikali. Hivyo
basi isingekuwa vyema kwa Serikali kujivua wajibu wake na kuipa Taasisi
nyingine. Mantiki ya utaratibu ule ilikuwa ni utaratibu wa muda hadi hapo
Serikali itakapopata uwezo wa kujenga hospitali zake. Cha kushangaza ni kuwa
kwa miaka 20 sasa tumeshuhudia namna fedha za Umma zinavyoporwa na kupelekwa
Makanisani kwa kisingizio cha kuendesha hospitali teule na kwamba Serikali
haina dalili ya kujenga hospitali za Umma. Ikiwa Serikali imeweza kujenga shule
za Kata nchi nzima kwa chini ya miaka 2, iweje leo Serikali imeshindwa kujenga
zahanati za Kata nchi nzima ili kukomesha uporaji wa mali ya Umma unaofanywa na
Makanisa?
Kwa
kuwa Bunge letu lipo katika kipindi cha kujadili Bajeti ya Serikali namwomba
Mhe Selasini wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Afya asimame na kuhoji
kwa nguvu zote tokea mwaka 1993 hadi leo Serikali imetumia kiasi gani kuhudumia
hospitali za Makanisa? Ni kiasi gani zinahitajika kujenga zahanati za Kata nchi
nzima? Kwa nini katika kipindi chote cha miaka 20 Serikali haikuona umuhimu wa
kujenga hospitali zake na kutimiza wajibu wake kwa raia ambao wanalipa kodi?
Iweje Serikali ishindwe kujenga na kuendesha hospitali hali ya kuwa ina vyanzo
vingi vya mapato lakini Kanisa liweze kufanya hivyo kwa kutegemea fedha za
Serikali na misaada? Ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa hospitali za Umma
ili kuachana na utaratibu wa sasa wa kupora fedha za Umma na kupeleka kwenye
mahospitali ya Kanisa?
HITIMISHO
Kwa
kuhitimisha tunapenda kumfahamisha Mhe Selasini na wenziwe wenye mawazo kama
yake kuwa nchi hii imekuwa na amani kwa muda mrefu kutokana na uvumilivu wa
Waislamu. Ni vyema Mhe Selasini akafahamu kuwa amani ya kweli inaenda na HAKI. Amani na haki ni sawa na watoto
pacha. Tokea nchi yetu ipate uhuru Waislamu wamefanyiwa madhila makubwa sana na
kumekuwa na hila nyingi sana za kuwarudisha nyuma kimaendeleo na pia
kuwagombanisha na jamii. Mara kadhaa Waislamu wamekuwa wakihusishwa na vitendo
vya uvunjaji wa amani kama vile kusingiziwa kuingiza kontena la majambia nk.
Lengo kuu ni kuionyesha jamii kuwa Waislamu ni watu wa shari. Aidha viongozi wa
Kiislamu Serikalini wamekuwa wakitupiwa shutuhuma mbalimbali kama ambavyo
alivyofanyiwa Profesa Kighoma Malima alipozushiwa uwongo kuwa amejenga msikiti
Wizara ya Elimu nambo mengineyo.
La
kushangaza ni kuwa wakati haya yote yanaendelea, Wakristo wamekuwa wakifanya
vitendo vya kutishia amani waziwazi lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa
dhidi yao. Mfano Wakristo wametangaza kuundwa kwa Tume ya Kijeshi ya Kikristo.
Jambo hili ni la hatari sana na linaacha maswali mengi bila kupata majibu. Je
Tume hii ipo ndani ya Jeshi letu la Ulinzi au nje ya Jeshi? Je Makamanda wake
ni nani na wanaripoti wapi? Je Amiri Jeshi Mkuu wake ni nani? nk.
Kwenye
Gazeti la Mtanzania la tarehe 10 Aprili 2013 kuna mwandishi ameandika makala
kuhusu vuguvugu la udini linaloendelea hivi sasa nchini. Kwa mujibu wa jina la
mwandishi, inaelekea ni Mkristo. Kubwa katika aliyoyaandika ni kuwa Waislamu
wanalalamika hawana uwakilishi wa kutosha kwenye vyombo vya maamuzi na
Serikalini. Pamoja ya kuwa huo ndio ukweli, mwandishi anasema kuwa si vyema
watu wakapewa dhamana kubwa kwa sababu tu za dini zao na kuwa na haja ya kupata
uwiano mzuri wa dini hizi mbili. Kama Waislamu hawapati fursa ya kushika
nyadhifa kubwa Serikalini kwa sababu ya upungufu wa sifa na hasa elimu, ni
vyema basi Serikali ikaliangalia suala la kuwaendeleza Waislamu kielimu. Pamoja
na Ukristo wake, mwandishi amekuwa mkweli na anaona hatari iliyopo mbele yetu
ya kuliacha kundi kubwa la raia likiwa nyuma kimaedeleo wakati kundi jingine
linapiga hatua. Hawa ndio wazalendo wa kweli na wanaoitakia mema Tanzania ili
iwe na amani ya kudumu sio kama Mhe Selasini ambae anaongozwa na jazba na
mihemuko.
Kwa
upande wa Waislamu, nadhani wakati sasa umefika wa kuzungumza na mwenye mbwa.
Mhe Juma Nkamia amefikisha ujumbe. Kilichobaki ni
wajibu wetu kuufanyia kazi.
1 comment:
Mzee Mohamed Said kitu kimoja kinanishangaza sana hapa kwetu Tanzania.
Wakristo wanapoongelea mambo mambo yao HUO UNAKUWA SIO UDINI!
Lakini Waislamu wakifanya hivyo hivyo UNAKUWA NI UDINI.
Sijui lini Viongozi wa Watanzania watakuja kufahamu kuwa Double Standard Mwisho wake huwa mbaya sana.
Elimu unayo itoa hapa Laiti wangeifuatilia basi naimani kubwa Kungekuwa na maendelea na mshikamano mkubwa sana baina ya wananchi wa imani zote mbili.
Mungu ibariki nchi yetu.
Amen.
Post a Comment