Thursday, 24 April 2014

PROF. MUSTAFA HAMZA NJOZI AZUNGUMZA BUNGE MAALUM LA KATIBA HANSARD YAULIZA MBONA LEO MAMBO TOFAUTI?


Ikulu haikutoa sifa za Prof. Mustafa Hamza Njozi wakati wanatoa majina ya wabunge kutoka Taasisi za Elimu:

TAASISI ZA ELIMU- TANZANIA BARA

1. Dr. Suzan Kolimba 
2. Prof. Esther Daniel Mwaikambo
3. Dr. Natujwa Mvungi 
4. Prof. Romuald Haule
5. Dr. Domitila A.R. Bashemera 
6. Dr. Jasmine Bendantunguka Tiisekwa
7. Prof. Bernadeta Kilian 
8. Teddy Ladislaus Patrick
9. Dr. Francis Michael 
10. Prof. Remmy J. Assey
11. Dr. Tulia Ackson 
12. Dr. Ave Maria Emilius Semakafu
13 ?Hamza Mustafa Njozi

Katika hali hii wengi wakashangazwa imekuwaje wasomi wote katika Bunge Maalum la katiba CV zao zimewekwa isipokuwa ya Prof. Njozi? Ikulu haikuweka hata baadhi ya vitabu alivyoandika ambavyo vyote ni maarufu kama ''Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania,'' na ''Muslim and the State in Tanzania.'' Umma ulipigwa na mshagao. Katika mitandao ya jamii jambo hili liliwashughuliwa watu wengi. Wako waliolaumu kwa Prof. Njozi kuvunjiwa heshima na kuna wengine ka kutomjua Prof. Njozi ni nani walimkejeli kuwa ''si lolote si chochote.'' Nilipoona kejeli na dharau kwa Prof. Njozi niliandika maneno haya:

''Katika mengi ambayo wengi hawayajui kuhusu Prof. Njozi ni kuwa wakati anafanya shahada yake ya pili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alifanyiwa njama za kufelishwa na akafelishwa japo kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiongoza darasa kwa uhodari. Mimi binafsi nimepata kufatana na Prof. Njozi katika mikutano ya kimataifa ambako alitoa mada za kusisimua. Nimewahi kufuatana na Prof. Njozi Kampala (2003), Nairobi (Chuo Kikuu Cha Kenyatta, (2006) na Chuo Kikuu Cha Johannesburg (2006). Kuwa watendaji wa serikali hawamjui Prof. Njozi hili sikubali. Kama hawamjui msomi wa kiwango wa Prof. Njozi watamjua msomi gani? Hii ndiyo hatari dini moja kuhodhi madaraka yote ya serikali. Sasa siku hizi ukitahadharisha kuhusu hili unaitwa, ''mchochezi'' kama si ''gaidi.''
http://www.mohammedsaid.com/2014/02/bunge-la-katiba-cv-ya-prof-hamza.html

Kushoto Kwenda Kulia: Prof. Njozi. Mohamed Said Johannesburg 2006

Kushoto Kwenda Kulia: Mohamed Said, Prof. Hamza Mustafa Njozi
Kenyatta University, Nairobi 2006


Prof. Njozi amekuwa mtu wa kuandamwa na ''bahati mbaya'' katika historia ya maisha yake. Kitabu chake, ''Mwembechai Kilings...kilipigwa marufuku na serikali na ukionekananacho utasimamishwa mahakamani kwa kosa la jinai. Sababu ya Prof. Njozi kuandika kitabu hiki ni kutokana na maneno ya Rais Benjamin Mkapa aliyetaka aletewa ushahidi wa kisayansi kuwa kuna udini katika serikali yake. Ushahidi ulipoifikia serikali kupitia kitabu cha Prof. Njozi serikali haikuweza kustahamili. Uamuzi ulikuwa ni kukipiga kitabu marufuku kisomwe na ukweli ukajajulikana na Waislam kuwa hakika wanabaguliwa. Leo Prof. Njozi kazungumza katika Bunge Maalum la Katiba. Hakika tofauti ilijitokeza wazi kiasi Hansard ikawa inashangaa kimezidi nini leo mbona uwanja kimya. Mechi hii watazamaji wamezuiliwa kuingia uwanjani?

Fuatilia ukurasa huu kwa maalumati ya Prof. Njozi.

Kalamu ya Hamza Njozi haina mfanowe. Yoyote aliyemsoma hili litamdhihirikia. Miaka mingi iliyopita wakati wa enzi la gazeti lililokuwa maarufu la Africa Events (AE) lililokuwa likichapwa London chini ya uhariri wa Mohamed Mlamali Adam, nilipata siku moja kuzungumza na Ahmed Saleh Yahya ambae alikuwa mmoja katika waandishi wa AE aliniambia kuwa wamepokea makala kutoka kwa ''jamaa mmoja.'' Ahmed Saleh Yahya akaendelea kusema kuwa ''huyu jamaa'' kutokana na ile makala inaelekea ana elimu ya juu sana. Mimi kwa pale sikuweza kujua ni nani aliyekuwa amekusudiwa. Ile makala ilipochapwa na ingawa jina lake alikuonyeshwa kwenye ile makala, mara moja niliitambua kalamu ya Hamza Njozi. Miaka mingi imepita sikumbuki khasa nini yalikuwa maudhui ya makala ile ila kitu kimoja nakikumbuka hadi leo. Prof. Njozi ni ''wordsmith.'' Bingwa wa lugha ya Kiingereza. Katika makala ile nilipata msemo ambao hadi leo nautumia kila nipatapo nafasi aidha niandikapo au ninapozungumza. Katika maka ile alitumia maneno haya katika kueleza ''tofauti.'' Aliandika maneno haya, ''...a different crop.'' Alikuwa na maana kuwa ''hicho ni kitu kingine,'' kwa maana kuwa mathalan kama ulikuwa unawaonea wale hawa ni watu tofauti, yaani usithubutu kwa hawa ''...these are a different crop.''

Msikilize Prof. Njozi akizungumza:
https://soundcloud.com/omari-abdallah-makoo/profesor-h-njozi
(Ikiwa huwezi kusikiza hapa nakili na weka kwenye browser)
Jaribu na hapa chini:
file:///C:/Users/Mama%20Nasir/Documents/Downloads/bdda033dce2f82d74d09a3aa2040c306%20(1).mp3

file:///C:/Users/Mama%20Nasir/Documents/Downloads/ANNUUR%201122-APRIL%2025-2014.pdf

http://www.mohammedsaid.com/2014/04/prof-mustafa-hamza-njozi-azungumza.html


No comments: