Hassan Abdullah Khamis wa Radio Kheri Akimuhoji Mohamed Said Katika Kipindi Maalum cha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar |
Msomaji,
Fuatilia hapa mazungumzo kati ya Meneja wa Radio Kheri Hassan Abdullah Khamis ujue nini kilizungumzwa…
Hivi ni vipindi viwili tarehe 25 na 26 Aprili vilivyotayarishwa rasmi kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar.
Katika ufunguzi nilijaribu kueleza umuhimu wa kuijua historia ya kweli ya Zanzibar kabla na baada ya mapinduzi. Nilisisitiza ukweli kuwa historia iliyoenea ni kuwa katika jamii za Kizanzibari enzi za ukoloni Waarabu walikuwa tabaka la juu na Waafrika walikuwa ni tabaka la chini, duni kabisa. Hii kwa hakika ilikuwa propaganda mbaya kwani kulikuwa na Waarabu wengi masikini wakifanya kazi nyingi tu za chini sana kama walizokuwa wakifanya Waafrika. Walikuwapo Waarabu vinyozi, wabeba mzega (wauza maji), waokota mbata, matopasi maarufu wakijulikana kama ''wazamia lulu'' na lulu yenyewe ni hicho kinyesi, wachumaji karafuu nk. nk. Nilizungumza kuhusu hatari za propaganda ya biashara ya utumwa na kueleza kuwa hiyo ndiyo iliyosababisha chuki kubwa dhidi ya Waarabu na wengi kuuliwa katika mapinduzi. Mwisho katika mengi yaliyozungumzwa siku ya kwanza ni kueleza ukweli kuwa Waarabu waliokuwapo Zanzibar si wageni ni watu walioishi katika visiwa hivyo karne na karne, mababu na mababu wakati wengine hata kupita Waafrika ambao walihamia miaka ya karibuni.
Fuatilia...
Wasomaji,
Tunatayarisha audio za kipindi na tutaziweka hapa In Sha Allah...
Fuatilia...
Waislam na Miaka 50 ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika - Part I - Mohamed Said

Hivi ndivyo walivyokuwa wakiishi watu wa visiwani kabla ya mapinduzi. Itazame picha hii ina ujumbe mzito uliojificha. |
Wasomaji,
Tunatayarisha audio za kipindi na tutaziweka hapa In Sha Allah...
Fuatilia...
Waislam na Miaka 50 ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika - Part I - Mohamed Said
No comments:
Post a Comment