Wednesday 14 May 2014

IN MEMORY OF ABDULWAHID SYKES (1924 - 1968)






Kutokana na Kiwanuka, mwandishi katika kumbukumbu ya miaka ishirini toka Abdulwahid afariki dunia, aliamua kuandika historia fupi ya maisha yake ili kukomesha upinzani wote kwa wakati ule na hapo baadae kuhusu nafasi ya Abdulwahid katika kuasisi TANU na kudai uhuru wa Tanganyika. Makala hii ilifuatiwa na kumbukumbu iliyotolewa na watoto wake katika gazeti la CCM - Uhuru (Oktoba 12, 1988), na gazeti la serikali  Daily News (October 12, 1988) Wahariri wa magazeti ya Chama na serikali waliposoma wasifu wa Abdulwahid tayari wakawa wameshatatizwa na habari zilizokuwa katika kumbukumbu ile. Tatizo kubwa lilikuwa habari zilizoandikwa katika kumbukumbu ile zilizokuwa zinahusisha jina la Abdulwahid na matukio muhimu katika historia ya Tanganyika. Mhariri wa Daily News, Reginald Mhango, alimpigia simu mtoto wa Abdulwahid, Kleist na kumweleza kuwa hatoweza kuchapisha kumbukumbu ile hadi amepata idhini kutoka Dodoma, Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi. Hakijulikani kilichofanyika lakini kwa bahati nzuri kumbukumbu zote mbili zilichapishwa na kutokea katika magazeti yote, ya chama na serikali siku ya pili yake. 

No comments: