Rajab Omar Mtana alikuwa ni mwanakijiji wa kawaida tu akiishi kijijini Lulago, Handeni kama wanavijiji wengine wanavyoishi na alikuwa na biashara yake kuuza hiliki. Siku moja akaja mnunuzi mfanyabiashara ya hiliki nyumbani kwake kununua hiliki na akamuuzia. Yule mfanyabiashara alipokuwa anatoka na gari yake akasimama kwenye kizuizi cha kulipia ushuru. Alipotakiwa kulipa ushuru akasema kuwa si hiliki yote amenunua katika kijiji hicho kwa hiyo hawezi kulipa ushuru wa hiliki yote. Hapo palitokea ubishi na mfanyabiashara yule akagonga lile geti na akaondoka. Hii ikapelekea kwa wakusanya ushuru kwenda nyumbani kwa Rajab Omar Mtana kumkamata na kumweka chini ya ulinzi katika ofisi ya serikali ya kijiji hadi hapo atakapolipa ushuru ambao yule mfanyabiashara alitakiwa alipe. Ndugu zake Rajab Omar Mtana wakenda pale ofisini kwa nia ya kumtoa ndugu yao na hapo pakatokea vurugu na mapigano. Katika mapigano hayo, mgambo ajulikanae kwa jina la Mbwana ambae ndiye aliyekuwa akishughulika na kudai ushuru akauawa. (Kisa hiki kipo humu na kimeelezwa kwa ufasaha na Sheikh Chambuso wasomaji mnaweza mkakisikiliza kupitia ''gallery.'' Tunatayarisha muhtasari wake na tutauweka hapa In Sha Allah). Kisa hiki cha ushuru wa hiliki ndicho kilichozua balaa kubwa la mauaji na uchomwaji moto nyumba za Waislam wa Madina na kuvunjwa kwa misikiti na vijiji ambavyo vilikuwa na idadi kubwa ya wakazi wake Waislam. Baada ya haya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa akatoa amri kuwa hapana ruhusa tena ya sehemu ile kuwa makazi kwa kisingizio kuwa hizo ni kambi za ugaidi. Huyu bibi alisema mengi ambayo takriban yote yamedhihirika kuwa ni uongo mathalan kuwa kuna Al Shabab, mahandaki ya vita, silaha za kutungulia ndege nk. nk.
Katika Waislam waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka mahakamani Handeni ni huyu kijana Rajab Omari Mtana. Baada ya kukaa rumande alipata dhamana yeye pamoja na wenzake na akawa nje. Mwezi uliopita Rajab Omar Mtana alirejea kijijini kwake. Wakati anakaribia kuingia kijijini alisimamishwa na askari wa kijiji akapekuliwa na akanyang'anywa simu yake na fedha taslimu. Baada ya mkasa huu walimwachia na yeye akaendelea na safari yake. Lakini nyumba yake ilikuwa imevurugwa haifai kuishi mtu kwa hiyo alifikia kwa dada yake. Akiwa nyumbani kwa dada yake usiku alifatwa na watu wa serikali ya kijiji wakiongozwa na mgambo wawili, Salimu Magingu na Salimu Mnyendo, akatolewa ndani na kuanza kupigwa kwa bakora na kisha kwa mapanga. Kujitetea kijana huyu alikimbia huku akifukuzwa. Asubuhi kulipokucha palionekana damu nyingi sana. Taarifa ilitolewa polisi lakini hakuna kilichofanyika. Dada yake na mumewe walikamatwa na kushitakiwa katika ''mahakama'' ya hapo kijiji na wakapigwa faini ya kila mtu shs. 20.000. Kosa lao ni kumleta kijiji mtu asiyetakiwa. Sasa ni mwezi mmoja Rajab Omar Mtana hajulikani alipo na inasadikiwa ameuawa na wale waliokuja kumtoa nyumbani kwa dada yake. Ndugu yetu Rajab ametafutwa kote hadi leo hajapatikana na waliompiga na kumjeruhi wako huru nje hawajaguswa wala kuhojiwa na polisi. Wakati Sheikh Chambuso alipokuwa akinighadithia mkasa huu ilinijia picha ya kisa cha vijana watatu waliouliwa na Klu Klux Klan Mississippi katika miaka wa 1960 wakati wa ubaguzi wa rangi Marekani. Waliuliwa kama vile mtu kauwa paka msumbufu na hakuna lolote lililofanyika hadi zilipotiwa juhudi za ziada kutoka nje ya Mississippi ndipo wauaji wakatiwa mbaroni. Mauaji ya Madina yamepita hivi hivi hakuna aliyesimamishwa mbele ya vyombo vya dola. Uwezekano mkubwa ni kuwa na mauaji haya yatafata mkondo ule ule. Jambo la kusikitisha ni kuwa mauaji haya yamelenga watu wa dini moja. Je, viongozi wetu wako hadhiri na mbegu hii wanayoiacha imee?
Chiku Galawa Mkuu wa Mkoa wa Tanga |

Fatilia kisa hiki kuna mengi ya kusikitisha...
Msikilize Sheikh Chambuso akikieleza chanzo cha kadhia iliyopelekea yote haya - Waislam kuhamishwa kwenye vijiji vyao, kuchomwa moto misikiti na mauaji yanayoendelea hivi sasa:
Msikilize Sheikh Chambuso akikieleza chanzo cha kadhia iliyopelekea yote haya - Waislam kuhamishwa kwenye vijiji vyao, kuchomwa moto misikiti na mauaji yanayoendelea hivi sasa:
Sheikh Chambuso Rajab Ramadhani UONGO MKUBWA NDIYO HUU HAPA CHINI
Kuongezeka
kwa vitisho vya al-Shabaab?
''Kuwepo kwa al-Shabaab wilayani humo kulitambulika
ndani ya wiki ya mwisho ya mwezi Oktoba, wakati wananchi wasamaria wema
walipowafahamisha viongozi wa serikali kuhusu kambi ya mafunzo iliyopo katika
msitu wa Lwande.
"Tulipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema,
hususan wafugaji ambao mifugo yao ilikamatwa kila ilipokatiza jirani na kamba
hiyo ya mafunzo," alisema Liwowa. "Pia, [wafundishaji wa al-Shabaab]
walikuwa wakiwafukuza na kuwanyang'anya ardhi wenyeji kwa kiasi ambacho
walipata ekari 500."
Viongozi wenyeji wamejifunza kwamba wafundishaji
wanne wa al-Shabaab waliwasili katika wilaya ya Kilindi mwaka 2008 na kujiunga
na msikiti wa Madina, lakini wanakijiji walijitenga na wafundishaji baada ya
kuona mawazo yao yalikuwa na msimamo mkali, alisema Liwowa.
"Baada ya mapigano hayo mwishoni mwa mwaka
2008," yakitokana na mzozo uliotokea ndani ya msikiti kati ya wenyeji na
wanachama wa al-Shabaab, "wafundishaji hao walinunua kipande chao cha
ardhi na kujenga msikiti tofauti ambao sasa waliutumia kufundishia mafunzo ya
al-Shabaab," alisema.
Kutokana na taarifa zilizokusanywa hadi sasa,
baadhi ya watoto waliopata mafunzo kutoka kwa al-Shabaab katika wilaya ya
Kilindi wamepelekwa Somalia kupitia Mombasa, Kenya, alisema Liwowa. Idadi kubwa
ya wafundishaji wa al-Shabaab kutoka Somalia na Mombasa pia walikuja Kilindi
mwanzoni mwa mwaka 2013, na inaonekana kuwa na mkakati wa ufundishaji katika
mikoa mingine, kama vile Kilimanjaro, Zanzibar, Pwani na Mtwara.
Operesheni ya polisi katika wilaya ya Kilindi
inafuatia ukamatwaji wa tarehe 7 Oktoba wa washukiwa 11 wa al-Shabaab waliokuwa wakifanya mafunzo ya kijeshi
katika mkoa wa Mtwara.
Aidha, polisi walimkamata mfanyabiashara wa Tanzania Juma Abdallah Kheri tarehe 31
Oktoba huko Tanga kwa kushukiwa kwamba alikuwa akijihusisha na kuwaghiramia
makundi ya kigaidi nchini Tanzania na washirika wa al-Shabaab nchini Kenya,
Kituo cha Vijana Waislamu.
Alipoulizwa Tanzania inafanya nini kukabiliana na
vitisho vya al-Shabaab vinavyoonekana kuongezeka,Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosaya Jinai Robert Manumba alisema
polisi walikuwa wakishirikiana na mashirika mengine ya usalama kupamaba na
tatizo hilo.
"Tumeunganisha idara zote za
usalama kuunda timu maalumu. Timu hiyo inahusisha maofisa usalama kutoka
polisi, jeshi, huduma yetu ya upelelezi ya taifa, uhamiaji na [Mamlaka ya
Mapato Tanzania] ambao wanafanya kazi kwa kushirikiana kutafuta suluhisho
litakalodumu," Manumba aliiambia Sabahi.''
ADS BY GOOGLE
Haya yangelikuwa na chembe ya ukweli basi tungeona wahusika wamefunguliwa kesi ya ugaidi. Hadi leo hakuna kitu kama hicho kimefanyika badala yake Waislam wanabughudhiwa na kuuliwa. Juma Abdallah Kheri ambae alikamatwa na kuwekwa rumande na kupigwa sana kiasi cha kupoteza jicho moja sasa yuko nje kwa dhamana pamoja na wenzake hawajafunguliwa kesi ya ugaidi. Huyu Juma Abdallah Kheri kubwa alilokuwa nafanya ni kuwalipa waalimu wanaosomesha Qur'an katika madrassa mbali mbali za vijijini. Hili analifanya kwa kutegemea malipo kutola kwa Allah na si jingine.
|
No comments:
Post a Comment