[QUOTE=CattleRustler;9628162]Kama wewe ni muislam na uamimi kama watu walichakachua pesa ya kujenga hicho chuo basi ndio unaudhihirishia ulimwengu kama amuthamini elimu kwasababu nazani kilitakiwa kiwe ndio chuo pekee kikubwa. Kama ungekuwa unafatilia maendeleo ya waislam ungelifahamu hili na ndio naamini mlipiga makelele kuhusu kuvunywa msikiti wa magomeni ili kupanua barabara wakati amujui watu walichakachua ela ya kujenga chuo.[/QUOCeE]
CattleRustler,
Inaelekea hujui historia ya EAMWS na ujenzi wa Chuo Kikuu.
Chuo hakikujengwa tena baada ya Nyerere kuivunja jumuia hiyo na
Sheikh Hassan bin Amir kufukuzwa Tanganyika kurudishwa Zanzibar.
Mradi hakufikia ngazi hata ya kulipwa mkandarasi kwa hiyo hizo fedha
hazikuja.
Mkandarasi wa chuo ilikuwa kampuni ya Kimisr ikiitwa Al Nasr.
Ofisi zake zilikuwa Mtaa wa Jamhuri mwisho inapokutana na Mtaa
wa Azikiwe.
Zingekujaje ilhal mteja EAMWS ilikuwa ishavunjwa tena kwa amri
ya serikali?
Kilichokuwa kinaogopwa na Nyerere na Kanisa Katoliki ni kwa Waislam
kujenga chuo na hivyo kuelimika.
Isingewezekana kwa BAKWATA kuachiwa wafanye lile lililokusudiwa
na EAMWS kwani BAKWATA iliundwa ili kuua ujenzi wa chuo.
Miaka michache iliyopita nilikuwa New York na jamaa zangu pale
waliniomba tuswali Ijumaa katika msikiti mkubwa wa New York kisha
twende tukale pamoja na wakanambia kuwa kulikuwa na jamaa kutoka
Misri alitaka kukutana na mimi.
Huyu jamaa wa Kimisr alifanihamisha kuwa yeye wakati wa mgogoro
wa EAMWS alikuwa katika Ubalozi wa Misri Dar es Salaam na alikuwa
ndiyo ''coordinator'' kati ya EAMWS na serikali yake.
Huyu jamaa anasema hakujua fitna iliyopitika hadi aliposoma kitabu
cha Sykes.
CattleRustler,
Ukweli wa ujenzi wa chuo hicho ni huo.
Hakuna fedha zozote zilizofanyiwa ufisadi.
Sunday, 25 May 2014
KUTOKA JF: EAST AFRICAN MUSLIM WELFARE SOCIETY NA UJENZI WA CHUO KIKUU CHANG'OMBE
About Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment